Watu naona mnasuasua, hehe wabongo mkiulizwa swali mnabaki kutaja tu topic, mara utasikia "hesabu, programming, C, microcontroller" ok, ila mbona hamjibu swali, au kama huna jibu si bora ukanyamaza tu kuliko kujaza thread ikafika page ya pili bila jibu.
Turudi kwenye mada, ntaelezea kwa kirefu kidogo, remote control zipo za aina nyingi, lakini niongelee hii ambayo wengi mmeizoea inayotumia Infrared light, remote karibia zote zinatumia logic ileile ila utofauti mdogo sana. Kuna kitu kinaitwa binary digit, yaani 0 na 1, hii ndiyo digital signal, analog yaweza kua voltage level yoyote lakini inafanyiwa abstraction na kua 0 au 1, tuseme voltage yoyote chini ya 2.3V ni 0 na juu ya 2.7V ni 1, kutokana na hilo basi unaweza kurepresent data yoyote, unachofanya ni kucheza na voltage tu ili isome unachokitaka, kama ambavyo wewe unahesabu 1 hadi 10 na kurudi 11, kwa binary digit unaanza 0 - 1 - 10 - 11 - 100 - 101 - 110 - 111 na kuendelea. Kupitia hizi namba unaweza represent information flani kua katika binary, mfano herufi 'a' kawaida hua ni 97 ambayo binary yake ni '01100001', kwa hiyo digital devices yoyote inayosoma ascii ikipata hiyo signal inajua hii ni herufi a.
Sasa kwenye remote inakuaje, unapobonyeza namba fulani, kuna kitaa kinakua kinawaka mbele ya remote, hiki kitaa kinawaka na kuzima kwa speed sana huwezi kuona, TV inauwezo wa kujua kua huyu kabonyeza namba fulani kupitia ule mwanga. Mwanga ukiwaka inakua 1, ukizima inakua 0, sasa ili kujua kua ni command kutoka kwenye remote, TV inakua programmed kupokea Start - Command - Stop, code ya start tuseme ni 110110 na ya kustop ni 111001, unapobonyeza remote inaanza kwanza kuwaka na kuzima kwa speed kuanzisha hiyo start command, tv inajua kabisa kua hiyo imetoka kwenye remote yake, then remote inatoa command sasa, kama ni namba au action flani, then inatoa command ya stop, tv inajua kua remote imemaliza kutuma command, alafu ina-execute ile command uliyotoa, kinachoshughulika na execution ni microcontroller, siingii deep zaidi hii inatengenezwaje maana najua hadi hapa kuna watu nilishawaacha kijijini.
Sasa kwa nini remote haziingiliani, sababu ni abstraction, code iliyokua encoded ya "Start-Command-Stop" sio sawa kwenye TV zote, anayetengeneza TV anajiamulia tu na ku-encode hizi commands anavyotaka. Universal remote kawaida hua zimekua encoded na common commands nyingi ndio maana zinaingiliana na tv nyingi, na nyingine ni programmable, ukiipata mara ya kwanza lazima uiset hadi ubahatishe commands zinazofanya kazi kwenye tv yako. Hapo nimekuelezea zinazotumia infrared light, ofcoz kuna njia nyingi sana za kutengeneza remote, hata sound inaweza tumika, cha muhimu ni ku-encode na ku-decode data kirahisi tu.