Utafiti WHO umeonesha 87%
ya watanzania wanakunywa pombe za
kienyeji, Dar, K'njaro zaongoza kwa
wanywaji wengi wa pombe hizo
Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa
wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu
wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa
zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo
kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.
Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza
kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana
wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia
shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali
inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili
na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.
Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu
mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili
Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene.
Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari
za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa
na chama cha waandishi wa habari wanawwake
‘TAMWA’.
#jamboLEO