Wastaafu pia watakaguliwa vyeti ili kujua uhalali wao kupokea pensheni?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
16,203
27,348
Nimekuwa nikijiuliza,inawezekana hili zoezi likagusa wastaafu pia?

Maana huku mtaani wazee wanaolipwa pensheni na serikali wanahofu kwamba wanaweza kuhojiwa uhalali wao wa kuendelea kupokea pensheni
 
Acha wazee wetu wapumzike bwana. Wewe mzee wa miaka 80 leo umuulize cheti, si unataka afe tu huyo. Unadhani kutunza hivyo vyeti ni rahisi sana ukichukulia mtindo wa maisha hasa ya vijijini enzi hizo?
 
Hahaa,jamaa anawachokoza wazee
 
Nimekuwa nikijiuliza,inawezekana hili zoezi likagusa wastaafu pia?

Maana huku mtaani wazee wanaolipwa pensheni na serikali wanahofu kwamba wanaweza kuhojiwa uhalali wao wa kuendelea kupokea pensheni
Ingekuwa busara kuwaacha hawa wazee wapumzike.Ninaamini wengi baada ya kustaafu hawakujali tena mambo ya vyeti na labda vimepotea au kuharibika.Ni siku nyingi mno zimepita.Ukianza kumkurupusha mzee saa hizi kuhusu cheti labda yuko Bukoba,unataka afe tu,hata kama cheti chake kilikuwa genuine.Atafikaje Dar es Salaam NECTA kwa mfano kukishuhulikia atawaza.Pension yenyewe ni 100,000/=.Nadhani tuwe na limit,tuishie kwa hawa walioko kazini.Tuwaheshimu wazee wetu jamani.

Hata hivyo zamani ku-forge vyeti ilikuwa kitu adimu sana.Ni siku hizi tu mambo yamekuwa mabaya sana.
 
Back
Top Bottom