Aurora
JF-Expert Member
- May 25, 2014
- 7,308
- 5,272
Habari Zenu Wapendwa
Hii Kauli mbiu ya Hapa Kazi tu, embu ifanyike kwa hawa wastaafu wa PSPF ambao inaendea mwaka sasa wanateseka bila kulipwa mafao yao.
Inajulikana kabisa pesa zao zilienda wapi, na kama zitarudi au hazirudi, hivyo basi Serikali ingechukua hatua stahiki ya haraka kufuta machozi ya hawa wastaafu.
Kitendo cha kukaa kimya bila kulitafutia ufumbuzi kinasikitisha sana, wazee hawa wameitumikia nchi yao kwa Moyo, na sasa muda wa kwenda kupumzika umefika,wanajibiwa kuwa pesa za kuwapa hazipo, si sahihi kabisa.
Wengine wamestaafu lakini bado wana majukumu ya kutunza familia zao, kutolipwa pesa zao mnawafanya waishi maisha yenye stress sana, yatakayoweza kuwapa magonjwa na hata kufupisha maisha yao.
Muwe na Siku njema