Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,259
Nimekuwa napata shida sana kuzielewa taarifa au michango toka katika magazeti mbalimbali hapa Tanzania na hata pia humu ndani ya JF. Baadhi ya makala ili uzielewe inatakiwa ujitahidi mwenyewe kuumba maneno na sentensi kama wafumbua fumbo. Mara nyingi lugha ya kiswahili huwa haitumiki kwa usanifu na usadifu. Na hata wanaochagua kutumia kiingereza huwa hawajali kama wametumia maneno sahihi ukiachia mbali mambo ya 'structure'.
Utashangaa mtu anaandika 'ajui' akiwa na maana 'hajui', 'akuwepo' akiwa na maana hakuwepo n.k. Pia sheria ya kuanzia herufi kubwa baada ya nukta haitumiki hasahasa watu wanapochangia hoja fulani. Hii ni mifano midogo katika matumizi mabaya ya lugha. Nashangaa inakuwaje twashindwa kutumia lugha vizuri, japo wengi wa wanaotumia lugha vibaya wanaonekana ni wasomi wazuri maana hoja zao huwa zimeshiba.
Binafsi si mtaalamu wa lugha, ila ninajitahidi kujifunza. Naamini hata makosa yakiwa ni madogodogo, hakika yataondoa imani ya hoja au ujumbe unaotolewa kwa kuwa yatakuwa yametoka kwa mtu asiye makini.