Wang Shu
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 2,563
- 3,708
Wakuu salaam
Nimekuwa mtu wa kujaribu kwa vitendo hili zoezi mara kwa mara katika siku tofauti nimelifanya takribani siku 8, sio siku zote mfululizo.
Muda ninaofanya meditation kuanzia saa 7 usiku hadi saa 10 kwa maeneo niliyopo huu muda ni rafiki na tulivu sana.
Nilifanya siku 4 mfululizo lakini nilishindwa kutuliza akili na mawazo sehemu moja, nikajipa likizo kama wiki moja nikiwaza nashindwaje nikapitia baadhi ya thread nikaongeza maarifa.
Kwa mara ya tano baada ya wiki kupita nilijiandaa tangia asubuhi nikajisemea kuwa leo usiku nitafanya meditation na ilipofika usiku eneo lilikuwa linanisubiri mimi tu nianze.
Siku hiyo ya tano ilikuwa ya tofauti sana tena sana nilifanikiwa kirahisi, ndio niliona matokea ya meditation lakini nilishindwa kuvumilia kutokana na vitu nilivyokuwa nahisi mwilini na kuona hali nisiyoilewa.
Mwili wangu uliganda nilikuwa kama nimechomwa sindano ya ganzi siwezi kuinua hata kidole macho pia nilishindwa kufumbua vitu vinaingiliana yaani sielewi mapigo ya moyo yakienda mbio sana, nilikuwa kama nazungushwa kwenye kiti.
Ilinikuta hofu kwa hali ile nikaanza kujaribu kutoka niache ilikuwa ngumu kiasi maana sikuweza kujifanyia chochote, lakini baadaye nilifanikiwa na sikuendelea lakini niliona mabadiliko makubwa sana, mwili mwepesi na baada ya hapo nililala usingizi mzito, nikasema mwanzo mzuri.
Kwa mara ya 6 siku iliyofuata nilifanya tena nikashindwa tena sikufikia hata robo ya siku iliyopita, niliendelea kurudia siku 3 mfululizo lakini nilishindwa kabisaa nimeshindwa kujua tatizo.
Mazingira ni yaleyale nafanya gizani nikiwa nimekaa mkao uleule wa siku niliyofanikisha lakini nashindwa kuupata mwendelezo wake.
Kwa sasa nimejipa muda wakupumzika sifanyi lakini naitaji kujua hii imeekaje nifanya nini? Niongeze kitu gani?
ili niendelee kuyaona matokeo kama yale au zaidi!!?
Nawasilisha..