Haya ni matumizi mabaya ya chombo cha habari cha umma kwa kuwa kipindi wamekipachika jina la 'kipindi maalum' lakini wala umaalum wake hauonekani.
Kwanza sijaelewa anaongea kama serikali au mtu wa CCM maana maneno yake mengi anaonekana kushabikia CCM
Pili huwezi kwenda kwenye TV ya uma kushutumu mtu bila hata kutoa evidence ya unayoyaongea na bila hata kumshirikisha huyo unayemshutumu ili ajibu hizo hoja zako,ni matumizi mabaya sana ya madaraka na kama wanafikiri kwa kufanya hivyo watawa-convince wananchi they are very wrong,wananchi wa miaka ile si wananchi wa leo,hawadanganyiki kwa propaganda za kipuuzi kama hizo.Angejibu hoja za Chadema angalao ningemuona wa maana kidogo