Wataka Urais CCM 2015 'watia sumu' CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wataka Urais CCM 2015 'watia sumu' CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 13, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  • Wapenyeza rushwa kuivuruga
  • Vigogo CHADEMA washitukia

  KATIKA kile kinachoonekana mkakati wa kuupata Urais kwa gharama zozote, kigogo mmoja anayetajwa kuwania nafasi hiyo ya juu, anadaiwa sasa kupenyeza sumu ya rushwa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Taarifa za ndani ya kambi ya mgombea huyo ambaye kwa sasa amejikita ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zinaeleza kwamba tayari amekua na mazungumzo na baadhi ya vijana ndani ya Chadema kwa nia ya kukihujumu chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

  Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba, uongozi wa juu wa chama hicho umekua makini na njama hizo na kwa kutumia makachero wake, umejipanga kukabiliana na yeyote anayekusudia kufanya hujuma.

  "Ameanza kushirikiana na Vigogo wenzanke hasa wale wenye "permanent interests" kuhakikisha wanaingiza mbegu ya rushwa ndani ya Chadema kwa kuwarubuni vijana walioko ndani ya chadema ikiwa ni pamoja na kurecruit wapya waingie kwa nia moja ya kuvuruga mikakati ya upinzani.

  "Mkakati huu umeanza muda mrefu na unaanza kuota mizizi. Vijana hawa watakuwa wanapinga kwa nguvu zote kunapotokea uelekeo wowote wa baadhi ya vigogo wazito wanaoweza kuihama CCM na kujiunga na Chadema kutokana na mizengwe na rushwa," anaeleza mtoa habari ndani ya kambi ya mgombea huyo.

  Tayari baadhi ya viongozi makini ndani ya Chadema wameshagundua mpango huu unaoendeshwa nje ya chama na huenda wakatoa tamko hivi karibuni kuwaweka sawa wanachama wake kuhusu mbinu hii ya kijasusi inayoendeshwa na walafi wa madaraka ndani ya chama tawala CCM.

  Ni hivi karibuni muasisi wa CHADEMA mzee Edwin Mtei ameonya tabia ya baadhi ya viongozi wake kuanza kujipanga kuwania Urais mwaka 2015.

  Pamoja na Mtei kutofafanua, baadhi ya watu ndani ya CCM na CHADEMA wameuelewa kwa undani mwanasiasa huyo mkongwe kutokana na angalizo ambalo linalenga kuwatahadharisha na mbinu za kutaka kuwagawa.

  "Watu wamejipanga kupata Urais na wako radhi kumnunua mtu yoyote ili njia yao iwe nyeupe. Ule msemo usemao kuwa kwenye siasa hakuna uadui wa kudumu ila kuna maslahi ya kudumu umeanza kuonekana kwenye chaguzi hizi za CCM zinazoendelea.

  "Ule wimbo wa kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi umesahauliwa na badala yake wahusika hao wameonekana ni vinara baada ya kupitishwa na Vikao vikuu vya CCM vilivyoasisi falsafa hiyo ya kujivua gamba," anaeleza.

  Katika kuonyesha kwa undani kinachoendelea ndani ya CCM, mtoa habari huyo anazungumzia kuwapo kundi la wana CCM wanaohofia nguvu ya Chadema baada ya 2015.

  "Zile permanent interests zimeonekana dhahiri hasa pale 'wastaafu watarajiwa' wamejikuta wakiungana kimkakati katika kuwazuia wale wanaoonekana kuwa tishio pindi wakipata nafasi ya kuingia kwenye vikao vya maamuzi. Taswira halisi ni huu muenendo wa nafasi za NEC, Wenyeviti Wilaya na mikoa unaoendelea ambao umebeba sura halisi ya kuweka rushwa mbele kwa ajili ya kuweka watu wao na kusahau kabisa kuwa uongozi ni kwa maslahi ya Taifa zima na si kwa ajili ya kundi dogo la wachache," anasema.

  Tayari kumekua na mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi mbalimbali wa mijini na vijijini kutokana na nguvu kubwa ya Chadema inayotokana na kampeni za kila siku nchi nzima za chama hicho zilizoanza na 'operesheni sangara' na sasa 'Movement for Change-M4C'.

  Chanzo: Kulikoni - Oktoba 12, 2012
   
 2. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Zitto Kabwe ndo anajimaliza mwenyewe kisiasa hivyo. CCM wabaya sana!! Kakijana kamebebeshwa magamba ile mbaya!
   
 3. A

  Apex JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 429
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  EL on work! Kweli 2015 ccm hawana chao cdm 2jipange vizuri na pale kijana,mzee yeyote anaefanya kazi za kukihujumu chama anapobainika basi hatua stahiki zichukuliwe bila kujali cheo,rangi,umri,kabila,elimu na kanda kwa maslah ya cdm na tz, Mungu ibariki cdm
   
 4. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wamekatwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Chadema lazima eawe macho, maana watu wanajipanga. Chama kimekua kazima kijiendeshe kisayansi zaidi. Watumie mbinu sahihi kubaini ujasusi, ili wasije kukurupuka dakika za mwisho 2015
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono andishi hili mia kwa mia.
   
 7. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Chama kina makamanda makini hakika watashughulikiwa vibaraka wote na watajuta kurudisha nyuma mapambano haya watakapohukumiwa na raia mnyonge anayehitaji ukombozi toka kwa manyang'au magamba...
   
 8. w

  wamwala Senior Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inahitajika uimara wa hali ya juu sana katika kupambana na hawa Magamba, bt naamini ukombozi upo unakaribia Magamba yatashindwa tu kwa namna yoyote ile
   
 9. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,715
  Likes Received: 17,763
  Trophy Points: 280
  Siku tukifanikiwa kumchomoa Zitto Kabwe CDM, chama hiki kitadumu sana, hata kama hakitachukua nchi 2015
   
 10. p

  promi demana JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dhambi ya unafiki miongoni mwa washabiki na wapenzi na viongozi wa CHADEAM soon itawatafuna kwani hata sisi ambao ni washabiki ambao si wanachama tunajua ila nyie mnajifanya hamjui.

  Acheni kuogopa na hilo kundi baya ni hili hapa chini.

  John shibuda, Zitto kabwe, Juliana shonza, Mtela mwampamba, Benard saanane, Habib Mchange, Nyakurungu, Rose kamili, Dr.kitila Mkumbo, erasto tumbo, Adamu chagulani, Henry matata, yule mbunge vitimalum kigoma ambaye ni binamu wa Zitto. ........

  Chadema kuweni makini na hawa watu na anayebisha aje nimchambue mmoja mmoja.
   
 11. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,278
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. i

  iseesa JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna sababu ya kumchomoa. Muacheni abaki tujifunze zaidi kutoka kwake. Ukisamfahamu mtu alivyo ni changamoto kwako na umemaliza kazi
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  promi demana

  Hapa ndipo mnapoanza kupotoka kwa kuingia mwenye mtego wao kwa kuanza kushutumu watu bila kufanya utafiti...

  Ni lazima Chadema kiwe makini na kiendeshe mambo yake kisayansi zaidi kuliko kuendeshwa mambo kwa hisia. Kuwepo chombo maalumu cha utafiti na ikibidi washirikine na wataalamu wa nje ya nchi ambao nuna hakika wapo wenye nia njema na Chadema na nchi kwa ujumla, vinginevyo tutajikuta nchi inaingia mikononi mwa mafisadi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. k

  kinai Senior Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika vita yoyote lazima kuna watakaokufa, kujeruhiwa na wasaliti hawakosekani. Cha muhimu ni kujipanga dhidi ya wasaliti. Hili ndio kundi baya na hatari sana
   
 15. p

  promi demana JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo hakuna cha kuficha kwani ukweli ndio huo hapo juu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Subira yavuta kheri. Siasa za kutumiwa zitawabakisha watz utumwani na mikononi mwa wakoloni ccm.
   
 17. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kabisa. Pamoja na kwamba hao wengine sijaweza kufuatilia nyendo zao lakini Dr. Mkumbo ninamwona kama mtu hatari kuliko hata Zitto. Dr. Mkumbo ameandika makala katika gazeti Raiamwema la tar. 10 - 16, 2012, yenye kichwa cha habari: "Unafiki wa Zitto na wapinzani wake". Kadiri ya makala yake ambapo ametoa ufafanuzi waq kisomi kwanini ni halali kwa Zitto kuonesha nia yake ya kugombea urais, lakini nina mashaka sana na Dr. Mkumbo. Ameeleza tu kwamba katika mfumo wa kiliberali Zitto hajakosea kujitokeza kuwania nafasi ya urais, kwa hoja kuwa katika uliberali nafasi ya madaraka ni jambo la mtu binafsi.

  Dr. Kitila Mkumbo, yeye kama kiongozi wa CDM hajaeleza maana ya kisiasa kuhusu kitendo cha Zitto kusema kwamba asingegombea ubunge mwaka 2010 na baadaye akagombea. Hajatueleza alipogombea nafasi ya uenyekiti CDM mwaka ule na hatimaye akajitoa kulikuwa na sababu gani? Pia hajaeleza ni kwanini Zitto alitofautiana na wabunge wenzake wa CDM wakati wabunge wenzake walikubaliana kususia hotuba ya rais Kikwete bungeni mwaka 2010? Dr. Mkumbo hajatueleza kwanini Zitto alipigania mitambo chakavu ya Dowans inunuliwe?

  Hata kama kikanuni Zitto hajakosea kuamua kujitokeza kugombea urais, kwanini Dr. Mkumbo anashindwa kutuambia kuwa Zitto anataka kugombea urais kwa maslahi ya nani? Au Dr. Mkumbo anataka tuamini kuwa Zitto anafaa kuwa rais? Haitoshi tu mtu kuruhusiwa na katiba (sina uhakika kama katiba ya sasa inaruhusu) kugombea urais bila kutuambia kama anafaa. Anataka kutuambia kuwa Watanzanika hatutambui kuwa Zitto haendani na viongozi wa juu wa CDM?

  Ni uzandiki wa hali ya juu kwa msomi kama Dr. Mkumbo kujengea hoja mambo mepesi kama uliberali katika masuala ya kugombea urais badala ya kujikita katika masuala ya msingi kama kwanini watu hupigania uongozi na kwa malengo yepi. Tumechoka na utaratibu huu wa kiliberali anaouzungumzi Dr. Mkumbo kwani gharama yake tunabeba wananchi hasa tunapowapata viongozi wasiojali maslahi ya umma kwa sababu uongozi waliutafuta kama kitu cha mtu binafsi.
   
 18. M

  Mwanandani Senior Member

  #18
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watakao bainika kweli wana taka kuhujumu chama,tupewe majina yao mapema,tutajua chakuwafanya.
   
 19. Y

  Young zee JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 398
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Thanx mdau, sioni kitufe cha like ila ww jua nimelike post yako.
   
 20. A

  Ame JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Wanapoteza muda nguvu na mali zao..Hakuna fisadi ataingia Ikulu..Its a convenant not even a promise! I am serious with this na wakiendelea will go a step further kuwa paralyse kabisa openly kabla ya wakati....
   
Loading...