Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,583
- 27,838
Nimejaribu kufanya tathmini yangu kuhusu jamii yetu nimegundua kwamba kuna matatizo mengi sana ambayo mengi chanzo chake ni kukosa mapenzi ktk kwa Wazazi utotoni.
Watanzania wengi wanalelewa bila mapenzi na upendo, wengi hata hawakupata muda wa kuwa watoto, wengi Wazazi wao walikuwa ni Wakatili kwa maana ya kupigwa na kuadhibiwa na Wazazi bila ya huruma, kuna Wazazi wanapiga watoto mpaka wanavunja viungo vya mwili, na hii ndo sababu au moja ya sababu kwa nini sisi kama jamii hatujithamini na tunaamini tunastahili kupata shida na siku zote tunawapendelea wageni, tuko radhi tulale chini lkn mgeni alale kitandani kwa maana tumelelewa na kukuzwa kikatili hata tumeuukubali ukatili wa Wazazi na kuona ni kawaida.
Na hawa Wazazi wanaopiga Watoto pia na wao walilelewa hivyo bila ya mapenzi na upendo.
Kuna Kaya nyingi Mzazi akisafiri Watoto wanafurahia, na siku akikaribia kurudi Amani kwa watoto inatoweka, nimeshakutana na Wasichana walioamua kuolewa mapema ili mradi tu wawakimbie Wazazi na kutoka nyumbani.
Jamii yetu ya TZ hatuwapendi watoto wetu, unakuta mzazi anampeleka mtoto wa miaka 5 boarding school sasa haumkumbuki mtoto wako? Kama kweli unampenda kwa nini umpeleke akalelewe na wengine?
Wazazi wa TZ leeni watoto wenu kwa upendo na Amani, msiwapige na kuwa wakali kupitiliza, wacha mtoto wako akuone rafiki na siyo adui, Watoto wa TZ wanakuwa wakiwaogopa Wazazi hata kama akiwa na tatizo hawezi kujadili na Mzazi wake kwa maana anamuhofia matokeo yake anakuwa na tatizo, sasa kama hawezi kujadiliana na Mzazi wake akajadiliane na nani tena Dunia hii? Mwishowe tunakuwa na jamii iliyo na watu wasiojithamini na hata wasioelewa maana ya Upendo, ...