Mwamba Usemao Kweli
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 744
- 186
Na Christopher Nyenyembe-
BABA wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliwahi kusema wakati wa uhai wake pale alipojaribu kuangalia na kuona utitiri wa vyama vingi vya siasa kuwa ana shaka havitakuwa na nguvu ya kutosha ya kuiondoa CCM madarakani.Alibainisha kilichokuwa kimejificha moyoni kwake kuwa kundi hatari na lenye nguvu za kutosha litakaloweza kukiangusha chama hicho litatoka ndani ya CCM na hao wataungana na chama angalau kimoja ili kutimiza azima yao.
Hakusita kukitaja chama cha siasa kutoka upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ni chama alichokiona kuwa kipo makini, kina sera nzuri na aliamini kuwa mfumo mzuri wa uongozi uliopo utakisaidia chama hicho kujijenga zaidi na kuwa chama kikubwa.Huo si utabiri wangu na hayo hayakuwa mawazo yangu, ni wazi kuwa alichoweza kukisema Nyerere kunaonyesha jinsi alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kutafiti, kuchunguza na kubainisha uhalisia wa jambo.
Uzuri uliokuwepo enzi za Nyerere ni kwamba alikuwa na muda wa kutosha wa kuwasoma viongozi wengi wa kisiasa waliokuwepo, aliwajua vizuri wana CCM wenzake na aliwajua vizuri sana Watanzania wengine walioamua kuunda vyama vya siasa.Nyerere hakuwa mtu wa kukurupuka, alikuwa kiongozi aliyethubutu kuyasema yale aliyoamini kabisa kuwa ndio msimamo wake na mwelekeo wake kama mtu aliyekuwa akiiangalia Tanzania kwa jicho la jumla bila ubaguzi.Alichokisema Nyerere kinasukuma uhalisia wa mambo, alijua fika kuwa watakaoiondoa CCM madarakani watatoka ndani ya chama hicho, dalili zinaonyesha wale waliojificha mafichoni wameanza kutoka.
Dhambi ya ubaguzi, dhambi ya udini na ukabila, dhambi ya kuhujumiana na dhambi ya tabaka la matajiri na masikini ndiyo inayozidisha Wana CCM wengi waliokuwa wavumilivu kwa muda mrefu waamue kuondoka mapema.Kadiri siku zinavyozidi kwenda hali inaonyesha kuwa hofu na shaka ya Mwalimu Nyerere kuwa utitiri wa vyama vingi vya siasa si mustakabali wa kuwa na vyama vyenye nguvu bali vingi vitasaidia kuwepo kwa utengano na utawanyaji wa wapiga kura.Mbali na wasiwasi huo bado utabiri wa Nyerere una mashiko makubwa alipowaaminisha Watanzania wengi kuwa aliiona CHADEMA ni mkombozi na chenye mfumo mzuri wa kiuongozi na hakika hali hiyo ndivyo inavyoendelea kushamiri.Ili kuhakikisha kuwa haki na wajibu wa wananchi katika harakati zao za kuvijenga vyama vyao na kuvipigania mara kadhaa alikuwa akivionya vyombo vya dola kuwazuia wananchi wasiwabebe viongozi wao.Alikataza kuwaingilia wananchi katika misafara yao ya kisiasa, kuwa wale waliokuwa tayari kuwabeba juu kwa juu viongozi wao waachwe wawabebe na wale waliokuwa tayari kusukuma magari bila mafuta waache wafanye hivyo, kuwa hayo ndiyo yalikuwa mahitaji ya kisiasa.Kwa kuamini kuwa kuwazuia wananchi wasiwabebe viongozi wao au kuwazuia wasisukume magari yao kumesaidia kuwaongezea zaidi umaarufu viongozi wa kisiasa kutoka upinzani na kufifisha nuru iliyokuwa iking'ara kwenye chama tawala, nuru ambayo haiwezi kurejeshwa.
Nyerere aliwapa wosia Watanzania mapema mno, alikionya chama tawala na serikali yake kuwa visithubutu kuwaonea wapinzani, visithubutu kusababisha damu ya Watanzania kumwagika kwa ajili ya mambo ya siasa.Hakupenda kuona Watanzania wanamwaga damu kwa ajili ya kuwapata viongozi wao, hakupenda kuona viongozi waliokosa uadilifu ndani ya CCM waking'ang'ania kwa gharama yoyote ile kuweza kuingia Ikulu, Nyerere aliwataja na kuwakataa moja kwa moja.
Aliowakataa Nyerere leo hii wanazidi kujipanga na chaguo la wao kwa wao kutaka kuingia Ikulu, wanataka kuingia kwa nguvu zozote zile na ushindani wao unaoendelea kuwepo ni chukizo kubwa kwa Watanzania wengine wapenda amani na Watanzania wengi wanaoamini kuwa hii si Tanzania waliyokuwa wakiitegemea.
Watanzania wanataka kuiona nchi yao ikiongozwa na viongozi wa watu, hawataki kuona nchi ikiongozwa kwa nguvu za fedha, hawataki kuona urais ukinunuliwa kutoka makanisani na misikitini.Nyerere hakuwa kiongozi wa rushwa, alisema rushwa ni adui wa haki, pale ambapo fedha chafu zinatumika kwa ajili ya kuupata uongozi lazima zitashawishi kiongozi wa aina hiyo atakapoingia Ikulu abariki uuzwaji holela wa rasilimali za nchi.Wale wanaojua madhara hayo wameanza kutoka mafichoni, wameanza kujiandaa sasa ili kuweza kukiondoa madarakani chama kilichoamua kuwabagua watu maskini na kuwakumbatia matajiri.Nani anayeweza kubisha kwa hilo kuwa wafanyabiashara wengi walioamua kuingia kwenye siasa hawakuingia kwa ajili ya kulinda na kutetea hali bora na usalama wa raia wote, wameingia madarakani kwa ajili ya kulinda masilahi yao.Wameingia kwenye siasa kwa kupitia mlango wa CCM ili kuhakikisha kuwa mambo yao hayawezi kuwaharibikia,watalindwa na watakuwa na kinga hata kama watajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Aliowakataa Nyerere ndani ya CCM--watajwe sasa kuwa ndio vinara wa uhujumu uchumi, ndio waliopo kwenye orodha ya ufisadi, ndio wanaowatumia wasanii kusafirisha dawa za kulevya na ndio wanaotaka kuingia Ikulu.Kama hali iko hivyo ni wazi kuwa Watanzania wapenda amani, wanaoitakia heri nchi yao si kwa sura ya UCCM pekee yake isipokuwa waliojeruhiwa na mfumo huo na wale ambao hawataki kuvuna dhambi ya usaliti sasa wameanza kutoka mafichoni.Vyama vya siasa vyenye nia na dhamira ya kweli ya kutaka kuchukua nchi mwaka 2015, vinapaswa kutumia mwanya wa utengano uliosababishwa na ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa uliojengeka ndani ya CCM ambayo haitaki kukubali kuwa wanaoanza kutoka mafichoni wamechoka.Kuendelea kuamini kuwa bado Watanzania wengi wana mawazo ya mwaka 47 huko ni kuendelea kujidanganya, uonevu na upendeleo wa wazi katika kuchaguana na kupeana madaraka kutakuwa sehemu ya mapito ya wapenda mabadiliko.Kwa mtazamo wa Nyerere na uchambuzi ninaoufanya, CHADEMA wanapaswa kujijenga zaidi kama chama kikubwa cha upinzani, sifa zote zipo na changamoto nyingi pia haziwezi kukosa, wanaotamani kuiona Tanzania mpya wapo wengi kuliko wanaoihitaji Tanzania ya zamani.
Mabadiliko ya uongozi ndiyo dira pekee inayoweza kuleta matumaini mapya, ushindani wa kisiasa ndio ukomavu wa kujenga demokrasia ya kweli, Watanzania wanaweza kujiongoza kwenye mipango yao-kusukumwa au kutegemea nguvu ya vyombo vya dola.Amani iliyopo ndilo tunda la ukombozi na ustawi wa nchi yenye neema, ndani ya neema iliyopo kumegeuka kuwa tanuri la shida na mahangaiko, tanuri la umaskini na maradhi yanayotishia maisha ya Watanzania wengi.Watanzania tumekalia kiti cha dhahabu, tumewekewa meza ya tanzanite, tumetandikiwa zulia la almasi na tunalalia mto wa vito vya thamani lakini tunaongoza kwenda kuomba nchi za ng'ambo.Mazingira hayo na aina ya maisha tuliyoishi kwa muda mrefu kunawafanya wale waliojificha mafichoni waanze kutoka na hao hao ndio watakaoiua CCM na wengi ndio wanaohama kuelekea safari ndefu, safari ya mwaka 2015.
Basi inawapasa wale walioshika kisu kwenye mpini, wakashindwa kuwapatia Watanzania nyama iliyonona kisha wakaamua kuvuta kisu chenye makali na kuwakata watu wanyonge ambao wameamua kutoka mafichoni, wataungana na wanasiasa wazalendo ili kuleta mabadiliko, si wajinga, isipokuwa dalili za mabadiliko zipo wazi.
Source: Tanzania Daima.