Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amenasa ujauzito.
Ujauzito huo ni wa aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma, mbunge wa Jimbo la Donge, Visiwani Zanzibar ambapo kitendo cha mimba hiyo kuwa ya mbunge, kimemsumbua Wastara hadi kuamua kuondoka ili akapate muda mzuri wa kutafakari nchini Msumbiji.
Taarifa kutoka katika familia yake, zinaeleza kuwa Wastara alipoondoka nchini, aliwaaga baadhi ya mastaa wenzake kuwa anakwenda kufuata biashara zake za nguo nchini humo lakini waandishi wa habari walipochimba lilichimba waligundua kuwa aliondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutafakari ujauzito huo.
NDUGU AFUNGUKA
Mmoja wa ndugu wa familia ya Wastara amefunguka kuwa baada ya Wastara kuachika, aligundua ni mjamzito hivyo alichanganyikiwa na kuamua kwenda Msumbiji kwa ajili ya kutafakari zaidi ujauzito huo.
“Hakuwa na jinsi kwani akiangalia alishatoka kwa mwanaume, angewezaje kumwambia kuwa ana ujauzito wake? Akaamua kukimbilia huko kwa ajili ya kujipanga ingawa anavyoonekana anatamani amzalie mbunge huyo,” alisema ndugu huyo.
NDUGU AZIDI KUTIRIRIKA
Ndugu huyo alizidi kushusha ‘vesi’ kuwa mimba ya Wastara inasadikiwa kuwa na miezi miwili au mitatu kwani tangu aachane na mumewe huyo, alikuwa akiumwaumwa na wakati mwingine alikuwa akitapika hovyo ambapo mwanzo alificha lakini yalipomfika shingoni alifunguka.
“Alitufichaficha lakini baadaye akawa hana jinsi, akaona atueleze na sisi tumemshauri tu aende akapumzike na ajiandae kutuletea kiumbe kipya,” alisema ndugu huyo.
Wastara alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi, alifunguka:
“Dah! Sijui niseme nini, kiukweli watu wanaongea sana, ni kweli nimeondoka nchini lakini maneno ni mengi, wewe si wa kwanza kunipigia simu. Sikutaka kuongea kabisa juu ya masuala yangu ya ndoa iliyopita wala maisha yangu kwa jumla.”
Mwandishi: Kwa nini unaongea hivyo wewe funguka swali nililokuuliza, una ujauzito au lah?
Wastara: Ndiyo, kwani cha ajabu ni nini? Yule niliyekuwa nalala naye si shangazi yangu, kila mtu anajua niliolewa na aliyenioa (Sadifa) wala si mjomba wangu.
Wastara aliachika Aprili, mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma ambapo ndoa yao ilidumu kwa muda kwa miezi mitatu tu na kuvunjika.
Source: Bongo Movie