Watanzania, hatumjui Paul Makonda?!

Watanzania, hatumjui Paul Makonda?!

Niko tayari kuitwa mnyama Mwenye jimwili kubwaaa bichwa Dogo ila kamwe siwezi kuwa upande wa huyo mtu wako anayejiita Sehemu ya Mungu huku anadhalilisha watu hadharani kwa Focus ya Kujijenga yeye zaid
Hii ni post ya Bashite mwenyewe.
 
Nchi zilizo endelea kiongozi ukiwa na kashifa hata ya kuwa na nyumba ndogo huna budi kujiuzuru,isu ya kutumia cheti cha mtu mbona ni isu ndogo sana ya kutoa ushahidi kwa dakika TANO tu kila kila kitu kina kuwa wazi
Achana na hypothesis za kusadikika acha maneno weka ushaidi isu kwisha ,unataka kukimbia wakati hauna b what do you expect ,hakuna isu lahis kama hiyo weka ushaidi itakuwa kimyaaaa yaan kimyaaaaa achana na hypothesis za kijinga weka ushaidi Wa ukweli the game will be over and over and over
 
Maneno kibao lakini yote sifuri.. Hakuna TISS ambaye alipata sifuri form four.. Naomba uheshimu kazi za watu.. Hakuna kilaza TISS. Ile imejaa intelligent guys who does intelligence work for the government.
Naona waTZ mmefikia kubaya hadi kuhusisha watu waliopata sifuri na Taasisi imara kama TISS.. Utatueleza kwanini umehusisha TISS na sifuri.
TISS Le Mutuz
 
Naona umeamua kuchagua upande wa kutetea, mbaya zaidi kila lililofanywa na upande ulioamua kuushabikia according 2ur hypothesis ni sahivi, ila kila aliyejaribu kukosoa usanii uliokuwa ukiendelea according 2u hayuko sahihi. Ila kumbuka hii nchi ni yetu sote ukweli utaendelea kuwa ukweli2...
Mazumbukuku wana quote liuzi lirefuuu
 
well said Sir/Madam, let's discuss issues, not personalities.
 
Kuanzia Sakata la kutaja Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya mpaka kinachodaiwa "Uvamizi wa kituo cha Clouds Media Gruoup"! RC Paul Makonda amekuwa gumzo kuu hapa Nchini kwa sasa ,kuanzia kwenye vyombo vya habari,mitaani na kwingineko!

Nikiwa hapa Kijijini kwangu Mwanduhitinje nimekuwa nikilifuatilia suala hili kwa taratibu sana bila mihemuko ili nijifunze kitu kipya na kwa kweli nimejifunza sana!

Kabla sijasema mafunzo niliyopata kutokana na "Sakata" hili niwaeleze kuwa nimesikiliza Clips zote za "Askofu" Gwajima kuhusu RC Paul Makonda,Nimesoma magezeti yote yaliyo na yanayoandika habari kuhusu RC Paul Makonda,Nimefuatilia post zote za Mange Kimambi kuhusu RC Paul Makonda,nimefuatilia comments za Watu mbalimbali kuanzia RC Paul Makonda akichipukia UVCCM akitokea TAHLISO kama Rais wake na hata alipom-blast Lowassa kuwa hana sifa za kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, na sasa naeleza mafunzo niliyopata na hasa baada ya kusoma Gazeti la JAMUHURI kwa kile walichokiita Uchunguzi uliofanywa na WAANDISHI WETU!

FUNZO LA KWANZA: Tanzania ni miongoni mwa Nchi Duniani zenye uhaba wa Waandishi wa habari na Wasomi (Ninaposema wasomi simaanishi wale wenye "A" zote na Makofia mengi lakini wameishia kufuga kuku na Nguruwe kule CHANGANYIKENI).

FUNZO LA PILI: Watanzania wengi ni watu wasio na agenda yoyote ya maana ya ku-accomplish katika maisha yao bali ni watu waliokata tamaa na wanaotumia MATUKIO kama "pain killers" ya kuwapunguzia maumivu kutokana na KUSHINDWA kwao.Ndio maana Watanzania wengi hushabikia sana habari zinazomdhalilisha mtu au kumshusha chini mtu aliyeko juu kama RC Paul Makonda.

FUNZO LA TATU: Watanzania hatuna wanasiasa wenye maono,wanasiasa wetu wengi ni waganga njaa tu ambao wamefanya siasa kama kichaka tu kujifichia na kutafuta riziki kwa ajili ya maisha yao na siyo maendeleo ya wapiga kura na Taifa kwa ujumla!

FUNZO LA NNE: Tanzania hakuna UPINZANI,na itachukua miongo mingi sana Nchi hii kuweza kuongozwa na Chama cha Upinzani.Hawana Ajenda na ni watu wa MIHEMUKO! Ajenda zao ni kama hizi WEMA SEPETU KUPOKELEWA CHADEMA,TUNDU LISSU KUWA RAIS WA TLS, RC PAUL MAKONDA KAVAMIA KITUO CHA CLOUDS MEDIA GROUP.

FUNZO LA TANO: Wapinzani wa Tanzania HAWAJITAMBUI na WALA HAWAJUI WANAMTUMIKIA NANI! Hawana Rafiki wa kudumu wala Adui wa Kudumu! LOWASSA FISADI,LEO LOWASSA JEMBE! NAPE VUVUZELA leo NAPE JEMBE kwa kuwa "amekurupuka" kutoa tamko la kulaani Kabla ya Taarifa ya uchunguzi wa kamati yake aliyounda kumfikia mezani!

Baada ya kusoma hayo MAFUNZO niliyopata kuhusu "SAKATA" la RC PAUL MAKONDA embu njoo sasa nikupitishe kwenye hizi "hypothesis" zangu kabla hamja-conclude jambo lolote.

Observation moja muhimu kwanza ni hii hapa: Watanzania wengi, Wanasiasa,Wasomi na Wananchi wa kawaida wanafananishwa na mnyama mmoja mwenye umbo kubwa sana sawa na Uwanja wa mpira wa miguu lakini ni mnyama mwenye kichwa kidogo mithili ya bakuli ndogo ya kulia supu! Uwezo wa mnyama huyu kufikiri ni mdogo sana na kuhisi chochote ni mpaka umguse kichwani.( Their brains are very small to entertain two big events at once ! they must drop one event to entertain the other !) ! Ndio maana Nchi hii ni ya MATUKIO hili likija litafunika hili na hakuna impact yoyote na hata hili la RC Paul Makonda litapita muda si mrefu kama unabisha subiri Bunge lianze April! RC Paul Makonda wewe vumilia tu bado KITAMBO KIDOGO WATASAHAU TU!

HYPOTHESIS YA KWANZA:
Nimesoma kwa utulivu sana Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI kuhusu Paul Makonda,Mtu aliyesemwa na akina "Askofu" Gwajima kuwa Paul Christian Makonda anatumia vyeti vyake Ndugu Paul Pierre Christian amekanusha vizuri sana na pia hana dada aitwaye Christina aliyetajwa na akina "Askofu" Gwajima. Hakuna dhambi yoyote jina lako kufanana na la mwingine, Juma Ali wako wangapi Zanzibar? Mohamedi Ali wako wangapi Duniani?!
Sheria inaruhusu kubadili jina na RC Paul Christian Makonda na kama ni kweli alikula kiapo mahakamani kubadili jina basi alijua jina alilokuwa akitaka kutumia la PAUL CHRISTIAN MAKONDA si lake la awali! Kwa nini basi aliende mahakamani?

HYPOTHESIS YA PILI;
Je PAUL CHRISTIAN MAKONDA hawezi kuwa ni mtu makini mwenye "SPECIAL MISSION" kutoka "KITENGO" fulani anayo-accomplish ?!
"Qualities "anazoonyesha RC PAUL MAKONDA zinazoweza ku-support hii hypothesis ni hii ya kupoteza "initial identity yake",pili angalia comments za Mzee Khamesse na familia yake ni watu ambao wamekuwa "disappointed" na tabia za RC PAUL MAKONDA, Nawanukuu kwa mujibu wa JAMHURI, " alikuja hapa kama mara mbili saa saba usiku na saa tano usiku,hakuingia ndani! Hapokei simu na namba anazowapa ni feki muda wote hazipatikani!
Kwa utamuduni wa kiafrika kwa watu waliokulea na tena kwa MUSUKUMA kama PAUL MAKONDA na pia kwa umaarufu na hesima aliyonayo Mzee Suleiman Khamesse lazima kuna KITU HAPA si Bure!!!!!

HYPOTHESIS YA TATU;
Katika vita hii ya Madawa ya kulevya tunajua RC PAUL MAKONDA amefanya jambo ambalo hata Marehemu Amina Chifupa alitaka kujaribu lakini hakulifikia.Kilichompata Amina Chifupa sote tunajua.Hivyo hawa WAUZA UNGA NA WATEGEMEZI WAO HAWAWEZI KUMFURAHIA RC PAUL MAKONDA LAZIMA WAJARIBU KUMWANGAMIZA TU! Na hapa Mheshimiwa Rais DR. JMP kama unaujua ukweli kuhusu kijana huyu basi please MLINDE KWA GHARAMA YOYOTE!
Ndio maana unapoona NAPE NNAUYE anatukuzwa kuwa ni jembe japo ukweli ni kuwa "AMEKURUPUKA" sana na kutozingatia ile dhana ya "collective responsibilty". WENGI WANAPIGANA VITA YA WAUZA UNGA DHIDI YA RC PAUL MAKONDA BILA WAO KUJUA au KWA KUJUA na Nape Nnauye AKIWEMO!

HYPOTHESIS YA NNE;
Kuhusu RC PAUL MAKONDA kuvamia kituo cha CLOUDS pamoja na kupewa Magari na Watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya kulevya yaani kampuni za TANGA PETROLEUM LIMITED NA NAS HAULAGE LIMITED. Hapa nikiri wazi kuwa najenga hoja yangu kufuatia maarifa niyopata kutokana na kusoma vitabu vifuatavyo: Kitabu cha The Book of Five Rings cha Mjapani Miyamoto Musashi, Kitabu cha 48 Rules of Power na Kitabu cha Lucifer Principles cha Howard Bloom.

Ukiangalia kwa hao marafiki zake kwa pamoja RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA amejaribu sana kujenga nao urafiki wa karibu mno! Je hii HAIWEZI kuwa ni strategy ya "kum-nail" adui ?! Je CLOUDS media Group hawatajwitajwi katika hii biashara HARAMU ya Madawa ya Kulevya?! Chunguza na fuatilia kifo cha Msanii Albert Mangwea kama MKONO wa CLOUDS MEDIA GROUP hautajwitajwi.

RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA anaweza kuwa ni mtu "HATARI" kuliko anavyochukuliwa ,kubezwa na kudhalilishwa na WATU WENYE UPEO MDOGO kama yule Mnyama niliyemwelezea hapo juu!

Yawezekana RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA akawa sawa na mtu anayetupia kuku wake mahindi pale tu anapotaka kumkamata ili amchinje! ZITTO KABWE anasema ameambiwa kuwa kile kikosi alichotumia RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA "kuvamia" CLOUDS kilikuwa maalum ambacho idhini yake hutolewa na Rais au Boss TISS. Je,tunajuaje kama RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA alitumia style ile ya YUDA ISKARIOTE aliyotumia kumtambulisha YESU Christo kwa wale maadui waliofika bustanini kumkamata? Labda RC PAUL MAKONDA "alinusa" kuwa CLOUDS MEDIA GROUP depot yao ya "UNGA" wameihamishia Studio na hivyo akaona aende na kikosi maalum incase ameukuta huo "UNGA" upo awakombe na incase ameukosa awapotezee tu kuwa yeye ni mtu wao na anafuatilia "Kipindi chake".

Kwanini isiwezekane hivyo kama ni huyu PAUL CHRISTIAN MAKONDA ambaye alituhumiwa kumfunga Ridhiwani Kikwete kamba za viatu na bado akaja kumuorodhesha katika orodha ya watu 97 anaowatuhumu kufanya Biashara ya dawa za kulevya!

Amemtaja Ridhiwani Kikwete na Yusufu Manji kuhusika na biashara ya Madawa ya kulevya kitu ambacho MWIGULNCHEMBA hawezi kufanya hata kama angekuwa na ushahidi mkononi!
Tungekuwa na Waandishi makini wangechunguza RC Paul Makonda anapokuwa nje ya Nchi anaongea na akina nani MISSIONS zake ni zipi lakini kwa hawa wetu ambao wakiamka wanakimbia kuangalia leo Mange Kimambi ame -post nini au Jumapili hii "Askofu" Gwajima atamchanaje Paul Makonda!

Hivi ukiwa hujapewa Vyeti uangalie na ukaambiwa uwasikilize wakijenga hoja SAED KUBENEA, BONIPHACE JACOB (MAYOR WA UBUNGO) na RC PAUL MAKONDA nani utasema ana ZIRO! obviousily ni KUBENEA na BONIPHACE JACOB! Je,ZIRO ya Paul Makonda haiwezi kuwa ni ya kutengeneza kwa "SPECIAL MISSION".?!

Albert Einstein alipata kusema kuwa akili iliyotumika kutengeneza tatizo haiwezi kutumika kutatua tatizo hilo.NDUGU WATANZANIA TUTAMBUE KUWA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA NI NGUMU KULIKO TUNAVYOFIKIRIA na kama unabisha kamuulize JAKAYA MRISHO KIKWETE au WILLIAM LUKUVI.
Unayepiga kelele bila kuruhusu kichwa chako kufanya kazi piga tu kelele LAKINI TAMBUA KUWA yawezekana unapiga kelele bila kujua kuwa wewe ni sawa tu na MBUZIaliyeko kwenye banda la mpika supu!
Kuwa rafiki wa wauza unga na kutumia Mali zao haina tofauti na wewe kua mmoja wao
Kumbuka Kajala masanja aliwekwa ndani na kutupwa gerezani na baade kuokolewa na Wema Sepetu kwa fine ya sh. Mil 13 kwa wingi wa makosa ambayo yeye Kajala hakuyafanya Direct
Ambapo ilidaiwa kwamba mume wa kajala Faraji Agustino alitakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC na kisha Ku oda mkewe kajala auze nyumba yao ambayo ilikua ikichunguzwa na Takukuru
Kwa makosa hayo hayo yaliyotaka kumtupa kajala Gerezani ndio makosa aliyonayo Daudi ya "kutakatisha Mali (magari) ya wauza unga",sasa kama sheria ilimuhukumu kajala na Faraji kwanini pia isitumike kumuhukumu RC? Hebu watanzani tujitahidi kuwa wakweli, tuache unafiki Leo unakaa hapa unashupaa kumtetea makonda kesho na kesho kutwa Dada au kaka yako ataja tupwa gerezani kwa kosa la kutumia Mali haramu au ya wizi ambao yeye pengine hakushiriki kuiba! Makonda alichotakiwa sio kuzitumia Mali za wa wauza unga Bali alitakiwa kuzishitaki kwenye mamlaka ili washughulikiwe, tutaachaje kusema kua makonda hizo Mali amehongwa ili awatoe hao washukiwa kwenye hicho kimbunga!!
SIKU ZOTE UKIWA MNAFIKI MCHANA JUA JIONI ITAKUHUKUMU
"Asalaam Aleykum"
 
[USER=403090]Fumadilu Kalimanzila[/USER] umeongea vyema nawe kwa uelewa wako na mawazo yako.. Ila sijui kama unaelewa maana ya special mission na sheria zake na how it comes to be special mission.. Sizani kama la kama ili la Paul Makonda ni special mission.

Nimesoma funzo zako naomba nikubaliane nawe..

Ila udhaifu wako nawe umelichukulia jambo juu juu bila kuangali pande zote kuhusu ili jambo.

Kuhusiana na nape sizani kama kakurupuka labda uniambie aje kutoa maamuzi yaliyo upande Mmoja kwa shinikizo flani... Ila kama kiongozi AME act kama kiongozi anaye respond jambo la dharura linapotokea..kama Paul Makonda mwenyewe alivyokuwa akifanya katika kazi sake.
 
Weraaaaaaaaaaa! waliotumwa wameanza kuja 'kusafisha' jitahidi baba ila waambie malipo uliyolipwa ni kdg sana waongeze! bora hao wafuga kuku na nguruwe kuliko wewe wa ukuwadi mkuu.
 
Nimeisoma mwanzo mwisho, laikini kama ulivyosema na wewe kwamba umewasoma na wenzio plus kumsikiliza Gwajima na mimi pia na conclude kua hata wewe umetengeneza conclusion yako wakati tayari unao upande. Tukio la mtu kuvamia studio ya watu kwa kutumia police halihitaji kua na kichwa kikubwa kujua kwamba kilicho fanyika sio sawa na pia lazima kukifanye ujue kwamba kuna kitu kinafichwa na mtekaji. Again, issue ya kuapa mahakamani kwa maana ya kubadiri jina that much can't be an issue kama kweli ulisomea jina la mtu, wengi wanafanya hivyo na hata wapo wengine wana vyeo vikubwa kuliko hata RC wanazo tuhuma hizo, but walikua wanafauru shuleni. Suala la kwenda shule kwa ktumia cheti cha mtu mwingine hasa baada ya secondary huo ni wizi cause baada ya secondary ili kwenda kwenye level nyingine, either iwe certificate au cheti chochote kunakuaga na SIFA za kuingilia huko, sasa hukua nazo cause ulitumia cheti cha mtu mwingine. Utetezi mwingine eti alitafutwa huyo anae itwa sijui Paul Christian???? Hivi ulitegemea mimi nimuuzie cheti change mtu Fulani na mtu huyo ana cheo kikubwa serikalini na raisi wa nchi anauunga mkono utegemee niwe pamoja na Gwajima??? Mkuu, hapo hata wewe hukutumia akili kama ulivyosema! Nimeuza cheti, niliyemuuzia anayo nafasi, who knows kama hua ananitoa kiana? But again hata kama hanitoi, mtu huyo anaweza kuvamia studio ya mabilionea na asifanywe chochote, mimi kapuku tu niliye kijijini naweza kua against him? Hapo hukufikiria and this is why nimesema, hata wewe ulikua na conclusion kabla hujasoma hayo ulioyasoma.
 
Kama aliapa mahakamani basi aje atuambie ili hili lipite kuliko kukaa kimya sababu watu hawachoki mpaka kieleweke
 
Nimesoma kufika sehemu ulipoanza kuuponda upinzani nakusifia CCM nikaacha.
Umeandika upuuzi mtupu
 
Hio ya kuongea na Sallah na GSM Sasa ndio mission yenyewe. Nadhani unatumia nguvu kubisha ila huna hoja, hivi iwapo USA walimpanda/ plant Gorbachev ili aiue USSR na ikawezekana, why hii hoja kwenye hii thread isiwe valid?

Inawezekana umezoea kuona uji wa ulezi na mahidi lakini ukasahau pia kuna uji wa viazi au ndizi.

Bakia na hasira zako
Mkuu hata mimi nimemcheki tu na povu lake mwenyewe anaona anapinga kipoint balaaa.
 
You killed it Kalimanzila

Nanukuu......."Watanzania wengi, Wanasiasa,Wasomi na Wananchi wa kawaida wanafananishwa na mnyama mmoja mwenye umbo kubwa sana sawa na Uwanja wa mpira wa miguu lakini ni mnyama mwenye kichwa kidogo mithili ya bakuli ndogo ya kulia supu! Uwezo wa mnyama huyu kufikiri ni mdogo sana na kuhisi chochote ni mpaka umguse kichwani.( Their brains are very small to entertain two big events at once ! they must drop one event to entertain the other !) ! Ndio maana Nchi hii ni ya MATUKIO hili likija litafunika hili na hakuna impact yoyote na hata hili la RC Paul Makonda litapita muda si mrefu kama unabisha subiri Bunge lianze April! RC Paul Makonda wewe vumilia tu bado KITAMBO KIDOGO WATASAHAU TU!

Hiki ndicho kinachotuponza Watanzania tuombe sana Mungu atuhurumie.

Tupunguze kusikia tu tuwe tunafanya na utafiti kidogo kuprove kama habari ina ukweli au la kwa kutumia common sense tu.

Tuache ushabiki wa vitu tusivyojua undani wake hii itasaidia watu kuwa na furaha......hahhahhahhah HATUTOKUWA WA MWISHO TENA.

Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki Africa.
 
Naunga mkono hoja ipeleke kwenye gazeti ili watu wasome na kuelewa,SUMU zote walizokunywa ziwatoke.
 
Back
Top Bottom