Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 25
Zimwi likujualo....pia kuendelea kulindana!
Nimefuatilia kwa muda mrefu suala la uteuzi wa viongozi katika Tanzania nikashindwa kuelewa usahihi wa mtu kustaafu, eneo moja (hasa jeshini) na kisha kupewa madaraka mengine eneo jingine.
Kwa mfano unasikia KANALI MSTAAFU ..... ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa fulani au wilayaa fulani.
Kuna siri gani kuhusu jammbo hili wana JF?
Dah! Ndugu yangu hao wastaafu walio tayari kujifunza toka kwa vijana, may be sio kutoka bongo, kama si Afrika.Kwa mfano wako wa kijeshi, tangu siasa itenganishwe na jeshi imekuwa hairuhusiwi kwa mwanajeshi kushika wadhifa wa kisiasa.Ndiyo maana ikibidi mtu aliye mwanajeshi aingie kwenye siasa, itatakiwa kwanza astaafu jeshi. Wanajeshi hawa hupenda kujulikana kwa vyeo vyao vya kijeshi kama achievement fulani/ title, ndiyo maana unasikia Kanali mstaafu Jaka Mwambi / Jakaya Kikwete etc.
Pia nje ya jeshi kuna dhana kwamba kuna watu wengi wamejenga uzoefu wa siku nyingi sana na kuachiwa wastaafu tu bila kutumiwa, hususan kama nguvu wanazo bado, itakuwa ni hasara, ndiyo maana wastaafu wsio wajeshi wanatumiwa.Lakini hapo hapo kuna vijana wanasema hii inazuia vijana wachanga kupanda ngazi. Hakuna sababu ya kufanya wastaafu wachache wenye rekodi nzuri sana kutotumiwa pamoja na vijana ili vijana wapate kujifunza kutoka kwa wastaafu walio na uzoefu wa siku nyingi na mara nyingine hata hawa wastaafu kujifunza mambo mapya kutoka kwa vijana, as long as hii haiwi tabia inayosababisha damu mpya kukosa nafasi.
Nimefuatilia kwa muda mrefu suala la uteuzi wa viongozi katika Tanzania nikashindwa kuelewa usahihi wa mtu kustaafu, eneo moja (hasa jeshini) na kisha kupewa madaraka mengine eneo jingine.
Kwa mfano unasikia KANALI MSTAAFU ..... ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa fulani au wilayaa fulani.
Kuna siri gani kuhusu jammbo hili wana JF?
Wastaafu wenyewe wana uroho wa madaraka, kama mtu umestaafu kwa nn ukubali kuchaguliwa/kuteuliwa tena? Hivyo mie naona hao wastaafu wanauchu/ uroho wa madaraka.
FOR GOD SAKE eti Peter Kisumo ateuliwa Mwenyekiti wa bodi wa Voda? Ana miaka 74 hivi?
BODI ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, imemteua Peter Kisumo (74) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo.
Taarifa iliyotolewa Jijini jana na Kampuni hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo ulianza rasmi mwezi Aprili mwaka 2009.
Bw. Kisumo anachukua nafasi ya Bw. Ferdinand Ruhinda aliyemaliza muda wake.
Bw. Kisumo ambaye historia yake ilianzia kwenye Vyama vya Wafanyakazi (Trade Union) aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini katika awamu ya kwanza hadi ya tatu.
Kwa mara ya kwanza, aliteuliwa kuwa Waziri kwenye serikali ya awamu ya kwanza mwaka 1964.
Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni Mwenyekiti Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kiwanda cha nguo cha Urafiki, Kiwanda cha Mbao Tanzania (TWICO) na Tanganyika Planting Company Limited (TPC).
Kwa sasa Bw. Kisumo ni Mwenyekiti Mtendaji wa Agro Vet na pia ni Mkurugenzi wa Chama cha Wakulima Tanzania (TFA) na Commercial Bank Africa.
Bw. Kisumo ana mke na watoto watatu na wajukuu kumi--- alistaafu utumishi wa Umma mwaka 2000.
Nafasi kama hizi za kuteuliwa zina madhumuni kadhaa:
1.Kulipa fadhila.
2.Kuua kisiasa maadui zako
3.Kutunza siri za serikali kutoka kwa wastaafu walio wahi kushika nafasi nyeti
4.Kusaidiana. Unakuta wengine wana staafu wamechacha kwa hiyo kama ana connection anapewa nafasi ya kuteuliwa.
5.political strategy. Huyo unayemteua sehemu fulani anaweza kwenda kukufanyia kazi fulani.
Kwa mfano wako wa kijeshi, tangu siasa itenganishwe na jeshi imekuwa hairuhusiwi kwa mwanajeshi kushika wadhifa wa kisiasa.Ndiyo maana ikibidi mtu aliye mwanajeshi aingie kwenye siasa, itatakiwa kwanza astaafu jeshi. Wanajeshi hawa hupenda kujulikana kwa vyeo vyao vya kijeshi kama achievement fulani/ title, ndiyo maana unasikia Kanali mstaafu Jaka Mwambi / Jakaya Kikwete etc.
Pia nje ya jeshi kuna dhana kwamba kuna watu wengi wamejenga uzoefu wa siku nyingi sana na kuachiwa wastaafu tu bila kutumiwa, hususan kama nguvu wanazo bado, itakuwa ni hasara, ndiyo maana wastaafu wsio wajeshi wanatumiwa.Lakini hapo hapo kuna vijana wanasema hii inazuia vijana wachanga kupanda ngazi. Hakuna sababu ya kufanya wastaafu wachache wenye rekodi nzuri sana kutotumiwa pamoja na vijana ili vijana wapate kujifunza kutoka kwa wastaafu walio na uzoefu wa siku nyingi na mara nyingine hata hawa wastaafu kujifunza mambo mapya kutoka kwa vijana, as long as hii haiwi tabia inayosababisha damu mpya kukosa nafasi.
ndo utaratibu wetu,umesahau? c hilo tu.vyeo zaidi ya kimoja je?