Watalii walalamikia Trafiki Polisi Tanzania

Watalii walalamikia Trafiki Polisi Tanzania

Nimemskia IGP Sirro akisema ukiona umeonewa usilipe faini uende mahakamani.

Nikajiuliza mahakama zenyewe ndiyo hizi ambazo kina Mbowe wanasotea dhamana kwa miezi 3 sasa?

Kama nia ni njema kwa nini pasiwe na hotline ya kulalamika na kupata ufumbuzi mara moja kama kwa makampuni ya simu?

Polisi traffic ni janga. Ajabu wenye mamlaka wanajifanya kutoliona.


Kama serikali ina nia njema inge replace hao watu na camera, hili litakuwa na faida mbili au zaidi.

Faida ya kwanza, camera zitasoma centrally na hapatakuwa na mambo ya rushwa na hivyo kuiongezea serikali mapato halali ambayo kwa kiasi kikubwa yanapotelea mifukoni mwa watu kwa njia ya rushwa.

Faida ya pili ni kuongeza mahusiano mema baina ya serikali na raia wake, kwa hivi sasa human errors zinazofanywa na traffic police zinawafanya raia kuichukia kabisa serikali

Faida nyingine ni kwamba askari watakaokuwa replaced na camera watakwenda kuongeza nguvu kwenye maeneo ambayo hayawezi kufanywa na vifaa vya kielectronic kama kupambana na ujambazi nk
 
Trafiki polisi bila kukaa barabarani hawana kazi. Ndio maana wanachukua waliofeli. Hata ukiwa na F zote unaweza kupiga faini ya spidi, na hiyo ndio kazi pekee wanajua. Napendekeza kazi ya trafiki wapewe darasa la saba kuongeza ajira nchini
Kweli wengi wa trafic ni form four division 4 za points za mwisho kabisa au wale waliofeli kabisa kwa kupata 0 kabisa isipokuwa wengine wanatumia vyeti vya kufoji kama bashite msako wa vyeti fake ungepita huko na kwa viongozi wa siasa wengi wangefyekwa ikiwa ni pamoja na wanasiasa kama daud
 
Toa link ya Trip Advisor tuwaambie watalii kwamba huo ni maradi wa serikali kukusanya mapato
 
Ni kweli kabisa maneno yako,Sehemu nyingi sana sio hapa ila kwenye Nchi za Kiarabu na sehemu zingine huo ndo mfumo wao wa kutumia Camera,ukiendesha spidi zaidi tofauti na kibao unarekodiwa au umefanya kosa lolote la barabarani unarekodiwa ila mwisho wa siku labda unataka lipia bili ya maji au kitu chochote kila unakuja kuona una deni la kosa ulilolifanya.hio inataka mfumo mmoja wa malipo ya Serikali,kama vile maji ,umeme,hospital na nk vyote vinaingizwa ktk system moja.wakati umefika sasa nasi tubadili huu mfumo wetu na hii itasaidia askari wetu kutokukaa mapolini na kuumwa na mijoka kwa kufizia kupiga tochi magari,naimani hayo yanawezekana tu
Kama serikali ina nia njema inge replace hao watu na camera, hili litakuwa na faida mbili au zaidi.

Faida ya kwanza, camera zitasoma centrally na hapatakuwa na mambo ya rushwa na hivyo kuiongezea serikali mapato halali ambayo kwa kiasi kikubwa yanapotelea mifukoni mwa watu kwa njia ya rushwa.

Faida ya pili ni kuongeza mahusiano mema baina ya serikali na raia wake, kwa hivi sasa human errors zinazofanywa na traffic police zinawafanya raia kuichukia kabisa serikali

Faida nyingine ni kwamba askari watakaokuwa replaced na camera watakwenda kuongeza nguvu kwenye maeneo ambayo hayawezi kufanywa na vifaa vya kielectronic kama kupambana na ujambazi nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemskia IGP Sirro akisema ukiona umeonewa usilipe faini uende mahakamani.


Hayo ni maneno ya mtu aliyekosa kabisa akili ya ubunifu na ni maneno ya mtu anayependa kuvuna kwa mrija, yawezekana ananeemeka na rushwa toka kwa askari, mtu mwenye busara angetumia muda wake mwingi kuonyesha tofauti kati ya anayefanya kazi kwa mazoea na yule anayekabiliana na changamoto mpya kila wakati
 
Back
Top Bottom