Watanzania na Paypal

Classic 1

Senior Member
Sep 11, 2021
113
111
Mengi na wengi wameshazungumza sana na kuandika sana kuhusu umuhimu wa huduma ya Paypal kwa nchi yetu.

Ajabu, kila kampuni mpya ya Fintech inakuja almost inafanya kama yule mwenzake hakuna aliyethubutu kwenda extra mile. Wanaigana na kuzunguka hapohapo kila siku. Hivi huwa wanasoma reviews na comments na kuelewa customers & prospective customers wanachohitaji ? Swala la Paypal limekua ni kilio cha online entrepreneurs na diasporas kwa muda mrefu but nothing has been done so far.

Watu huko nje wanatushangaa na kutuona wa ajabu tena waajabu sana, how comes mpaka Karne na miaka hii hakuna huduma Kama Paypal , stripe, etc. Yani ni one way service. Unaruhusiwa kutuma ila huruhusiwi KUPOKEA. Ajabu! Maana yake, just be a consumer!

Halafu tunasema dunia imekuwa Kijiji changamkieni fursa.
They can't think beyond WU & MG.

Ni wakati sasa japo tumechelewa, ministers wa sector husika na CEOs wa FinTech companies ku-step in.

Ngoja niishie hapa ila acha nikope maneno ya Ronald Reagan
Mr..... come, Open the gate &
Tear down this wall!
 
PayPal ndo nini? Toa kwanza elimu ya nadharia unayoizungumzia! Vinginevyo unajizungumzia mwenyewe hakuna anayekuelewa
 
PayPal ndo nini? Toa kwanza elimu ya nadharia unayoizungumzia! Vinginevyo unajizungumzia mwenyewe hakuna anayekuelewa
Ungechukua hata a minute ku-Google au ku- search hata hapa JF kuna threads kadhaa zimeshatoa hiyo "elimu" unayotaka tena kwa kiswahili miaka kadhaa iliyopita. So, sihitaji kuwapotezea muda wasomaji wanaojua ninachosema. SOMA paragraph ya kwanza sijaandika hivyo accidentally. Jiongeze japo kidogo tu, tutaenda sawa.

NB: Wanaonielewa wapo tena wengi tu.

This thread is not the beginning and is not even the end. We just keep on reminding them.
 
Poleni vijana ushauri wangu ni ule ule siku zote , kamata fursa timkia majuu.

Uzalendo sio kuishi nchi uliyozaliwa wala kuipenda serikali iliyopo.

Wezi wapo huko Tanzania na wanatajwa kwenye report za CAG kila uchwao na wapo ofisini kinachofanyika ni badala ya kuwaweka nyuma ya nondo wanahamishwa ofisi tu.

Uzalendo sio kuiibia nchi wala sio kuipenda na kuisifia serikali iliyofeli.

Hebu jiulize mnasemaje mnae waziri wa masuala ya ICT asiyejua chochote hadi anakataa dili la nchi kuwa na internet yenye kasi kama ya Starlink?

Fursa mtakazoshindwa kuzipata huko mnafanyiwa hisani huku ulimwenguni ni mahitaji muhimu ya kila siku mtu kujikwamua kiuchumi.
 
Back
Top Bottom