Wataka mahakama ya wanawake

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
Wataka mahakama ya wanawake

2007-11-07 10:12:09
Na Godfrey Monyo


Chama Cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), kimeiomba serikali kuanzisha kitengo cha mahakama kitakachoshughulikia masuala ya wanawake.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Bi. Victoria Mandari, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa jukwaa la wazi juu ya maisha ya wanawake lililofanyika jana.

Alisema kuwa kesi nyingi zimekuwa haziripotiwi katika vituo vya polisi kwa sababu akina mama wengi wamekuwa na imani kuwa kesi huchukua muda mrefu, na hivyo hukata tamaa mapema.

Bi. Mandari alisema mfumo unaotumiwa na polisi wa kupokea taarifa za akina mama waliofanyiwa ukatili hadharani katika kaunta, huwafanya wasijisikie huru kutoa taarifa zao.

Alitolea mfano ambapo mama anakwenda polisi kutoa taarifa za kupigwa na mume wake, akifika anatakiwa kutoa maelezo yake akiwa kaunta.

Aliongeza kuwa kama mama huyo atakuwa amepigwa sehemu za siri, akiwa kaunta ya polisi hataweza kuwaonyesha askari ama kusimulia kwa uhuru.

Aidha, alisema hata ukifika katika vituo vyenyewe vya polisi, unakutana na vijana wadogo kiasi kwamba kama mama ni mtu mzima, hatoweza kujieleza juu ya ukatili aliofanyiwa.

Aliongeza kuwa ni vyema kama kungekuwepo na sehemu za faragha ambazo wahusika watafika na kutoa taarifa zao ili wapatiwe msaada.

Naye Bi. Justa Mwaituka kutoka Shirika la Afya, Maendeleo na kutetea Haki za Watoto na Wanawake (KIWOHEDE), alisema wanawake wengi wamekuwa wakifanyishwa kazi za ndani na huku wakifanyiwa maovu mengi, lakini hakuna watu wanaowasemea.

Naye Mkurugenzi wa UTU Bi. Maggi Bangster, alisema kila saa inayopita nchini, msichana ama mwanamke hufa kwa matatizo yanayohusiana na ujauzito.
 
walianza na mahakama ya Khadhi sasa ya wanawake, then ya wakristo, mhakama ya walemavu, mahakama ya waathirika wa ukimwi, mahakama za watoto, mahakama za kikabila nazo zitaombwa yetu macho.
 
Back
Top Bottom