Wastaafu tunaungana kupinga sheria na Kanuni mpya ya mafao ya mwaka 2018 Mahakamani

Nyongeza, kama wanaona wastaafu wana haribu pesa wazipatapo kwa mkupuo mmoja, basi selikali ianze utaratibu wa kuwalipa wastaafu mafao yao mapema kabla ya kustafu

Mtumishi akibakiza miaka kumi kufikia muda wa kustaafu, basi aanze kulipwa kwa awamu kumi. Hiyo 75% ilipwe mfanyakaz akiwa kazin na hyo 25% inayobaki alipwe mwaka anao staafu rasmi.

Huko "kuharibu" pesa kukoje?....si mtu anatumia pesa yae halali kununua bidhaa, huduma au kuwapa wategemezi au michepuko? hapo si anakua amechangia kukua na kustawi kwa taifa lake! yani tunafikia hatua ya kuhimiza watu waweke hela wenye masanduku badala ya kuwahimiza watumie ili zizunguke? sasa kila mtu akitumia hela "vizuri" ka kuziifadhi hyo kodi serikali itatoa wapi? na mbaya zaidi mtu alizichangia kwa shida kweli...hapa lazima kuna sababu nyingine
 
Wazo zuri sana. Fatma Karume chukua kesi hii haraka sana, onesha uzalendo. Serikali imegeuka jambazi dhidi ya raia wake.

hahaha...yani wastaafu tutakao umia ni sisi lakini maslai ayapiganie fatma karume?? alafu akimaliza kutupigania atupe mrejesho sisi mabosi zake kwamba amemaliza kazi eeh....alafu tutampigia makofi ya hongeraaa...imaraaa...waaaa! au sio?
 
Ili n'sije nikafa mapema nimeamua nitastaafu mapema sana kabla sijafikia hata hayo masheria mwitu
 
Hizi sheria kichaa hawa wabunge kuna siku nao watakufa kisha waliowabebesha hizi sheria watakataa kuwazika au watafukua makaburi yao kwa hasira wawatukane
 
Maha

Sheria hii ni wizi na ujambazi wa Serikali dhidi ya watumishi.Kimsingi mafao ni malimbikizo ya michango mtumishi na mwajiri,kwa ufupi ni matokeo ya mishahara ya mtumishi.Kanuni ya kutoa 25% ya mafao kwa mkupuo na 75% serikali kubaki nazo kwa sababu nyepesi kama matumizi mabaya ya wastaafu ni sababu za ovyo .Tukutane mahakamani na Serikali kupinga Sheria hii ya ujambazi.Tunataka sheria na Kanuni za zamani zitumike ,ziwe adopted na Pssf na Nssf.hatutaki ujinga sisi.

Huko ni kupoteza muda na raslimali!! MAHAKAMA zetu kamwe haziwezi kukinzana na maamuzi halali yaliyopitishwa na Bunge letu tukufu linalojali maslahi ya raia wa Tanzania
 
Jamani dawa ni kuwanyima kura wabunge woote wa CCM ili wasipitishe hiyo sheria maana ipo wazi serikali inataka tu kuwaibia wanachi walioitumikia kwa miaka dahali
 
Ila najiuliza, kama kweli sheria mpya ya mafao ni nzuri kivile hadi wabunge kuipitisha kwa mbwembwe, itahusu mafao yao pia? Charity begins at home.
 
Sheria hii ni wizi na ujambazi wa Serikali dhidi ya watumishi.Kimsingi mafao ni malimbikizo ya michango mtumishi na mwajiri,kwa ufupi ni matokeo ya mishahara ya mtumishi.Kanuni ya kutoa 25% ya mafao kwa mkupuo na 75% serikali kubaki nazo kwa sababu nyepesi kama matumizi mabaya ya wastaafu ni sababu za ovyo .Tukutane mahakamani na Serikali kupinga Sheria hii ya ujambazi.Tunataka sheria na Kanuni za zamani zitumike ,ziwe adopted na Pssf na Nssf.hatutaki ujinga sisi.
Na wastaf wapenzi wa ccm wanaovaa tisheti na kofia watakuwepo
 
Hii sheria itaanza kutumika kwa wastaaf wa mwaka gani maana mzee wangu kastaaf june mwaka huu km akiskia hii taarifa na hili rungu likimhusu anaweza kufa kwa presha kwa mipango aliyopanga
Muulize kwanza 2015 kura yake alipigia wapi?
 
Watumishi wakiungana na Familia, ukoo wanaweza kabisa kubadili matokeo
 
Mstaafu akisikiliza sheria mpya ya KUSTAAFU na MCHANGO atakaopewa. Akicheki nyumba hata mlango wa mbao hana, anajuta kwanini hata aliiunga mkono CCM miaka yote hio. Sura ya huzuni na kukata tamaa.

Anasikia "Tunajenga SGR" wakati hata hajui nini kirefu cha SGR wala FLYOVER.View attachment 939373

Yani serikali hii imekaa kitapeli tapeli kweli.

Wito wangu kwa serikali, kama wanataka hela ya haraka haraka bila kukera mtu, si waanzishe sera ya kuruhusu WIZARA ziwe zina BET katika MIKEKA.
Cheki waliopigika kimaisha hao
 
Sheria hii ni wizi na ujambazi wa Serikali dhidi ya watumishi.Kimsingi mafao ni malimbikizo ya michango mtumishi na mwajiri,kwa ufupi ni matokeo ya mishahara ya mtumishi.Kanuni ya kutoa 25% ya mafao kwa mkupuo na 75% serikali kubaki nazo kwa sababu nyepesi kama matumizi mabaya ya wastaafu ni sababu za ovyo .Tukutane mahakamani na Serikali kupinga Sheria hii ya ujambazi.Tunataka sheria na Kanuni za zamani zitumike ,ziwe adopted na Pssf na Nssf.hatutaki ujinga sisi.
Mkiambiwa muandamane hamtaki, anashangaa kwani nini mmeachiwa 25% mngepewa5%
 
Back
Top Bottom