Waswahili sanifu, husudu na husda , tupeni tofauti.

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,322
24,192
Tumemsikia mzee Mwinyi akisemanana mhusudu JPM.
Mimi nikifikiri kuhusudu ni kupenda kunako ambatana na matamanio.

Bungeni tunasikia maombi ya kutuepusha na husda.
Hapa ni kama kummind mtu kwa nia mbaya.

Waswahili hebu tupeni undani wa haya manenu, husudu na husda.
 
Kuhusudu ni kupenda kupita kiasi,kupenda kwa kutamani,kwahiyo ndugu mpemba anamtamani huyu m chattle(dooh wapemba barna)...husda ni kamati ya roho mbaya,vijicho wasio na huruma! Kama ilivyo kwa Mwenyekiti na Chama Cha Milele
Nami nikifikiri hivyo, ingawaje mifano ysko ni yako mwenyewe.
 
Samahani sana muanzisha uzi kwanza kabisa hakuna neno Husda bali ni Husuda.
Basi sasa nikirudi kwenye mada tajwa.
1).Husudu;Ni hali ya kupenda kupita kiasi/Sana/kuonea wivu/kuonea kijicho.
Lakini;
2).Husuda;Ni tabia ya mtu kutofurahia mafanikio na maendeleo ya mtu mwingine
 
Labda muanzisha uzi muarab wao hawasemi husuda wanasema husda kwa hiyo maneno yote yanaweza kuwa sahihi
 
Husda au Husuda
inaweza kutumika kwa maana ya wivu uliomzuri
unapenda upate kama alivyopata mwenzako,lkh hauna maana ya kuwa vimuondokee vile uvipendavyo kwake
 
Tumemsikia mzee Mwinyi akisemanana mhusudu JPM.
Mimi nikifikiri kuhusudu ni kupenda kunako ambatana na matamanio.

Bungeni tunasikia maombi ya kutuepusha na husda.
Hapa ni kama kummind mtu kwa nia mbaya.

Waswahili hebu tupeni undani wa haya manenu, husudu na husda.
Kulingana na kamusi,toleo la tatu,husudu kwanza ina maana mbili.ya kwanza ni kuonea mtu kijicho,na ya pili kupenda mno.na husuda,mleta mada wala si husda.Ni mtazamo Wa ubaya kwa mtu na mali yake.au kutopendezwa na mafanikio ya mtu na kuhisi hastahili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom