Watangazaji wetu: Juu tai, shati, koti ila chini jinsi /kaptula na raba

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
Wakuu utafiti unathibitisha kuwa watangazaji wengi wa television hapa bongo wanavaa ndivyo sivyo kisa tu katika TV huonekana kuanzia kichwani mpaka kiunoni.

Wanachofanya sasa wanahakikisha wanaulambia sehemu ya juu inayoonekana luningani yaani anapiga tai kali, shati kali na bonge la koti, ila sasa kwa chini anavaa anavyojua yeye yaani wanapiga jeans au kaptula na raba si hawaonekani kwa chini mazee.

Ushauri wa bure jamani watangazaji wetu achezi hizo bana
 
Hii kali saaana ila mkuu ni vema ungetuweka wazi ni kituo gani cha TV gani ambacho watangazaji wake wanavaa kiajabuajabu kama hivyo
 
kwani shida ni nii hapo anaonekana nadhifu ...
tena hata huko akivaa taulo na ndala hakuna taabu
 
Mtu dhaifu siku zote hufikiri kuwa nguo inaweza kumuongezea hadhi. Kwani wewe uliambiwa na nani kuna sharti la kuvaa suti studioni?

Inaonesha ndio ukoo ule ule wa kuhitimu chuo na joho kichwani hamna kitu
 
wakuu utafiti unathibitisha kuwa watangazaji wengi wa television hapa bongo wanavaa ndivyo sivyo kisa tu katika tv uonekana kuanzia kichwani mpaka kiunoni, wanachofanya sasa wanahakikisha wanaulambia sehemu ya juu inayoonekana luningani yaani anapiga tai kali,shati kali na bonge la koti, ila sasa kwa chini anavaa anavyojua yeye yaani wanapiga jeans au kaptula na raba si hawaonekani kwa chini mazee. ushauri wa bure jamani watangazaji wetu achezi hizo bana
Hapo kwenye red, unajua maana ya utafiti? Weka hiyo report ya utafiti hapa kabla sijachangia.
 
Si kweli, code za mavazi kwenye TV zipo wazi, inategemea mtangazaji ana kipindi gani siku husika. Mara nyingi wanaosoma taarifa ya habari na mahojiano siriaz, suti zao huwa ziko pale studio na kuna chumba maalumu cha kubadilishia nguo na kujiweka vizuri. Naongelea experience.
 
K 4 LIFE HAWA WACHANGIAJI HAWAKUFAHAMU VIZURI, VIPI MIKUMI HUJAPITA TENA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom