getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wakuu sina sababu ya kuwatusi wataalamu wetu katika Nyanja ya ubunifu na ujenzi serikalini lakini nimekuwa najiuliza maswali ambayo siku zote kwangu haina majibu.! Hivi tatizo letu kubwa ni nini? tumelogwa na nani?
Niliongelea ujenzi mbovu na wa kiwango cha chini wa majengo yetu ya mpakani ambapo ni rahisi tu kulinganisha na yale ta upande wa pili wa Nchi za wenzetu. Mathalani nilitoa mfano wa Jengo letu pale Kyaka Kagera tayari lina hali ya uchakavu wakati lile la uganda lipo imara.!
Mfano wa pili Jengo la Kasumulu mpakani na Malawi ukifika mapokezi jengo letu tayari limechoka na wakati jengo la wenzetu bado imara nawaza hawa watu waliotoa idhini ya ujenzi na kuyapokea majengo hayo bado wapo?
je wakandarasi waliojenga majengo hayo bado wapo?
Tukiacha majengo hayo ni tafakuri yangu kuhusi mradi wa mabasi uanayoenda haraka rapid transit in Dar es salaam maarufu kama mwendo kasi.!
najiuliza je kulikuwa na wataalam walio angalia mchoro na wa barabara na kuupitisha? Yamkini ulikuwa mchoro bora.! Lakini najiuliza kwa akili tu ya kawaida watu hawa walishindwa kuchukua uzoefu wa daraja la zamani la Manzese !? kama kivuko cha waenda kwa miguu..?
nakumbuka walipokuja morogoro kwenye maonesho kabla hawajaanza kuutekeleza mradi huu niliwahi hoji.
Kwanini wanajenga vivuko vya wenda kwa miguu vya kupanda juu kwanini wasitengeneze madaraja ya chini ambapo waenda kwa miguu wangepita chini na magari yakapita juu? Ipi ni gharama kujenga Daraja kama lile la kimara na Ubungo au kutengeneza handaki ambalo watu watapita kwa urahisi?
mathalani kuna wazee kuna walemavu kuna watoto kuna wagonjwa ambao wote wanatumia usafiri huu wa mwendo kasi je ni sahihi na kuwapandisha yale madaraja?!
Wakati bado naendelea kupigwa na butwaa na mradi huu wa DART..
kuna ujenzi wa Stendi ya mabasi au kituo cha mabasi pale kibaha unaendelea kwa style ileile na mazingira yaleyale.. unajiuliza swali lile lile je tuna focus katika mipango yetu?
Au tunafanya kwa sabbu tumetumwa kufanya kazi kwa faida ya watu fulani..
Kibaha ndio Mji ulio karibu na Dare es salaam ambapo kwa wenye kufikiri mara mbili mji huu ndio mahali mabasi kutoka mikoani yalipaswa kuishia ama yanapaswa kuishia ili kukwepa msongamano ya magari katika jiji la Dar..
endapo mabasi yataishia kibaha unatengeza ajira kwa wasafirishaji wadogo kutoka kibaha kwenda katikati ya jiji.
kutoka kibaha kuna njia ya kisarawe kutoka kibaha kuna njia ya bagamoyo.! Ni fursa ya miji hii kukua kiuchumi..
hakuna maono ya namna hii..[emoji52]
ajabu stand ya mabasi inapojengwa na vile inavyojengwa sidhani kama itakuwa tofauti na kituo tu cha daradara haina tofauti na kituo cha mabasi cha ILULA pale Iringa
je miaka 20 ama 10 mbele kituo hicho kitakuwa msaada ama kero ya foleni kwa wasafiri wengine wanaotumia barabara? Kwanini standi hii isijengwe kule ndani kama lilivyonjwa soko la Mnarani?
Wewe uliedhinisha ujenzi huu miaka 30 ijayo je utakuwepo ofisini utaona fahari kwa ulichokifanya?
Sina tusi zuri la kuwapa..!
i dare to say ua all mazwazwa.!