Watano kizimbani kesi ya mauaji ya mwanaharakati

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Watu watano akiwamo ofisa wa Benki ya NBC na raia wa Burundi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama ya kufanya mauaji na mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la Palms Foundation, Wayne Lotter (52).

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Yamiko Mlekano leo Februari 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amewataja washtakiwa hao kuwa ni raia wa Burundi, Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi na mfanyabiashara Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A.

Wengine ni mfanyabiashara Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, mfanyabiashara Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo katika shtaka la kwanza wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16, 2017 walikula njama ya kufanya mauaji ya Lotter.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la mauaji ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni Dar es Salaam kwa kumuua Lotter.

Chanzo: Mwananchi
 
Kama Kweli walihusika wanastahili adhabu Kali kabisa
 
Kama kweli wao ndiyo walifanya hicho kitendo basi sheria kali ichukue mkondo wake. Inauma sana kumuua mtu asiye na hatia.
 
uchunguzi ufanyike kwa umakini mkubwa sana, nna wasiwasi na hao wanaoshikiliwa huenda ikawa si wahusika kabisa wa hilo tukio
 
Back
Top Bottom