1. kwa case ya simu ya android kujirestart kila mara possible cause and solution ni nini?
2. kama nataka kuweka firmware mpya, napata wapi au zilezile za samsung zinakubali?
snipa tatizo ukifanya recovery mode au download mode menu ni chinese kila kitu mie kichina chali,
kaka c6 simu za kichina zinawekwa firmware kutokana na chip inayotumika, mfano simu yako ni phantom a+ na inachip mediatek 6755h basi inaingiliana rom na simu zoteeee zenye mediatek 6755 hivyo kwanza anza na cpu z idownload halafu cheki specs usome aina ya chip ya mediatek iliotumika halafu tukishaijua tutaanzia hapo
kama recovery yake ya kichina..jarib kuweka custom recovery kama clockworkmod,twcrpthanks chief, ngoja niinstall then ntaleta feedback
Nahitaji kujua na mimi S4 original ntaitambuaje wadau ili nisikamatishwe
Nenda tu Settings>>>>Security>>>>SIM Change Alert
Kama hautokuta sim change alert ujue hiyo sio simu ya samsung
La hasha ukiikuta sogea ndani uone kama kuna sehemu ya kujaza "Samsung account" kama ipo basi jua you are 100% confident kwamba ni original phone...
Hiyo ni siplest test ambayo kila Layman anaweza kuielewa
Dogo kaja na simu yake Galaxy s4 inajirestart kila muda mpaka itakapoisha chaji izimike. mie kwa haraka haraka nikaona hapa naiwekea firmware mpya maana factory reset haijasaidia kitu,
hapo ndio shida ilipoanzia, kabla sijaanza kudownload android 4.4.2 kitkat nikaona kwanza niikague nikaiconnect kwenye pc iliupoanza kuinstall drivers nikaona kitu kama MT-ngapingapi drivers installing nikashtuka ikabidi niinstall aNTutu benchmark test nikagundua kwanza sio original ni clone baada ya kuona ina kitu cha mediatek, sasa hapo ikabidi niwe mpole nikaone nije jukwaani mnipe usaidizi wa maswali yangu yafuatayo
1. kwa case ya simu ya android kujirestart kila mara possible cause and solution ni nini?
2. kama nataka kuweka firmware mpya, napata wapi au zilezile za samsung zinakubali?
waione chief-mkwawa njunwa wamavoko snipa na wengine wote wenye ujuzi wa hizi simu
Aksante mkuu
Ukifanikiwa urudi jukwaani kusema kama una original au fake. Usiingie mitini kama utakuta ni fake.