Mkuu, sio Tanzania tu bali takriban ni duniani kote.
1. Wataalam wengi wanapo staafu hujikuta wanaanza aina ya maisha mapya tofauti na kazi za Ofisini e.g. hakuna routine work kama za Ofisini, Hakuna mtu(Boss) anayekufuatilia utendaji wako i.e. husukumwi na yeyote kufanya jambo/kazi n.k. na hatimaye kutolea Taarifa ya ulichokifanya.
2. Wengi hujikuta mwisho wa mwezi wanapata kitu kidogo sana (pension tu) ukilinganisha na alichokuwa akipata alipokuwa Ofisini/mwajiriwa (Mshahara , Night Outs, Allowances, n.k......Kutokana na hilo wengi wanakuwa ni wahangaikaji lakini ramani hazisomi kwa hiyo hawana utulivu wa kuweza kuandika vitabu. Hata hivyo wataandika kwa ajili ya nani?
3. Wengi huwa frustrated kutokana na ile hali kwamba hawana Umaarufu tena katika Jamii na ndo mana hata ww unasema wapowapo tu.
4. Wengi wanakuwa Localised/sedentary i.e. Huwa hawasafiri-safiri sana na muda mwingi wanaonekana kana kwamba wameridhika - sio wachakarikaji kwani kila anachofikiria kinakuwa kama ni too late.