Watambue watu, jitambue pia: Human Nature 01

Watambue watu, jitambue pia: Human Nature 01

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,990
Reaction score
4,361
Katika ulimwengu wa leo, wanadamu tunapambana na vikwazo anuai. Mara tu baada ya kuhitimu vyuo, tunajikuta ghafla tupo kwenye ulimwengu wa kutafuta ajira ama shughuli ya kuingiza kipato, maeneo ambayo maisha si rahisi na ushindani ni mkubwa sana.

Miaka michache iliyopita, kama ulikuwa na bahati wazazi wako walikuwa wakikupatia mahitaji yako na walikuwa pembeni kukuongoza, na hata kukulinda dhidi ya madhira ya dunia na walimwengu.

Unajikuta umebaki mwenyewe, bila kuwa na uzoefu wowote wa maisha binafsi. Unatambua sasa unatakiwa kujifanyia maamuzi ambayo yataathiri maisha yako yajayo.

Miaka michache iliyopita, taaluma na maisha ya ajira hayakuwa na machaguo mengi. Watu wengi wangeweza kubaki katika kazi/ajira kwa miaka mingi. Ndugu, jamaa, viongozi wa kidini na marafiki wa wazazi wetu wangeweza kutupatia mwongozo pale ilipohitajika.

Lakini kwa sasa ni nadra kupata msaada wa namna hiyo, kadiri ambavyo dunia inabadilika haraka sana. Kila mwanadamu yupo kwenye harakati za kustawisha maisha yake, watu wamekuwa wabinafsi kwa mambo yao wenyewe.

Ushauri na maelekezo ya wazazi yanaweza kuonekana yaliyopitwa na wakati na hayaendani na kasi ya maisha kwa sasa. Tunapopitia kipindi hiki cha maisha wengi huwa wanaamua kwa namna mbili.

Moja, baadhi huaamua kuvutiwa na mabadiliko haya, wakijichanganya kadiri ulimwengu unavyotaka. Bado vijana na wenye nguvu, wakiwa na fursa nyingi za maisha, huamua kujaribu kila kinachokuja katika ulimwengu huu wa teknolojia. Wakihama kutoka shughuli moja kwenda nyingine, wakiingia na kutoka katika mahusiano mbalimbali na kufanya mambo mengine mengi.

Kwa vijana hawa kuwa na fani moja na mahusiano thabiti kwao si muhimu kwa kuwa inaonekana kama kujifunga katika udhibiti usio na lazima. Kusikiliza maonyo, kufuata misingi ya kidini kwao ni mambo ya kizamani na yasiofaa. Kwao lililo sawa ni kufurahia maisha.

Lakini muda utakuja ambapo wanagundua kwamba yapo mambo ya muhimu katika maisha. Wakiwa wanafurahia uhuru wa kufanya chochote kadiri wanavyotaka, kwenda popote kama unavyotaka huwa linakuwa lengo kuu la maisha.

Mbili, wengine huwa wanaamua na kuishi tofauti, wakiogopa na kuwa na hofu juu ya mambo yanayoendelea duniani, huamua kujikita kwenye ajira ambayo inampa uhakika wa kuishi kwa kipindi kirefu na kutulia, inaweza kuwa inahusiana na kitu anachopenda au vinginevyo.

Huamua kuingia kwenye mahusiano mapema na hata kuoa na kutulia na mwenza wake. Hawa mara nyingi hubaki kuwa karibu wazazi wao. Lengo la watu wa kundi hili ni kutaka kuishi maisha ya utulivu ambao hata hapa duniani haupatikani.

Njia zote hizi mbili, huwa zina kawaida ya kusababisha matatizo kwa maisha ya mbele.

Kwa lile kundi la kwanza, kujaribu mambo mengi, kushiriki katika kila kitu duniani, kuwa na ushabiki wa kila jambo hufanya watu wa kundi hili kutoendeleza fani moja mahsusi. Hujikuta hawaweza kutuliza akili katika jambo moja kwa kuwa akili zao zimeshazoeshwa kuhama na kushiriki katika mambo mengi.

Uwezo na ufanisi wa kazi hupungua kwa kuwa wanahama na kubadili taaluma kila mara, hali mbaya ya kimahusiano kwa kuwa hawawezi kutengeneza mahusiano thabiti. Hawana uvumilivu na ustahimilivu, wanaweza kutaka mahusiano yanayodumu lakini hawa ujuzi wa kudumu katika mahusiano na ni ngumu kuacha kuwa huru katika mahuasiano, kudumu katika mahusiano na mwenza mmoja hugeuka kuwa kifungo na kukosa uhuru.

Kwa watu wa kudi la pili, kwa kuwa wameanza kuwa –commited mapema katika maisha, wakifika miaka thelathini huanza kupoteza umakini, huisi kuna vitu wamekosa katika ulimwengu halisi. Wanaanza kuhisi na kufikiri kwamba kuna vitu vingi vizuri wamekosa maishani kwa sababu ya woga tu, huona wenzao kama wanafaidi maisha na wana furaha zaidi yao.

Wengi hujikuta wakianza kupata hamu ya kufanya mambo ambayo hapo mwanzo waliona kuwa hayana maana, kama ulevi na kutafuta kufurahishwa kingono. Matatizo katika familia huanzia hapo. Unashangaa ndoa iliyokuwa bora kabisa inapata misukosuko ya hatari, mwanaume anaamua kutafuta nyumba ndogo na mwanamke anapata mtu wa kumridhisha nje ya ndoa.

Kwa makundi yote mawili, watu huwa wanafanya wanachofanya kwa sababu ya kukabiliana na matatizo ya kihisia zaidi.

Watu katika makundi yote mawili huanza kupitia hali ya kukosa utulivu, frustrations, discomfort, bila kujua chanzo cha yote haya ni nini?Wengi huanza kuona kuwa wamekosa lengo na mwelekeo wa maisha yao. Hali hii hutuletea maumivu ya kihisia mioyoni mwetu na usumbufu akilini.

Hapa ndipo watu huanza kuwa na tabia tofauti na kuanza kushiriki kwnye mambo ambayo alikuwa hayafanyi miaka iliyopita.

Unashangaa mtu unayemfahamu ambaye alikuwa mlevi, ghafla anaacha pombe?
Unashangaa mtu ambaye amekulia kanisani/msikitini ghafla anaasi imani?
Unashangaa mume wako aliyekuwa mwaminifu wa kiwango cha juu ghafla ana michepuko isiyohesabika?

Unashangaa kugundua mkeo ambaye hukuwahi hata kumtilia mashaka anatoka na kijana muuza vocha mtaa wa pili?

Tutaendelea sehemu ya pili...
Unashangaa kugundua mkeo ambaye hukuwahi hata kumtilia mashaka anatoka na kijana muuza vocha mtaa wa pili?

SEHEMU YA PILI:-

Sisi wanadamu tunapenda kuamini kwamba tuna mwelekeo sahihi katika maamuzi na tumepevuka vya kutosha kufanya maamuzi katika maisha yetu. Tunafanya maamuzi katika kwa kutumia akili katika kile tunachodhani kuwa kina manufaa kwa maisha yetu. Tuna nia huru ya kuamua, tunadhani tunafahamu kuwa sisi ni nani. Lakini katika maisha halisi ndipo tunapogundua kuwa ‘’self-opinions’’ zetu huwa zinaanguka katika matukio kadhaa. Mara ngapi umekaa ukajutia maamuzi uliyofanya?
Katika muktadha wa mahusiano ya kimapenzi, tunapoanzisha mahusiano ya kimapenzi, huwa tunafanya maamuzi ambayo wakati mwingine ni vigumu hata kuyaelezea kwa nini ulifanya.


Wengi wetu huwa na bahati ya kuwa na mahusiano yaliyofanikiwa walau mara moja katika maisha lakini pia tutakuwa na mahusiano mengi amabyo hayatakuwa na mafanikio na kushindwa. Mara kadhaa tunarudia kufanya maamuzi mabaya katika mahusiano kana kwamba tunasukumwa na zimwi ndani ya mioyo yetu.

Tunajiridhisha kwa kujiambia wenyewe kuwa tulifanya baadhi ya mambo kwa sababu tulikuwa kwenye mapenzi, tulipitiwa na kichaa cha mapenzi. Tunadhani tukiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi basi ni sawa tu kufanya baadhi ya mambo ambayo huwa tunakuja kujutia baadaye.

Kiukweli, tunapokuwa kwenye mahusiano ndipo ambapo wengi huonyesha tabia zao halisi, ukitaka kujua mtu ana ujinga basi mtazame akiwa katika mahusiano ya kimapenzi, ukitaka kujua mtu ana upendo basi mtazame akiwa kwenye mapenzi, ukitaka kujua mtu mwenye hasira mtazame akiwa kwenye mapenzi.
Embu tuangalie mabadiliko ya kawaida yanayotokea kwa watu wakiwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Akili zetu huanza kuwa katika hali ya kuzingwa(distraction), kadiri unavyoingia zaidi katika mapenzi ndivyo usikivu (attention) huamia kwa mtu mmoja(mpenzi wako). Tunaanza kuwa vichaa bila kujua , tunaanza kusahau mambo mengine na kuwekeza katika mapenzi pekee.

Wanadamu wanapenda na kusukumwa kujionyesha kwa namna fulani kwa jamii, tunataka kuonyesha sifa njema kwa ulimwengu, sifa zinazoonyesha nguvu na umakini wetu. Lakini tunapokuwa kwenye mapenzi, tabia tofauti huanza kujitokeza. Najua una ushahidi wa kutosha, kabla ya kuwa wapenzi , mwanamume alionekana kuwa mpole na anayejali sana, lakini baada ya kuanza kuwa wapenzi anaanza kuwa mkali na kuonyesha tabia ambazo hakuzionyesha hapo awali. Wengi husema kuwa mpenzi wangu/mke wangu/mume wangu amebadilika, ila ukweli ni kuwa huyo ndivyo alivyo.

Mtu ambaye hapo awali alionekana kuwa imara na thabiti ghafla anakuwa dhaifu sana, mtegemezi na mwenye akili isiyotulia. Dada aliyeonekana mpole, mtulivu na mstaarabu ghafla anaanza kuwa mwenye kulazimisha mambo, asiyeelewa, m-binafsi na anayepaniki hata kwa vitu vidogo.

Tunapoluwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tunakuwa tunapitia hofu na kutokujiamini lakini kwa kiwango kisicho halisi. Unashangaa mkeo anaogopa wewe kwenda sokoni na dada wa kazi? Kwa nini unaogopa kijana wa ng’ombe kuzoeana na mke wako? Hofu uliyoikuza mwenyewe katika mfumo wa akili yako.
Tunapata hofu ya kusalitiwa, hofu ya kutopendwa, hofu ya kuachwa. Tunapata hali ya kukosa utulivu wa akili, kutoka kwenye hisia za upendo na kuhamia kwenye chuki, kutoka hisia za kumuamini mpenzi wako unapata hisia za kutokumuamini kabisa.
Mara nyingi kila mmoja wetu hupenda kudhani kuwa ana uwezo mzuri wa kupima na kujua tabia za wengine. Lakini tunapokuwa kwenye mapenzi huwa tunaona vitu tofauti kabisa, tunaweza kufanya kosa la kuona mwanaume mpole kuwa ni ishara ya upendo, mwanamume muongeaji kuwa ni ishara ya upendo, na mwanamume mpole kuwa ishara ya kujivuna. Dhana zote hizi zinaweza kuwa sio sahihi.

Wengine wanaweza wakaona na kujua tabia halisi ya mtu na kutuonya lakini ukiwa katika mapenzi hutasikiliza, kwa kuwa wewe unaona tofauti.
Na mara nyingi wengi wetu huishia kufanya makosa yale yale katika kila mahusiano tunayoingia kwa kuwa tunakosa umakini katika maamuzi.
Kwa nini mtu anaingia kwenye mahusiano zaidi ya mara tano na yote yanashindwa kuendelea?

Unadhani tatizo ni la hao uliochana nao? Acha nikwambie, tatizo ni wewe kwa kuwa umekosa uwezo wa kujua na kupima tabia za watu kwa kuwa huwa wanakulaghai wakati mnapotaka kuanzisha mahusiano.
Wanakuonyesha tabia nzuri unazozitaka, huku wakificha tabia hali. Lakini wakishakuwa kwenye mahusiano na wewe ndipo tabia halisi hutokeza.

Tutaendele sehemu ya Tatu
 
Naona hii kiongozi umedonoa na kuchanganya kutoka kwenye kitabu cha Mwanafalsafa John Green katika kitabu kinachoitwa: Laws of Human Nature.

Ahsante sana uzi umetulia ila kwa kuwa hakuna kugegedana humo ndani raia hawatasoma.
 
Uzi murwa sana Ila Kwa dunia ya sasa ni Jambo jema sana na utafurahia maisha kama ukifanya kila kitu Kwa kiasi unapenda kungonoka fanya Kwa kiasi bila kuzidisha ambapo hutatulia na mmoja au wawili unapenda pombe fanya Kunywa kwakiasi utaifurahia unapenda club nenda Kwa kiasi usiwe mlowezi nafurahia maisha Kwa staili hii nakunywa nafika kipindi natulia kabisa ata mwaka au miezi mi3 sinywi nangonoka Ila inaweza pita miezi mi2 sina penzi la nje easy na happy
 
Madini juu ya Madini.
Ahsante sana kwa Uzi mzuri Rafiki.

''Tatizo ni wewe kwa kuwa umekosa uwezo wa kujua na kupima tabia za watu, wanakulaghai wakati mnapotaka kuanzisha mahusiano.''​
 
Back
Top Bottom