Watanzania ndivyo tulivyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ndivyo tulivyo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by howard, Mar 19, 2011.

 1. howard

  howard Senior Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  JAMANI LEO NILIKUWA NAANGALIA MNET STAR CHANNEL MOJAWAPO KWENYE DSTV KUNA KIPINDI NIKAKUTANA NACHO KINAITWA "STAND UP COMEDY LIVE FROM MOMBASA"KUNA COMEDIAN MMOJA MKENYA ALIKUWA ANAONYESHA UTUNDU WAKE.AKAANZA KWA KUELEZEA HULKA NA TABIA ZA WATU WA NCHI MBALI MBALI, AKAILELEZEA JAMAICA WATU WAKE NA HULKA ZAO, AKAINGIA KENYA NA AKAIGUSA TANZANIA,AKATOLEA MFANO KWAMBA NI SIKU YA HUKUMU KWA ULIMWENGU WOTE NA WATU WA MATAIFA MBALI MBALI WAMEJAA, HUKUMU IKAANZA NA WATU WA KENYA, AKAITWA MWANANCHI WA KENYA AKAAMBIWA NA MALAIKA WEWE NENDA KULE JEHANAMU KWENYE MOTO MKENYA AKAANZA KULETA UBISHI ANATAKA KUJUA KWA NINI ANATAKIWA AENDE KULE, WANABISHANA NA MALAIKA, ANASEMA HAO NDIO WAKENYA JINSI WALIVYO HAWAKUBALI MAMBO KIRAHISI RAHISI TU, AKAINGIA TANZANIA, AKASEMA HAO NI WAPOLE SANA NA KILA KITU NDIO MZEE KWAO HUKO, BASI MALAIKA AKAMWITA MTANZANIA AKAMWAMBIA WEWE ELEKEA KWENYE MOTO KULE, MTANZANIA KWA UPOLE AKASEMA SAWA MALAIKA NJIA IKO WAPI, AKAONYESHWA AKAWA KWA SHINGO UPANDE ANAELEKEA KWENYE MOTO AKAFIKA NA MARA MTANZANIA AKARUDI KWA MALAIKA AKAMWAMBIA MALAIKA KUNI ZIMEKWISHA NAOMBA UONGEZE KULE, NA WAKATI ANAFANYA HIZO MOVEMENT ZAKE ETI MKENYA BADO ANABISHANA NA MALAIKA KAGOMA KWENDA ANAJITETEA, KWA HIYO ANAJARIBU KUSEMA KWAMBA WAKENYA SI WATU WA KUKUBALI KILA KITU LAKINI WATANZANIA WENYEWE HATA KAMA WANADHULUMIWA HAKI ZAO WAO NI NDIO MZEE.
  MY TAKE:
  Iliniuma sana nikajiuliza hivi ndivyo tulivyo kumbe na majirani zetu wanajua hili
  Wazee wa jamvini hapa naomba mtazamo wenu kwenye hili. nawasilisha
   
 2. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hiyo ni typical overgeneralization na usikubali watu wengine waku-define na ukaingia kwenye mtego wao.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa!tujiulize tangu migodi ya dhahabu,almasi,tanzanite,almasi imeanza kuchimbwa na wawekezaji imetusaidia nini watanzania?mchango wa viwanda vya sukari ni mkubwa kwa wananchi wanaozunguka mashamba kuliko hata hiyo migodi,kila siku tatizo la umeme haliishi na tumekaa kimya!waziri ngeleja anadanganya bunge kiwira imechukuliwa na serikali kumbe ipo mnadani hatujamshughulikia
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  ni kweli watz ni wapuuzi kikweli kila kitu ndio mzee. Hamna issue, hata tunakaa gizani tunasema ndio mzee kama wase****nge vile. Hata tembea yenyewe tu utajua ni mitz . Hate mpaka basi . Amkeni you have nothing to loose yoo......
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kutambua haki zetu za msingi na kuzidai iwe ni #1 priority. Lakini shida inakuja watu wakifanya hivyo, basi inaingizwa karata ya udini na wananywea
   
 6. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Siyo kweli, Wapole hawaendi motoni "Heri wenye upole kwa maana watairithi nchi, Matt. 5:5"
   
 7. howard

  howard Senior Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Upole wenyewe sio siku ya hukumu mkubwa upole ni hapa duniani hapo ndio utairithi nchi, na inakuwaje uwe mpole wakati unajua haki yako inaporwa au ndio samehe saba mara sabini?
   
 8. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kimantiki ni kweli na ndo maana wanataka kwa haraka muungano wa EAC
   
 9. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ufalme wake si wa dunia hii. Je tuache upole kwa sababu CCM inatunyanyasa? La hasha sisi tutaendelea kuwa wapole na mafisadi watapata malipo yao kama siyo hapa duniani basi inayokuja.
  Tunaweza kupambana na udhalimu na ufedhuli wa CCM bila kupoteza upole wetu, Dr. Slaa na CDM wameonyesha hiyo inawezekana pale NEC ilipotangaza matokeo tofauti na yaliyopigiwa kura.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,138
  Trophy Points: 280
  Sasa kutuandikia na hiyo mi herufi mikubwa (capital letters) ndio nini? Au mwalim wako hajakufundisha hutumika vipi hizo?
   
Loading...