Wataalamu wa afya wataja chanzo cha usugu wa dawa za antibayotiki

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
pic+wataalam+afya.jpg

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammed Kambi
Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa matumizi ya dawa aina ya antibayotiki kwenye sekta ya kilimo na mifugo yanachangia usugu wa dawa kwa binadamu.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku mbili ulioanza leo jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammed Kambi alisema mkutano huo utajadili kwa kina kuhusu usugu wa dawa za antibayotiki.

Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ikishirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo Shirika la afya Duniani (WHO).

Imeelezwa kuwa mkutano huo ni mwanzo wa kampeni maalumu ya kusimamia matumizi ya dawa aina hiyo.

Alisema usugu huo hujengeka kwa kuwa dawa za antibayotiki zinapotumika kwenye kilimo au mifugo, baadaye huingia mwilini mwa binadamu kwa kupitia mazao ya chakula au nyama bila kipimo na hivyo kujenga usugu.

“Tumewakutanisha hapa wadau, wataalamu kutoka katika maeneo hayo na maeneo mbalimbali kama hayo, kujadili kwa pamoja sisi kama Tanzania tunafanya nini kukabiliana na hali hiyo”alisema Profesa Kambi.
 
Back
Top Bottom