Wataalam wakutana kupitia Wimbo wa Taifa

PNC

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
8,107
14,352
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu leo Mei 10, 2022 jijini Dodoma amekutana na wataalamu wa Ala za Muziki ambao wanapitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye

Wataalamu hao wanaongozwa na Mwalimu Mstaafu wa Shule za Sekondari Alexander Ngonyani ambao wanapitia Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Uzalendo na Wimbo wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kubaini makosa yanayofanyika wakati wa uimbaji na hatimaye kuyarekebisha ili nyimbo hizo ziimbwe kwa usahihi.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Yakubu amesema kuwa Wimbo wa Taifa ni miongoni mwa Tunu za Taifa, hivyo unapaswa kuheshimiwa.

"Nawasisitiza kubainisha makosa yaliyopo kwenye nyimbo hizo, pamoja na usahihi unaotakiwa ili sisi kama Serikali tuchukue hatua ikiwemo kutoa elimu Kwa jamii ili makosa hayo yasirudiwe"Amesema Bw.Yakubu.

Kwa upande wake Mzee Ngonyani amesema kuwa chimbuko la kazi hiyo ni kutokana na kubaini makosa mengi katika uimbaji wa nyimbo hizo unaofanywa na Taasisi, Shule na katika hafla mbalimbali za kitaifa, na tayari ameshawasiliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na BASATA ambao wamepokea utafiti huo ambao na kushauri aonane na uongozi wa Wizara ili kufanyiwa kazi ipasavyo.

IMG_20220510_170152.jpg
 
Usijeshangaa tukaambiwa bajeti ya kupitia wimbo huo ni bilioni 2
Na Cha ajabu pesa ikaenda na wakaja kusema hawajagundua shida yeyote ile
Kama yale ya rangi za bendera ya taifa mwaka ule
 
Nakumbuka wakati lipumba anagombea urais moja ya hotuba zake alisema amipata urais angefuta wimbo wa taifa maana una verses za kikristo na umeimbwa kikristo zaidi. Inawezekana mama anataka atekeleze hilo Mana waislamu Sasa hivi ndo wameteka nchi
Kweli kabisa wameteka nchi hata kwenye iddi zao na mwisho wa mwaka wanapamba ofisi za umma kwa maua na kadi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom