Watanzania kimpira nani katuloga???

Heh, kilimo sijui kwanza, mmeshindwa, utalii, mnagawa na kuiba Twiga huku mkifanya magendo ya pembe za ndovu, uchumi mmewaachia wachina tena wafungwa, ufugaji ndo kila kukicha vita ya wakulima na wafugaji, ubondia ndo Cheka anapigania mkanda usotambulika, madini ndo Kenya ya kwanza kuuza TANZANITE duniani, soka ndo kwanza hata wimbo wa taifa wachezaji hawawezi hata kuuimba. Siasa, kila kukicha ni Chadema vs CCM........., tena majukwaani na mtandaoni, mtaweza nini nyie?

# teamentreprenur

Yaani mkuu Genekai mimi nashindwa hata kuelewa sisi tunaongoza ktk lipi sasa. Au taarabu?
 
Kuna makala nimewahi kuiona hapa JF imeandikwa na somebody Kumwembe ningependa mtu aiweke hapa ili ndugu yangu @MIDFIED aisome.

Twalalamikia mpira kwani tumefanikiwa katika lipi? Je kila mtu ametimiza wajibu wake kufanikisha siku Tanzania iwe na timu bora au ndo lawama tu kwa huyo Ngassa na wenzake?

Hapana mkuu siyo lawama ni haki yetu kabisa kuhoji utendaji wa timu yetu kwani kufanikisha kwangu ili timu yetu ifanye vizuri kwa nafasi niliyonayo na Watanzania tulio wengi ni mambo makuu mawili:
1. Kuchangia kwangu ninapoingia mpirani, kile kiingilio kintumika ktk maendeleo ya mpira.
2. Kuishangilia timu yangu inapocheza ni mchango mkubwa sana kisaikolojia kwa wachezaji kuweza kufanya vizuri na
3. Michango wanayopata kupitia wadhamini mbalimbali, viwanja n.k. ni kodi zetu wananchi

Hivyo ni wajibu wao kucheza kwa kujituma ili kutuondoa ktk aibu ya kufungwa kila mwaka hakuna tunapofika. wadau wengine wenye nyongeza ktk haya wanaweza kunisaidia
 
Tuache "politiks" kwenye mpira.

Tufike na kusema na kufanya kwa vitendo kwamba mpira ni
"business" kama zilivyo biashara zingine.

Iwe kama biashara zingine ambazo zinasimamiwa na sera, sheria na kanuni madhubuti.

Tanzania tunazalisha vipaji vingi sana akina "Messi" na "Ronaldo" wengi sana lakini bahati mbaya mfumo tulio nao wa soka ni wa kienyeji mno ambao haujui kutunza na kulea vipaji.

Vipaji vinavyokuja kujitokeza kwenye Timu zetu za wakubwa ni kama kuku wa kienyeji waliojitafutia na kusimama wao wenyewe.

Tutaishia tu na "politics" zetu za magazeti ya michezo na kurasa za michezo, tambo zetu siku Simba na Yanga zikicheza, misuguano ya kugombea uongozi TFF, vilabu vikubwa, vyama vya waamuzi, marefarii, kimsingi "business as usual" .

Tutapeana matumaini yasiyotimilizika basi muda unakwenda wanakuja na kuondoka na wanakuja na kuondoka wanakuja na kuondoka hamna chochote cha maana cha kujivunia kwenye medani ya soka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom