Yaani hata mimi ingawa ni CCM wameni bore sana. Anayesema wamechoka basi wangetoka tu na waingie wengine waendeleze. Sikiliza kuna sababu kubwa sana za kuendelea.
1.Ukiahidi kitu lazima utimize. Hakuna aliye walazimisha Asubuhi kabisa wao walisema wakati wote watakuwa live mpaka watoe matokeo.
2.Watanzania wana haki ya kupata habari tena ya muhimu kama hii. Uchaguzi huu si mdogo (ingawa ni mdogo kieneo) Ndio maana hata Rais mstaafu, Waziri mkuu Mstaafu, Mawaziri n.k walifika na kupiga kampeni. Je ITV hamjawahi kushuhuduia vyombo vya wenzetu wanavyo pokezana na kuchambua kwa takwimu ukutani jinsi matokeo yanavyoingia mpaka asubuhi? Je hamjaona watu wako Studio saa zote wanaendelea kuripoti zoezi la uokoaji watu waliokuwa machimboni?
3. Kila Mtumishi hata Wachezaji, wana ndoto na dhamira za kufanya vyema kazini au katika chochote wakifanyacho kwenye Public ili ikiwezekana wazidi kuaminiwa kwa performance zao. Hivi ninyi hamna ndoto za hivyo? Hamkumbuki Meya wa NY alipanda chati ghafla kwa kuoneka kuwa anajishughulisha bila kuchoka (24/7) baada ya tukio baya la tisa kumi na moja. Hivi mnafikiri kwa nini,vipindi kama 360 au Situation Room n.k vinaheshimika na pia Watangazaji wake wanaheshimika? Hakika kweli nadhani angekuwepo ndg. Gondwe asingetoka na angetumia hata kaprojector (non touch screen) kutujuza kinachoendelea na kuonyesha umahiri wake kama mhitimu wa MA Mass Com!
4. Mbona Msimamizi wa Uchaguzi mliongea naye wala yeye hakusema kuwa wanasitisha shughuli pamoja na kukiri kuwa kuna fujo za hapa na pale.
Agrhhh! Ni Watu kama ninyi na yule Mh. wetu aliyeporomosha matusi kweupe (na watu wote sasa wana kile kipande toka You Tube kama ushahidi) mnaofanya tutukanwe kuwa TUNACHAKACHUA KURA HATA KAMA WATU WAMENYUKWA KI-UKWELI.
Hivi kwa nini tunakosa Mastrategist wanaofikiri nje ya viota vya zamani? Ukweli ni kwamba mazungumzo ya Mzee wetu Masako na mwenzake yalikuwa yachekesha sana hasa wakianza kusema 'Oh! hivi kweli shughuli itaendelea kwa hali hiyo?' LOL, yaani vibomu vitatu tu vya machozi kutawanyisha kundi linaloziuia watu kuleta kura panapojulmlishiwa ninyi mnaanza kulalama. Na kile kichekesho cha eti mmoja wenu gari lake limeanguka sijui mtoni / mtaroni sasa ajali za binafsi nazo ziwe sababu ya kuacha kutoa taarifa. Hivi ninyi mliwahi kucover news kwenye battle ground hata siku moja?
Mweshimiwa Mengi naona kuna umuhimu wa hawa Wanahabari (na zaidi pia wale wa TBC wakati fulani wapelekwe kwenye mazoezini rasmi ya mazingira ya danger zones yaliyotengenezwa kama huko kwenye makambi ya JKT ili wajifunze maana bila stadi za maisha ya kivita / ktk fujo basi watakuwa wanakimbia ovyo na pia kuumia kizembe sana!