Watangazaji Ebony FM waponzwa na rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watangazaji Ebony FM waponzwa na rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 24, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATANGAZAJI watatu wa kituo cha redio cha Ebony FM mkoani Iringa, wamehukumiwa
  kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa muuguzi.

  Washitakiwa katika kesi hiyo, walikuwa ni Mcdonald Masse, Maregesi Eraga na Allen Emily.

  Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mfawidhi Marry Moyo wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi iliyopo katika Mji Mdogo wa Mafinga baada ya kuridhika na maelezo ya upande wa mashtaka juu ya kesi hiyo namba 162 ya mwaka 2010.

  Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Iringa, Nitume Mizizi kuwa watangazaji hao kwa pamoja, Oktoba 15, mwaka huu waliomba na hatimaye kupokea rushwa kutoka kwa muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Miraja Ngole ili wasitangaze habari zilizokuwa zinamhusu.

  Mizizi alifafanua kuwa watangazaji hao walifikia hatua hiyo baada ya kupata taarifa za muuguzi huyo kutuhumiwa kukataa kumuuguza mtoto Neema Malea aliyefikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu siku hiyo na kisha mjomba wa mtoto huyo kuwapa taarifa.

  Alidai baada ya watangazaji hao kupokea habari hiyo waliwasiliana na muuguzi huyo na kisha kumwomba rushwa hiyo, ambayo alikubali kuwapatia fedha hizo na kuwataka waende Mafinga kuzichukua.

  Alidai kuwa muuguzi huyo aliamua kutoa taarifa Takukuru Wilaya ya Mufindi, walioandaa mtego na kisha kuwakamata watuhumiwa eneo la Kinyanamba A wakiwa njiani kwenye gari lenye namba za usajili T629 AUD aina ya Honda CRV wakirejea mjini Iringa baada ya kupokea fedha hizo.

  Alidai baada ya kukamatwa na Takukuru, watuhumiwa walifikishwa mahakamani Oktoba 26, mwaka huu na kusomewa mashitaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa kinyume cha kifungu cha Sheria Namba 15, Kifungu Kidogo Namba 1 A cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Kifungu Namba 11 ya 2007.

  Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka watuhumiwa wote kwa pamoja, walikana mashitaka hayo na kesi hiyo kuahirishwa hadi juzi Desemba 22, mwaka huu kesi hiyo ilipokuja kwa kusoma maelezo ya awali.

  Hakimu Moyo alitaka upande wa mashitaka kuwakumbusha watuhumiwa mashitaka yao na baada ya upande huo kufanya hivyo, watuhumiwa walikubali mashitaka yao, ndipo hakimu alipotaka wasomewe maelezo ya awali ya kosa na washitakiwa kukubali maelezo hayo kwa
  mara nyingine.
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Takukuru bwana!!! Vipi wale wa richmond na rada.
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  haya yetu macho naq masikio,mala nyingi rushwa ndogo ndio zenye madhara ni bora uwe mla rushwa mkubwa hapa tz utapona kuliko hizi sh 38 na 29
  mapinduziii daimaaaaa
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ebony FM? mmenikumbusha enzi za njombe-iringa, nilikua nafanya kazi na shirika moja huko..yaani hicho kiredio kimejaa umbea na uzushi, ingawa sikua mwenyeji wa kule but hakikua na credibility ya kua redio, sikujua hata elimu ya watangazaji wake but walionekana ni watu wa kuokoteza tu, but vipi wale wa rushwa za uchaguzi? akina flani wa pale iringa na wale wagombea wengine? nimeuliza tu
   
Loading...