Deacons to close shop in Tanzania over endless losses
The cost of rental space in Tanzania is $40 dollars compared with $18 dollars per square foot in the rest of the region.
Tanzania's middle class make up just 12 per cent of the total population, which is far much smaller compared with Kenya's 44.9 per cent and Uganda's 18.7 per cent of the population. Rwanda's middle class is at 7 per cent its population."The cost of doing business in Tanzania is 30 to 40 per cent higher compared with other markets. The middle class is also not as big and the uptake of our brands was also not as big," said Deacons chief executive Muchiri Wahome.
Dar es Salaam, Tanzania's Capital, only boasts of two shopping malls. In contrast, Nairobi, Uganda and Rwanda are experiencing a boom in the construction of malls and hence rapid growth of the shopping mall concept.
Also, long supply chain in Dar es Salaam is a challenge, where it can take up to five times longer by air to clear and deliver goods compared with the rest of the region.
..............
...............
...........................
Pinpoint investment Ltd (12.06 per cent), Charles Mwangi Gathuri (11.04 per cent) and Diana Bird (11.03 per cent) are the other main shareholders of the publicly traded firm, which hopes to list its shares on the Nairobi Securities Exchange later this year.
yaani mitumba ndio symbol ya kuingia kwetu kwenye utandawazi na kumetugharimu sana maana viwanda vyote vya nguo vimekufa bila sababu ya kueleweka. Hivi tunajua kwamba lethoto inauza nguo nyingi sana nje kuliko tanzania? Tunalima pamba na tuna viwanda vingi vya nguo. Badala ya kuendesha textile industry kutoka kwenye kulima, mpaka kutengeneza na kuuza nguo, sasa hivi biasharta njema ni kufuata nguo china na far east. Wachina wamegeuza urafiki sijui godown au sehemu za kulala wakitoka kufanya uchuuzi kariakoo. Mwatex, na kwingineko kumesambaratika jumla. What a good country!
Hii ndio sababu wawekezaji wanaokuja hapa wanajisubject kama risk takers kama kwenda Afghanistani, Kongo, Irak na labda Somalia. Matokeo yake wawekezaji wazuri hapa ni dizaini ya DOWANS na MEREMETA. Hatupati wawekezaji walio serious sana on long term basis na sio ajabu hata makampuni ya madini yanatoa kidogo as they are not certain with the future.
Suala la rent, mwekezaji mmoja alikuwa tayari amesign mkataba na Mlimani city Mall lakini alivyoangalia uhalisia wa vitu alivyotaka kuuza akaamua kuachia mwenyewe maana aliona wazi kwa gharama ile biashara isingewezekana kutengeneza faida katika mazigira ya ukweli.
Alafu kitu ambacho sikujua ni kuwa kwa Tz middle class income ni 12%, hii ina maana high income (naomba kukosolewa) ni kama >2% ya Watz. Kwa maana hiyo lower income (wanaoishi >$1 per day) ni zaidi ya 85%! ambapo kwa Kenya nadhani inaweza kuwa >30%. Hapo ndio ujue kuwa sisi ni fukara kiasi gani pamoja na rasilimali tulizojaliwa. Ndio sababu concept ta 'supermarkets' inakuwa ngumu kwa mswahili wa kawaida huku tukiendelea kuamini kuwa ni ya 'wazungu'!
Kwenye supply chain hapo kila kitu ni nani anamjua nani na kwa walivyoandika kuwa kama unaweza kufanya clearance ya mzigo bandarini/airport kwa siku moja Kenya/Uganda, Tz ni siku tano na kana ratio itakuwa siku 3 basi hapa ndio siku 15! Hapa kuna 'wazee' TRA, utadhani hawa 'matajiri' wa nchi hii hawaishi hapa kwa jinsi wanavyorelax wakati mizigo ya wafanya biashara ikiongeza demmurage na storage charges!
Kwa hakika mfumo wetu ni mbaya sana na wote tunajua lakini wanaofaidika nao ni wale walioko kwenye sysytem. Matokeo ndo kama haya, wawekezaji ambao tunatumia gharama kuwaita wanaondoka!
mkuu, pamoja na tatizo la rent, suala la serikali kubuni sera za kupanua hii middle class ni la muhimu sana.Tukiendelea na huu utaratibu wa ajabu sana wa kulipia kwa mwaka tutajikuta hatuna wawekezaji kabisa, na watu wengi sana wanashindwa kufanya biashara kwa sababu ya rent kuwa juu sana na ya kulipia kwa mwaka mzima,
umeongea vizuri mkuu na hapo kwenye red umemaliza kila kitu hasa underline!Swala la supermarkets Tanznaia ni geni sana kwa watu wengi labda wale wa zamani walioziona COASATA na STC (Saidia Tujenge Chetu) na ambao wametembea sana nje ya nchi. Baada ya COSATA kutaifishwa na kufanywa STC, STC ilikufa na badala yake yakatokea maduka ya kila nyumba. Ndiyo maana Tanzania kumejaa "mafremu" kila mahali, mpaka Osterbay na Masaki. Watanzania hata wale wenye kipato cha kati (Middle Income) hawana utamaduni wa kununua kwenye "supermarkets". Aliyeandika kuwa sababu ya watu kutonunua "supermarket" ni "low percentage" ya "middle income group" anaweza kuwa hajalifahamu tatizo vizuri. Botswana ina watu millioni mbili lakini karibu kila mtu anaishi kwa kwenda "supermarket" ambako unanunua hadi mchicha. Hata viduka vya mitaani vinapata bidhaa zao supermarket. Ndiyo maana ukiwa Botswana ni nafuu kununua "supermarket" kuliko mtaaani. Kwa Tanzania, kwa ujumla, ni kinyume.
Kama middle income ya Tanzania ni 12% hiyo ni sawa na kusema watu karibu millioni tano. Kama ni 5% ni sawa na watu millioni 2, yaani idadi ya watu wote wa Botswana. Kama watu wote wangenunua supermarket basi supermarket zingestawi kuliko Botswana ambako kumejaa "Shopping Malls, supermarkets and hypermarkets".
Kilichoua viwanda vyetu vya nguo ilikuwa ni siasa mbaya - Ujamaa, siyo liberalization. Kwa wenye kumbukumbu nadhani wanakumbuka kuwa alikuwa ni Salim Ahmed Salim wakati alipotembelea Mtwara aliruhusu mitumba iletwe Tanzania baada ya kuona watu wakitembea bila nguo. Tukumbuke tena kuwa kuna wakati watanzania walikuwa na shida sana ya nguo na wengine walitembea uchi! Sipendi kuzikumbuka siku zile kwani huko vijijini watu khanga na kitenge zilikuwa ni "tie-and-die" tu na sisi wa mjini tulikuwa tunavaa tacron za Msumbiji. Chupi zilipotea kabisa. Watu tayari walikuwa wameshaanza kuiba mitambo ya viwanda kama Kilimannjaro Textile na Sunguratex.
Serikali ya leo ina wajibu wa kutunza viwanda vyetu vya nguo, vya serikali na vya watu bianfsi. Kuna wengi wanataka Mwatex na Urafiki vifanye vizuri. Ukweli ni kuwa viwanda licha ya kutomudu ushindani wa bidhaa kutoka nje vinashindwa kupambana na viwanda vya binafsi vilivyopo Tanzania. Kiwanda cha Urafiki ikiwezekana kiuuzwe tu - lakini mafisadi watapeana wao kwa wao, bureeeeee!
Mpaka leo sielewi ni kwa nini watanzania wanashindwa kutumia cherehani kushona nguo na kuilazimu nchi kuagiza bidhaa hizo nje hata kama ni sare za shule.
Swala la supermarkets Tanznaia ni geni sana kwa watu wengi labda wale wa zamani walioziona COASATA na STC (Saidia Tujenge Chetu) na ambao wametembea sana nje ya nchi. Baada ya COSATA kutaifishwa na kufanywa STC, STC ilikufa na badala yake yakatokea maduka ya kila nyumba. Ndiyo maana Tanzania kumejaa "mafremu" kila mahali, mpaka Osterbay na Masaki. Watanzania hata wale wenye kipato cha kati (Middle Income) hawana utamaduni wa kununua kwenye "supermarkets". Aliyeandika kuwa sababu ya watu kutonunua "supermarket" ni "low percentage" ya "middle income group" anaweza kuwa hajalifahamu tatizo vizuri. Botswana ina watu millioni mbili lakini karibu kila mtu anaishi kwa kwenda "supermarket" ambako unanunua hadi mchicha. Hata viduka vya mitaani vinapata bidhaa zao supermarket. Ndiyo maana ukiwa Botswana ni nafuu kununua "supermarket" kuliko mtaaani. Kwa Tanzania, kwa ujumla, ni kinyume.
Kama middle income ya Tanzania ni 12% hiyo ni sawa na kusema watu karibu millioni tano. Kama ni 5% ni sawa na watu millioni 2, yaani idadi ya watu wote wa Botswana. Kama watu wote wangenunua supermarket basi supermarket zingestawi kuliko Botswana ambako kumejaa "Shopping Malls, supermarkets and hypermarkets".
Kilichoua viwanda vyetu vya nguo ilikuwa ni siasa mbaya - Ujamaa, siyo liberalization. Kwa wenye kumbukumbu nadhani wanakumbuka kuwa alikuwa ni Salim Ahmed Salim wakati alipotembelea Mtwara aliruhusu mitumba iletwe Tanzania baada ya kuona watu wakitembea bila nguo. Tukumbuke tena kuwa kuna wakati watanzania walikuwa na shida sana ya nguo na wengine walitembea uchi! Sipendi kuzikumbuka siku zile kwani huko vijijini watu khanga na kitenge zilikuwa ni "tie-and-die" tu na sisi wa mjini tulikuwa tunavaa tacron za Msumbiji. Chupi zilipotea kabisa. Watu tayari walikuwa wameshaanza kuiba mitambo ya viwanda kama Kilimannjaro Textile na Sunguratex.
Serikali ya leo ina wajibu wa kutunza viwanda vyetu vya nguo, vya serikali na vya watu bianfsi. Kuna wengi wanataka Mwatex na Urafiki vifanye vizuri. Ukweli ni kuwa viwanda licha ya kutomudu ushindani wa bidhaa kutoka nje vinashindwa kupambana na viwanda vya binafsi vilivyopo Tanzania. Kiwanda cha Urafiki ikiwezekana kiuuzwe tu - lakini mafisadi watapeana wao kwa wao, bureeeeee!
Mpaka leo sielewi ni kwa nini watanzania wanashindwa kutumia cherehani kushona nguo na kuilazimu nchi kuagiza bidhaa hizo nje hata kama ni sare za shule.
Mkuu hata kiwanda cha urafiki kikiuzwa kwa haki je kitaweza ushindani? Viwanda vingi vya nguo baada ya kufufuliwa/kubansifishwa vilianza angalau kutengeneza mashuka na vitambaa mbalimbali, ila hata mashuka kwa sasa hawatengenezi tena kutokana na kuwepo mashuka mengi sana ya mitumba,
Kinacho takiwa hapa ni sera na ili kulinda viwanda vya nguo ni lazima serikali ije na mikakati ya uhakika kuhusu mitumba na ikibidi waweka hata import quota ya mitumba kutoka nje, kwa sasa hakuna mwekezaji atakaye kuja tanzania na kuwekeza kwenye viwanda vya nguo, wanafahamu fika kabisa hawataweza ushindani wa second hand kutoka Ulaya,
Hili swala la supermarket ni kweli kabisa ni vitu vigeni sana Tanzania na kuna factor nyingi sana kwa nini supermarket hazifanyi vizuri Tanzania kama Kenya na nchi zingine.
Na hata viwanda vya ndani vinavyo fanya vizuri kama A to Z Arusha ni kwa sababu ta tenda ya Net za bushi na ukiangalia mwenzake Sunflag amabae mwanzoni walikuwa sawa kwa sasa yuko huoi sana na amebakia kutengeneza shuka za kimasai tu, ingawa bado nako ni tatizo
Moja ya sababu ni kwamba,
1. Yale maduka watanzania wengi wanaya chukulia kama ni sehemu ya anasa
2. Haya maduka ni kwa ajili ya wazungu na watanzania wachache wenye pesa
3. Watanzania wengi vijijini na hata mijini wana mudu kulima na kuzazlisha mazao ya chakula kama mahindi, mchele. kufuga kuku wa kula, na kazalika na haya maduka mkubwa ununuzi mkubwa uko kwenye chakula na watanzani wengi wana magunia ya mahindi na mipunga ndani so hawaoni umuhimu wa kwenda kununua unga wa superparket wakati wana mahindi ndani.