Watanzania: Bado mnawaza kuwa viongozi wanamuenzi Mwalimu Nyerere

FrediusSnowden

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
269
250
Habari za asubuhi wakuu. Natumaini kwamba mko salama kabisa. Ni jambo la heri sana kwake Mungu kwetu sisi wanawe. Basi kwa kuanza niwapongeze wote kwa kuadhimisha kumbukizi ya Mwl J.K. Nyerere alifariki mnamo mwaka 1999, mwezi wa kumi tarehe 14. Ni wazi kwamba Mwl J.K. Nyerere ni ICON kwa viongozi wengi na pia ameleta heshima ya kipekee kwa taifa letu hili kongwe kiumri changa kimaendeleo.

Katika pitia zangu katika mitandao ya kijamii kuona ni namna gani viongozi kiserikali wanamuenzi Mwl J.K. Nyerere, ndipo nilipo pata mshangao wangu na kufanya kichwa kufikiri kisha kuandika uzi huu.(kama wewe ni kiongozi naomba tulia, na kisha yaa he hapa).

Maswali ni kama yafuatayo..
1. Kwanini siku ya kumuenzi Mwalimu Nyerere iingiliane na shughuli za mwenge?
2. Mwalimu alikuwa ni kiongozi wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, kwanini maadhimisho haya hayajafanyika Tanganyika (Tanzania Bara)?
3. Kwanini shughuli hii haikunakishiwa na mabango jumbe na picha za Mwalimu Nyerere?
4. Kwanini hapakuwa na mijadala mikubwa juu ya kumbukizi hili?
5. Kwanini mashati ya vitenge ya mwenge zaidi kuliko mashati ya vitenge ya mwalimu?
6. Kwanini kuingiza siasa na shughuli za chama katika shughuli za kitaifa kubwa kama hizi?
7. Kwanini kupanga makusudi mwingiano mkali kama huu wa tarehe za hii shughuli na masuala ya mbio za mwenge?
8. Kwanini kutokutaka mualiko wowote katika shughuli za maadhimisho hayo?
9. Kwanini sisi kama watanzania tuko kimya katika hili;au ni bumbuwazi la sintofahamu fahamu?
10. Kwanini kwanini ziko nyingi?

Basi niishie hapo. Taarifa ni kwamba shemeji yenu kajiunga baada ya pilikapilika nyingi za hapa na pale. Tulipima mkojo na nk mambo sasa mswano. Nawafikishia salamu zake kwenu. Ni mapacha? Tutajuzana.
 

dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,389
2,000
Mwenge kuutenganisha na Hayati baba wa taifa ni vigumu.
Sijaelimishwa vya kuyosha kuuona umuhimu wa mwenge siku nikielimishwa huenda nikajua ni kwanini tunamwenge unaokimbizwa nchi nzima.
Mungu atujaalie kuyajua tusiyoyajua.
"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 

FrediusSnowden

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
269
250
Mwenge kuutenganisha na Hayati baba wa taifa ni vigumu.
Sijaelimishwa vya kuyosha kuuona umuhimu wa mwenge siku nikielimishwa huenda nikajua ni kwanini tunamwenge unaokimbizwa nchi nzima.
Mungu atujaalie kuyajua tusiyoyajua.
"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
Mkuu hoja ni kwanini iwe siku ya kumbukizi la Mwalimu Nyerere, jambo linalofunika siku husika? Sijawai shuhudia hali hii kama iko mtu itujuze..
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,360
2,000
Taarifa ni kwamba shemeji yenu kajiunga baada ya pilikapilika nyingi za hapa na pale. Tulipima mkojo na nk mambo sasa mswano.
Usiwe unataka kuleta visingizio kwa shemeji Baada Ya poor perfomance maana hakuna sababu Ya malalamiko yote haya, ikishindwa kata kiu kwa bombadia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom