Wateule
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 390
- 368
KAKA UNAONGELEA,HAKI GANI?KATIBA IPI?HII ILOFUNGWA SANDA?KATIBA HAIFUATWI WALA KUHESHIMIWA NA WATAWALA,UTAPATA HAKI GANI?NAKUOMBA JITAFAKARI WW MWENYEWE UPO KUNDI GANI?LA MJINGA AU MPUMBAVU NI HAYO TU.
Katiba hiyohiyo ambayo CCM hawaiheshimu na kuikanyaga kila siku kuna haki tulani wewe imekupa. Kwa mfano, haki ya kutoa taarifa polisi ndani ya siku kadhaa ili upewe ulinzi wakati unafanya maandamano ya amani kuishinikiza serikali kutekeleza wajibu wake kuhusu suala fulani. Haki hii anatokea mtu mmoja na kikundi chake anasema usiandamane na kuamuru polisi wake na wanajeshi waanze mazoezi mtaani. Wewe ukiona hivyo, unaona isiwe taabu, unaufyata na kujifungia nyumbani. Unategemea hiyo haki atakuletea nani kwenye sahani ili hali umeshaona wanaotakia kutoa haki ni dhalim? Hapa sikulaumu wewe Mtanzania mfuasi muoga tu, bali nawalaumu sana viongozi waoga pia, ambao wanaitisha "UKUTA" leo, halafu kesho wanakuja na visingizio vingine. Siku tutakayopata upinzani makini, ambao upo tayari kutangaza mgomo na kuusimamia mgomo huo mpaka unatekelezeka bila kujali hila na vitisho vya mtawala dhalim, basi tutafika. Lakini, kama uoga huu na uzembe huu utaendelea, tutarajie CCM kuendelea kutawala miaka mingine mingi tu!