Watanzania nane waliokabiliwa na kesi ya ujasusi, nchini Malawi wameachiwa huru

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_95628512_malawi1.jpg

Watanzania wanane waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ujasusi, nchini Malawi wameachiwa huru jana na sasa wapo njiani kurejea nchini Tanzania .

Hukumu ya kesi yao ilitolewa jana jioni tarehe 12 mwezi Aprili mwaka huu,Watanzania hao waliokuwa wanashikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani uliopo eneo liitwalo Kayerekera.

Serikali ya Tanzania ilikataa kwamba Watanzania hao walitumwa na serikali ili kufanya shughuli za kijasusi katika mgodi huo wa urani. Tanzania iliongeza kwamba watu hao walikuwa ni wafanyakazi wa Taasisi ya misaada ya Caritas iliyo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Songea mkoani Ruvuma.

Wakili aliyekuwa anaisimamia kesi hiyo ,Flaviana Charles ameiambia BBC kuwa watu hao kwa sasa wako huru pamoja na kuwa wamepitia katika magumu mengi na ya kukatisha tamaa lakini kila kitu kilikuwa wazi na upande wa walalamikaji hawakuwa na ushaidi wa kutosha wa kuwafunga kwa kuwa watanzania hao waliingia nchini humo kihalali kuanzia mpakani na walikuwa na mualiko na wakati wanawakamata walikuwa hawajafika mgodini bado maana walikamatwa wakiwa wanatoka hotelini hivyo hawakufika mgodini au kuhoji mtu yeyote hivyo shutuma zao zilikuwa zenye mashaka sana.

_95630459_590eef0d-3633-4706-973b-c6ed1e2f35b7.jpg

Je,kuna fidia ambayo wamelipwa baada ya kuwekwa kizuzini tangu mwezi desemba mwaka jana?

Wakili Flaviana amesema kuwa kuna ujanja ambao mahakama imeutumia ili kukwepa fidia kwa kudai kuwa ambayo wameshatumikia kifungo kwa kipindi hicho chote watuhumiwa hao walipokuwa kizuizini hivyo kwa sasa wako huru.

BBC imezungumza pia na baadhi ya watu hao waliokuwa wanatuhumiwa,,wanasema wana furaha sana maana walikuwa wameenda Malawi kwa matarajio ya kukaaa siku 3 lakini sasa wamejikuta wamekaa zaidi ya miezi mitatu,bila kujua kinachoendelea katika familia zao pamoja na shughuli zao za kila siku

wamesema walikuwa wakiteseka bila sababu ilhali nia yao kwenda Malawi ilikuwa njema kabisa .

Watanzania hao nane,wanashukuru sana serikali yao ya Tanzania haswa kwa balozi kufika kuwaona.

Chanzo: BBC Swahili
 
Alafu......
Kwanini hawajasema kilicho wapeleka huko Malawi?
Zaidi wamesema eti waliingia kihalali na walitarajia kukaa siku tatu tu tena wakiwa na nia njema..
Alafu.....
Sisi watanzani sijui nani alituroga...
Yaani mtu amekaa gerezani kwa zaidi ya mizi mitatu, alafu anatoka kwa juhudi za mwanasheria alie simamia kesi...... Kisha anapo toka kwa kutokukutwa na hatia na huku alie mshtaki akiwa hana ushaidi ulio jitosheleza..... Hapo mtu huyo anae achiwa kwa haki kabisa, anatoka na kuishukuru serikali ya nchi yake...... Ilhali serikali yake ilimkana...
Aaagggghhhhhh.......
Ebu ngoja niishie hapa, maana naona nazidi kukasirika tu
 
Kuna unachokitafuta,
 
Kwanini Mkuu....
Kama kuuliza maswali na kutoa maoni ya mawazo hiru ni kosa.....
Basi samahani....
Tumechoka kusikia watu wanapotea mazingira tatanishi,

Usijione uko huru sana kuongea , nchi sio yako hiii,

Kamwombe samahani dereva wa Lori
 
Alafu......
Kwanini hawajasema kilicho wapeleka huko Malawi?
Zaidi wamesema eti waliingia kihalali na walitarajia kukaa siku tatu tu tena wakiwa na nia njema..
Alafu.....
Sisi watanzani sijui nani alituroga...
Yaani mtu amekaa gerezani kwa zaidi ya mizi mitatu, alafu anatoka kwa juhudi za mwanasheria alie simamia kesi...... Kisha anapo toka kwa kutokukutwa na hatia na huku alie mshtaki akiwa hana ushaidi ulio jitosheleza..... Hapo mtu huyo anae achiwa kwa haki kabisa, anatoka na kuishukuru serikali ya nchi yake...... Ilhali serikali yake ilimkana...
Aaagggghhhhhh.......
Ebu ngoja niishie hapa, maana naona nazidi kukasirika tu

Mkuu, ni lini serikali iliwakana hawa wenzetu wakati balozi alikuwa akiwatembelea huko jela?
 
Back
Top Bottom