''watanzania hivi ndivyo tunavyouwana'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

''watanzania hivi ndivyo tunavyouwana''

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ahmed samwel, Mar 18, 2012.

 1. A

  Ahmed samwel New Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asalaam alaykum ndugu wanaJ.F.
  Kuna hili shirika la kuthibitisha ubora na usalama wa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu,hapa nchini,kwa lugha ya kiingereza ''TANZANIA BUREAU STANDARDS''yaani (tbs)na watanzania tulio wengi tumekuwa na imani kuwa bidhaa yoyote tuinunuayo ikiwa na nembo ya shirika hili yaani(TBS)huwa ni bora na salama kwa matumizi ya binaadamu,hususani hizi bidhaa za vyakula na vinywaji.
  Lakini hebu tujaribu wenyewe kuchunguza kama kweli hili shirika linawajibika na kweli kama tunapaswa kuamini ubora wa viwango vilivyowekwa na (TBS)je ni salama kweli?au ndio sisi tutabaki kuwa vipofu wa fikra na macho?
  Ndugu zangu nyote mnajua na mnaamini kuwa uvutaji wa tumbaku yaani(sigara)ni hatari kwa matumizi ya afya ya mtumiaji,Na hata kwenye pakiti za bidhaa hiyo utaona wameweka onyo,kwa maandishi madogo kabisa pale chini ya pakit,
  lakini ndugu zangu utakapojaribu kuigeuzageuza pakit hiyohiyo utakuta imepigwa chapa ya nembo ya (TBS)ikimaanisha kuwa ni bora na salama kwa mtumiaji,sasa hivi ni vituko?au ndio tunaishi kwa nguvu za giza?
  Kwa hali hii tutakwisha,Na hebu tuangalie na hii mipira ya kiume yaani CONDOM ambayo kwa asilimia flani inaaminika kuzuia mimba zisizotarajiwa na pia kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya zinaa,ukiwemo ukimwi.Pia utakapojaribu kufanya uchunguzi katika pakt ya ''salama''utaona nembo ya(tbs)pale sasa jamani je?ni kweli mipira hii ni salama na haina madhara yoyote kwa mtumiaji?ikiwa sigara tu ina madhara na tbs wameidhinisha je sisi tunaoamini hii mipira tupo salama?
  ''WATANZANIA TUAMKE HUU WAKATI SIO JAMANI TUTAKWISHA''
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Aisee kuna kitu nimenunua cha kutumia yani ni fake kabisa nimekitupa baada ya kuona kina test tofauti na niliyoizoea,wafanyabiashara na watu wa tbs wanatuua!
   
 3. michosho

  michosho JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 454
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  mawazo yako ni kweli,na tunahitaji kufkiri sana hasa kwa bidhaa nyingi tuzitumiazo,kwani TBS hawafanyi kazi yao ipasavyo,ni jina tu lakia kiuhalisia hawafanyi kazi zao km objectives zao zilivyo kote duniani.
   
Loading...