Watanzania na ulimbukeni wa mpira na mitandao ya kijamii

changaule

JF-Expert Member
Jan 10, 2020
5,587
9,179
Watanzania tumekuwa na tabia ya ajabu sana ya kiherere na kuonesha hali ya upumbavu na ujinga katika mitandao ya kijamii. Tabia tunayoinesha sio kwamba ndio tunaujua sana mpira kuliko mataifa mengine ya Africa, bali tunaonesha ndio wapumbavu na wajinga kuliko mataifa mengine Africa.

1) Tabia ya kulalamika kupostiwa postiwa ni swala la ajabu mno, kupostiwa hakuifanyi timu iwe kigogo zaidi ya kuucheza mpira uwanjani na kuchukua kombe.

2) kujisifu kwa kupostiwa nalo ni upuuzi, wanao tawala soka la Africa wakipostiwa huwezi kuona shangwe, wala tambo wala comments nyingi ila sisi watanzania tu ndio bado tuna ushamba mwingi na mambo ya CAF.

3) ku comment vitu visivyoendana na content. Mara nyingi sana CAF wanapo tweet habari inahusiana na mchezaji au timu za kariakoo basi tegemea page kuchafuka kwa kila aina ya uharo. Hakuna anayetoa fact, au kwendana na content zaidi ya kuandika upuuzi mwingi mno. Juzi ilipostiwa nani anastahili kuwa kipa wa decade wakapost wanaowania ila cha ajabu mtu anajiropokea tu Manula, Manula.

4) Tabia ya kuvamia kwenye page za timu ambazo unakutana nao kwenye mechi inayofuata na kuandika upuuzi na tambo nyingi. Hii tabia ilianza tokea zamani sio msimu huu.
 
Mbona unafoka foka hovyo! Kumetokea nini tena?
.
IMG_20220923_115506.jpg
IMG_20220923_115822.jpg
 
Asante kwa kuliona hilo. Tabia kama hii ilisababisha kijana wetu Samatta akatemwa na Aston Villa (hata kama kuna sababu nyingine pia). Jitu linaibuka tu from nowhere na kuwatukana teamates wa Samatta ati hawampi pasi na matusi mengine lukuki, tena kwenye page za mitandao ya kijamii ya timu yao.
 
Ni kweli Aston villa walikwazwa na matusi kwenye page yao mbaya zaidi hakuna mtu alijotokeza kusema hilo, sasa hivi utakuta page za opponents wa timu hizi mbili (CAF) zimejaa matusi ya ajabu siku Simba wamecheza na Orlando pirates nliangalia page yao aisee mpka aibu
 
Hasa mashabiki wa yanga ndio maana Morrison aliwaambia waende shule.
 
Uki postiwa unapata nini?
Yapo mengi sana ila kwa uchache tu unapo postiwa unapata covarage pana ya kuongeza mashabiki na kujulikana worldwide kwasababu page ya caf inetembelewa na sehemu kubwa sana ya familia ya soka ulimwenguni.hivyo basi ni rahisi kuuza product za club kama jezi,wachezaji,kampuni kubwa kuwekeza kwenye club n,k.
 
Football na hooliganism huwezi kuvitenganisha. Hizi teams za EPL nazo mashbiki wake pia ni hooligans.

Unaweza kumkuta mtu ana PhD lakini akiwa mpirani, wote hatujaelimika.
Msio mashbiki ndio mnaleta stress zenu huku. Mashbiki huwa hawjali hayo.
 
Asante kwa kuliona hilo. Tabia kama hii ilisababisha kijana wetu Samatta akatemwa na Aston Villa (hata kama kuna sababu nyingine pia). Jitu linaibuka tu from nowhere na kuwatukana teamates wa Samatta ati hawampi pasi na matusi mengine lukuki, tena kwenye page za mitandao ya kijamii ya timu yao.
Mkuu kuna watu walikuwa wanaenda dm za Grelish kule insta na kumtukana,halafu ndo captain wa Aston villa wakati huo,watanzania wamekuwa washamba kwenye mitandao,unakuta mchezaji hajacheza vizuri basi wataenda kumfuata kwenye comments wamtukane,ndo maana watu kama kina Bocco wanafunga comments zao ,kila club ya bongo inapocheza na wengine lazima wahamie kwenye hiyo page .
 
Kwakweli tuna generation ya mashabiki washamba sana. Sijawahi kuona vijana wa nchi nyingine wakifanya huo upuuzi.
 
Back
Top Bottom