Yaani asubuhi ya leo nikitoka nyumbani nasikiliza magazeti redioni hili wazo lilinijia, 'hivi Kigoda ye hataki urais' sijamsikia, kumbe anatangaza!
Si bora sheria ikawekwa tu kuwa urais uwe mwezi mmoja mmoja ili kila mtanzania apate? Maana kama ni hivyo kila mtu anaweza. Tangu nipate akili ndio sasa napata kushangaa mno kwa hizi nia zinazotangwazwa hasa na wanachama wa CCM. Hivi wanaamini wana jipya au basi tu! Hivi wanajua wanavyotuchosha?
Kwa CCM kashfa ni jambo la msingi sana, % kubwa wenye/waliokuwa na kashfa ndio wako mbele kutaka urais na tena wanaungana mkono ka mazuzu vile. Ngoja tuendelee kuwasikiliza