Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,760
Kauli ya STEVEN wasira kuwa Rais Jakaya Kikwete kukutana na Vyama vya upinzani wwkiwemo UKAWA hakutabadili msimamo wa Wabhnge wa CCM wa serikali 2 iko sahihi kabisa kwa sababu kuu moja nayo ni:
Wapinzani wameitwa na rais, lakini, hata kama angewaita kama Mwenyekiti wa CCM, bado wabunge wake wana haki ya kutokubaliana naye kwa kile atakachoafikiana na wapinzani. Labda hapa niwaulize swali wale wanaobeza kauli ya Mzee Wasira na hasa UKAWA. Muungano wa UKAWA ni Muungano wa MBATIA, MBOWE na LIPUMBA au ni muungano wa vyama vya NCCR, CHADEMA na CUF? Kama jibu ni muungano wa vyama na siyo watu, basi msimamo wa UKAWA kutorudi bungeni ni msimamo wa wabunge wote wa vyama vinavyounda UKAWA. Vivyo hivyo msimamo wa serikali 2 ni msimamo wa Wabunge wote wa CCM na siyo wa JK.
katiba ni ya ccm au ya chadema, nccr au cuf...