Wassira rudisha pesa za stimulus package | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wassira rudisha pesa za stimulus package

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Mar 19, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Wote tunajua kwamba Katika Namna ya Kipee Bunge la Jamuhuri ya Muungano kati ya mwaka 2008 au 2009 lilipitisha kiwango kikubwa sana cha Fedha za watanzania ili kutuliza mtikisiko wa kiuchumi kwa baadhi ya sekta za kiuchumi nchini uliosababishwa na mtikisiko kiuchumi huko ulaya na America.

  Na pia wote tunajua kwamba Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali alishindwa kujiridhisha juu ya namna mabilioni mengi tu (around 45 Billion) za packahe hiyo zilizotumika.

  Japo hili limeisha zungumziwa humu ndani, leo naomba kukumbusha kwamba, Ndugu wasira ni mmoja wa wanufaika wa pesa hizo isivyo halali.

  Kilichofanyika ni kwamba, Kuna kiasi cha pesa hizo kilitengwa katika kupoza maumivu kwenye sekta ya kilimo cha Pamba, Wanunuzi wa Pamba kutoka kwa wakulima walipatiwa pesa hizo kwa ajiri ya kukata bima kwa pamba ambazo zingekaa store kwa muda mrefu sababu ya kukosekana kwa soko huko ulaya, kilichofanyika ni kwamba wanunuzi wengi wa pamba hawakuzitumia pesa hizo kwa matumizi yalioainishwa badara yake waliingia mikataba ya kifisadi na maadhi ya madalali wa Bima kwa pamba ambazo hazikuwa store wala hazikuwahi kununuliwa.

  Moja ya Kampuni ya udalali wa Bima iliyofaidika na pesa hizo ni GATI INSURANCE BROKERS ambayo inamilikiwa na GATI ambaye ni mjane wa Marehemu Ndege.

  Baada ya kubanwa na kampuni moja ya Bima juu ya mikataba hiyo, mama huyu aliwaambia maafisa wa kampuni hiyo wamtafute steven wasira atawapa cheque.

  Nadhani CAG anaweza akaanzia hapa kuzitafuta zile 45 Billion
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  CCM wote wezi tu
   
 3. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo viongozi wetu ndiyo hao hao wafanyabiashara wa nchi! matokeo yake ndiyo hayo, kila kiongozi ndani ya CCM ni Fisadi!
   
 4. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wasira kumbe mchafu!du!mpaka usomi.
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kumbe na lenyewe jizi???
   
 6. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  c.c.m mafisadi ndio chaka lao.lakini pesa hizo watarudisha tu one day.mbona BAE wamerudisha chenji ya rada.watarudisha
   
 7. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  By the way, STIMULUS PACKAGE imetuibia hela nyingi sana watanzania na hakuna kilichofanyika. Ni vile tu hatuna waandishi wahabari watafiti. Hapo baadae tutagundua wizi mkubwa wa stimulus package na kama hatukuibiwa, basi raisi alitudanganya. Watanzania tumeibiwa sana na watu wachache. Pamoja na jasho la mlala hoi, kuna watu wanaishi peponi hapa hapa Tanzania kwa jasho letu
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  usitupe mawe wakati unaishi kwnye nyumba ya vioo
   
 9. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hapa tunapoongea kuna kesi inawakabiri wauza pamba ambao kama hizi fedha zingetumika vizuri wasingekuwa kwenye matatizo.
   
 10. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Jamani kwani hii ni kweli? Wasira si aliwahi kuwa Waziri wa kilimo lakini! - anawezaje kutumia kampuni ya udalali ya BIMA mali ya mkewe kufanya mambo ya ajabu kama hayo, mimi siamini. Kikwete ni Raisi makini sana sidhani kama analifahamu hilo, kama CAG anaweza kuthibitisha hilo sina shaka JK atalivalia njuga, hawezi kuliacha lipite hivi hivi.
   
 11. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kayataka.
   
 12. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mkuu hiyo ya stimulus package nilisikia muda sana. Nakumbuka ilikuwa kwenye gazeti la Mwanahalisi la muda sana, mmoja aliyetajwa ni Wasira, sio jambo geni kusikia
   
 13. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Usilinganishe BAE na akina Wasira Bae liko nchini Uingereza nchi yenye sheria sio Tanzania nchi ambayo kila kiongozi anatoa amri. Nchi ambayo hata mahakama inaamrishwa na serikali. Wapo wasomi, Mahakimu lakini bado wanaendeshwa utafikiri hakwenda shule kisa kitu kidogo na vyeo, hawapendi kabisa kusimamia taaluma yao.
   
 14. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  If my memories still serves me correctly, nakumbuka Zitto Kabwe aliwahi kumuomba PM bungeni awatajie makampuni yaliyofaidika na STIMULUS PACKAGE na kiasi cha pesa walichopewa. Lakini mtoto wa Mkulima akajiapiza kwa mbingu na ardhi kwamba hawezi kayataja hayo makampuni na pesa walizopata, kwasababau ni SIRI ya makampuni na ma-bank. Kumbe makampuni yenyewe ndiyo hayo ya akina Ghati?!

  CCM na UFISADI NI DAMU DAMU na sera nambari one ya CCM ni kulindana kwenye UFISDI kwa KASI MPYA ARI MPYA NA NGUVU MPYA.

  Wenye pesa (Watanzania walipa kodi) tunataka kujua pesa yetu alipewa nani, leo tunaambiwa kwamba hatuna haki ya kufahamu pesa yetu alipewa nani. Mambo kama haya ndiyo yananifanya kuichukia CCM na kuipenda CDM.
   
Loading...