Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,589
- 28,755
Jawilat hibu hili swali basi utatusaidia wengi, maana dawa za dukani nazo ni gharama sana na nyingi ni fekimkuu Jawilat embu nifafanulie hiyo tiba mbadala. Kitunguu saumu ukikitwanga unaweka kwenye.maji au pumba? Unaweka kwa ratio ipi? Muarobaini na alovera ukiiloweka na kuitwanga unawekaje kwenye pumba?
Aisee kumbe na kuku wanaweza kupata shinikizo! Bas ndo maana Mama yangu kuku Wake wanaumwa anawafungia!
umefikia wapi na huu ugonjwa? Mimi nafikiri ni Mareks ila haina dawa sababu ni virus inaua kinga hivyo ni lishe bora na kutibu magonjwa nyemelezi. Nafikiri hata kwenye uzi wa zijue mbinu zangu Kubota aliongelea hili tukajua ni ndui, lakini ukiangalia ndui haina vifo vingi au kusababisha uambiwe uuze au uue kuku wote na kuanza moja. Nitaweka maelezo kidogo kutoka link na tiba zake. Haiwezi kuwa shinikizo kwani kuku wake wako active wanajitafutia na nafikiri msimu wa mvua umeisha wadudu na majani hamna hivyo lishe unajionyesha. Dalili zake ni macho kuziba kuweka uvimbe ila sio vidonda vya ndui na kupooza kisha kufa . Umri wiki kumi na mbili ndio unawaadhiri zaidi. Dawa ni antibiotic kutibu opportunistic kama mafua, typhoid, mafuta kwenye vidonda lakini kikubwa lishe bora.
Hali ndiyo inazidi kuwa mbaya,leo wakati ninawafungulia jogoo ametoka akiwa mzima,ghafla nikamuona ana rudi akiwa ana tembea kama ana nyatia kitu vile huku akiwa amelifinya tumbo kama vile tumbo linamsokota.Nilipomkamata na kumfungia kwenye chumba hakumaliza hata saa moja akawa amekufa.Mwingine alikuwa ana taga ameingia kutaga,alipotaga tu naye akafa hapohapo kwenye kiyota.Mwingine alikuwa na vifaranga vidogo akawa ana fukuzana na kuku wenzake alipowafukuza kuku wenzake baada ya kuvirudia vifaranga vyake naye alianguka na kufa hapohapo.Kinachonishangaza ni kwamba hawa kuku hawajikunyati kwa kuinamisha kichwa chini wanasimama wima huku wakiwa wamefinya tumbo na wanatembea kwa kunyatanyata huku wakiwa wameinua shingo zao juu.
umemuona mtaalamu yoyote? unawapa chakula gani? nakushauri anza kuwapa chakula wadogo starter wakubwa finisher, jaribu hii antibiotic tylosin kama hujapewa dawa zozote ni broad spectrum. jitahidi watulie ndani maana ni wagonjwa na wape maji ya kutosha. Jaribu kuwatenga wadogo na wakubwa labda mama zao ili kuwawezesha kula vizuri na kutoambukizana magojwa.
Nimewaita bwana mifugo 2 wamekuja kuwaona wakasema kuwa ni kideri,Ila nimeshindwa kuamini kama ni kideri kweli kutokana na namna ambavyo vifo vinavyotokea dalili zenyewe siyo zakideri,Kuku wanapotembea hawaonyeshi dalili zozote za kuumwa,dalili za kuumwa zinapojitokeza tayari ana kuwaameshaisha kabisa,kinachofuata ni kufa moja kwa moja.Watalamu wamenipa OTC 20% ndiyo ninayowawekea kwenye maji ila hii dawa uliyo ni shauri nitaitafuta ni itumie inaweza kunisadia kwani kuna baadhi ya kuku wana mafua yasiyoisha na nilisoma mahali kuwa dawa hii ina uwezo wa kutibu na mafua pia.Kwa vile hawa kuku nimewafuga kwa ufugaji huria sehemu kubwa huwa wanajitafutia chakula na hili ndilo lililosababisha yote haya ila ninapowafungulia huwa ninawapa pumba ambazo zimechanganywa na dagaa au uduvi.Baadhi ya kuku nimesha wafungia tayari,wenye vifaranga nimewafungia chumba chao pamoja na vifaranga vyao.
OTC ni tetracycline kwa kweli sio broad spectrum kihivyo ila tylosine itasaidia magonjwa ya tumbo na hewa ambayo ndio kuku wengi huumwa na kufa. kila la heri ila jitahidi chakula hasa kwa hao wadogo kipindi hiki wanaumwa