Wassira usitafute mchawi wa udhaifu wako ndani ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira usitafute mchawi wa udhaifu wako ndani ya Chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Sep 14, 2012.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KINYWA cha mwanadamu hutamka yale yanayotawala na kuijaza akili yake, ndiyo maana simshangai mbunge wa jimbo la Bunda mkoani Mara ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (mahusiano na uratibu), Stephen Wassira, akitamka kuwa serikali ya chama chake ina uwezo wa kumwomba msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa kukifuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).  Matamshi hayo ya Wassira tunayaona yanakwenda sambamba na Tendwa huyo huyo kuanza kuyatamka kwamba chama kitakachosababisha mauaji, atakifuta lakini kinachosumbua akili ni kwa nini Wassira anaona ni CCM tu ndio inaweza kumuomba Tendwa afute Chadema na si kinyume chake? Kweli tukichambua kwa mapana yake uongozi wa serikali ya CCM umesababisha madhila mangapi kwa Watanzania? Nani ataomba Tendwa akifute chama hiki ili Watanzania wapumue na kufaidiki na raslimali zao?

  Tuyaache hayo. Turudi kwenye kauli ya Wassira. Kwangu mimi, huo ni udikteta, ubinafsi na ubabe ulioijaza akili ya mheshimiwa huyo kiasi cha kuhisi kuwa ana uwezo huo wa kuwanyima Watanzania haki yao ya kidemokrasia ili atimize matakwa yake ya kisiasa bila kujali wala kuheshimu uhuru wa mawazo wa watu wengine, kama ambavyo haki yao kikatiba inavyowataka wafanye bila kuathiri sheria za nchi.
   
 2. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kw amaoni yangu Wassira ni wa kumsikia tu na kuachana nae.......nadhani kuna mambo ya msingi zaidi kwa tanzania yetu hii zaidi ya hizi pumba za huyu babu
   
Loading...