"Watanzania milioni 39 wanakunywa mataputapu"

Betason

JF-Expert Member
Feb 2, 2015
352
584
Utafiti WHO umeonesha 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, Dar, K'njaro zaongoza kwa wanywaji wengi wa pombe hizo

Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06. Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.

Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene.Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawwake

‘TAMWA’.

#jamboLEO
 
Uwongo mtupu, wala uhitajiki kuwa msomi kujuwa hizi ni takwimu za kupikwa mezani pesa za fied watu wanaingiza matumboni mwao.
 
Ha ha haaaaa!!! Hakuna shida. Kumbe tuko wengi hivyo!! Nikadhani ni Rombo tu.
 
Utafiti WHO umeonesha 87%
ya watanzania wanakunywa pombe za
kienyeji, Dar, K'njaro zaongoza kwa
wanywaji wengi wa pombe hizo

Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa
wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu
wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa
zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo
kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.
Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza
kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana
wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia
shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali
inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili
na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.

Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu
mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili
Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene.
Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari
za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa
na chama cha waandishi wa habari wanawwake
‘TAMWA’.

#jamboLEO
Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni, Milioni 39.06 kati ya Milioni 44.9 ya watanzania wanakunywa pombe!??. Mbona idadi inatisha mno?
 
Hakuna vinywaji viletavyo Afya kama mataputapu maana yale yamepikwa kiasili zaidi bila ya kukoboa nafaka.

Tatizo lake Ukienda Kunya.
 
ukweli ni upi mkuu? ebu tujuze
87% ya Watanzania wanakunywa mataputapu, sasa tukiongeza na asilimia ya wanaokunywa bia si jibu litakuja Watanzania wote ni walevi? Au hulioni tatizo hapo?

Yaani 13% ya Watanzania ndio humo wamo wasiotumia kilevi na wanywa bia? Hii nchi ilipofikia sijui hata nani wa kumuamini, maprofesa hovyo madoctor hovyo yaani ni shidaaa.
 
Nadhani alimaanisha kuwa 87% ya wanaokunywa pombe wanakunywa mataputapu,ina maana asilimia 13 tu ndio wanakunywa pombe za viwandani.
 
Nadhani alimaanisha kuwa 87% ya wanaokunywa pombe wanakunywa mataputapu,ina maana asilimia 13 tu ndio wanakunywa pombe za viwandani.
hata mm nafikiri hivi lkn bado ni % kubwa sana..nadhani hii sheria ya kufungua baa saa kuanzia saa kumi jioni litasaidia kupunguza hizi %
 
Hiyo ndiyo asili yetu Waafrika, mbona mababu walikunywa hizo hizo na wakaishi hadi karne.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom