Life2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,377
- 4,847
Hii kasumba ipo sana miongoni mwa Watanzania, zamani ilikua ni kwenye vijiwe vya kahawa.
Hatimaye imekua Kansa sugu, taasisi za kidini, vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi, viongozi wakubwa wa nchi wastaafu na wasasa, vijana, wazee, Radio na hata mitandao ya kijamii.
Kwa sasa ni kitu cha kawaida maovu kutetewa kwa nguvu kubwa mnoo, je tatizo ni umaskini wetu au?
Ukitaka kupendwa kwa sasa Tanzania wewe tenda maovu.
Iba kura
Piga watu wasio na hatia risasi
Teka na poteza watanzania
Wape ndugu zako vyeo kiharamu.
Finya haki za wafanyaki.
Kamata wapinzani weka ndani bila kesi
Sema uwongo uwongo...nk
Ukiwa shujaa wa hayo mambo zitajitokeza taasisi za dini zitakutetea, watakuja viongozi wa dini watasimama na wewe na wengine hata kutishia kuchinja wenzao, watasimama vyombo vya usalama watakutetea, kabla hakujapoa watakuja wana siasa, wanamichezo, machawa Pro max, vyama vya bodaboda, bajaji, Tax, na mbaya zaidi hata wanasheria na wao watakutetea.
Hivi ni kwamba watu wanakua hawafahamu ukweli au ni kujizima data tu haiwezekani dunia nzima wanasema flani muovu halafu wewe kutwa kucha kuwatetea.
Ni lini hii kasumba itakwisha na watanzania kuzungumza ukweli na kuacha kutetea maovu?
Kama wewe ni mmoja wao hebu badilika ili hata siku ukifa uwache historia nzuri duniani na si watu kuanza kushangilia kifo chako.