Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,274
- 25,322
Serikali mkoani Singida imewaagiza wakuu wa wilaya kuwatafuta na kuwakamata baadhi ya watu wanao chapisha kadi za kliniki na kuwauzia wakina mama wajawazito.
Mkuu wa mkoa wa Singida Daktari Rehema Nchimbi ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akikabidhi vitanda vya kujifungulia na kulazwa wagonjwa pamoja na mashuka yaliyotolewa na mheshimiwa Rais katika kituo cha afya Ikungi na kusema kuwa kadi za kliniki zinatolewa bure na serikali na hazitakiwi kuuzwa.
Akisoma taarifa ya afya ya wilaya ya Ikungi mganga mkuu wa wilaya ya Ikungi Daktari Christopher Mtomakaya amesema wilaya ina upungufu wa vitanda vya kulaza wagonjwa na ambavyo vinatumika ni asilimia nne pointi tatu tu.
Kwa upande wake mbunge wa Singida Magharibi mheshimiwa Elibariki Kingu ameunga mkono juhudi za mheshimwa rais kwa kuchangia vitanda vya kujifungulia thelasini na nne katika hospitali , vituo vya afya na zahanati za wilaya ya Ikungi,huku wakinamama waliokutwa na ITV wakiwa kliniki wamesifu juhudi za rais za kutoa vitanda vya kujifungulia nchi nzima.
Chanzo: ITV