Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Napenda kusema Watanzania sisi tunapenda Cheap popularity and kweli, sisi ni cheap commodities. Na watawala wanatujua vema, ndiyo maana wanafanya wapendavyo
Fundi Mkuu
Siyo rahisi kuwa makini kama kila kitu kinachopita mbele yako unataka ukijadili. Hii inapelekea Watanzania wengi kuwa ni rahisi kuwahamisha kutoka mjadala mkuu na kuwapeleka chaka kifikra kwa sababu umeibua kitu fulani kitakachowakosesha muda wa kufikiria suala lililokuwa mbele yao.
Mfano mzuri ni Tanzania yetu jinsi ilivyo na rasilimali nyingi tulizojaaliwa na mwenyezi Mungu, na zingine zinazidi kuibuka kila kukicha kama gesi. mafuta na makaa ya mawe. Kwa bahati mbaya sana tunasahau kama zilizopo tayari ni rasilimali za kutosha kuboresha uchumi wa nchi. Tunahamishia mawazo kwenye gesi na mafuta.
Hivi kama rasilimali zilizopo Tanzania toka miaka mingi iliyopita zimeshindwa kutumika kujenga uchumi wa nchi, leo hizi mpya zitakuja na maajabu gani?
Wananchi nao mambo ni yale yale. Iliwahi kutokea Misiba Tanzania kwa wakati mmoja, iliyowagusa wanasiasa maarufu kama Zitto Kabwe (Mamake) na Martha Mlata (Babake) ilituhamisha kwenye mjadala wa namna mapesa ya nchi yetu ya ESCROW yalivyotafunwa kule Nishati na Madini na kwingineko.
Iliwahi kutokea tena kitu kinaitwa Babu wa Loloiondo, (Kikombe cha babu) ni kipindi cha Vugu vugu la Katiba mpya, watu walihamishwa, zikatumika gharama kubwa kusomba watu nchi nzima, wakaelea huko, wakafanya wanayoyajua, na UKIMWI ukaendelea kuwamaliza.
Juzi hapa tulikuwa na shida ya Demokrasia bungeni, na Sukari kwa wakati mmoja, lakini "Wataalamu"wakatuletea kWizi wa kiafaru, Bunge likaendelea kuzimwa, Sukari imeendelea kupanda, Ujinga unaendelea kututawala, In fact, we are Most of Tanzania are Cheap Commodities.
Kwa mtindo huu sio rahisi kujenga nchi. Maana kujenga nchi kunahitaji kushikiria hoja kuu (Concentraion) na kuhakikisha kuwa inakupa matokeo yale uliyohitaji toka awali. Najiuliza hoja yetu ni ipi sisi, mbona hatuna hoja za kudumu..! Ndiyo maana nasema Watanzania sisi tunapenda Cheap popularity and in fact, we are cheap commodities