Wassira: Nitagombea urais 2015

Wassira: Nitagombea urais 2015

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,613
Reaction score
6,731
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira (69), ataomba kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Mapinduzi.

(CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Raia Mwema linaweza kuthibitisha.

Katika mahojiano maalumu aliyofanya na gazeti hili mjini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita, Wassira alisema kilichomfanya awaze kufanya hivyo ni maombi mengi kutoka kwa wanaCCM wanaoona anaweza kukabiliana na changamoto zinazolikabili taifa katika wakati huu.

"Kwanza niseme kwamba nimeombwa na watu wengi sana kugombea urais, lakini mimi ni mwanachama wa CCM na lazima nifuate kanuni za chama zinazotuongoza kufanya kampeni.

"Lakini inakuwa vigumu kutofautisha hatua ya kutangaza nia ya kugombea na hatua kama hii ya kuniuliza ili upate habari ya kuandika gazetini.

"Kwa kifupi, nimekwishashauriwa sana, lakini ninasubiri kwanza ruhusa ya kanuni za chama, wakati ukifika nitatoa kauli kuhusu suala hilo la kugombea urais, maana nimeombwa sana.

"Kwa kweli kwa kiasi kikubwa nimeshafikia uamuzi wa kugombea. Nitagombea kupitia CCM," alisema Wassira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bunda mkoani Mara, kupitia chama hicho.

Jina la Wassira limekuwa likitajwa miongoni mwa watu wanaotaka kuwania urais kupitia chama hicho katika uchaguzi huo wa mwaka 2015, lakini hii ni mara ya kwanza kwa Wassira kuzungumzia dhamira yake hiyo na chombo cha habari cha Tanzania.

Akieleza kuhusu nini kinatakiwa kwa Rais ajaye wa Tanzania, Wassira alitaja mambo makubwa manne ambayo yanapaswa kufanyika.

"Kwanza, kuboresha kilimo kwa kuwekeza zaidi katika sekta hiyo ili kuondoa umasikini uliojikita kwa wakulima vijijini na wananchi kwa ujumla.

"Namaanisha kuongeza bajeti ya kilimo itakayotosha kugharimia huduma ambazo mkulima hawezi kujigharimia zikiwamo za utafiti, ugani, uzalishaji mbegu bora na umwagiliaji maji badala ya kutegemea mvua zisizo na uhakika. Hayo yatawezesha kilimo kuwa cha kisasa na chenye tija kwa wakulima.

"Pili, kufufua na kuongeza viwanda vya kusindika mazao ya kilimo nchini. Tunalima mahindi kwa wingi, lakini tunauza mahindi badala ya unga. Zao hilo linahitaji usindikaji ili tufaidike nalo ipasavyo kwa kuuza unga badala ya mahindi ghafi.

"Vivyo hivyo, tuongeze viwanda vya kusindika korosho, pamba, n.k. Tunataka viwanda vi-support (vipige jeki) kilimo. Tukiwa na viwanda vingi vikiwamo vya nguo tutaongeza ajira kwa vijana na kuinua uchumi wa wakulima na Watanzania kwa ujumla.

"Tatu, ni suala la miundombinu. Kwanza katika hili niseme kwamba Rais Jakaya Kikwete anastahili pongezi kubwa kutokana na juhudi zake kubwa za kuwezesha ujenzi wa barabara nyingi katika kipindi cha uongozi wake. Masuala ya ujenzi wa barabara, reli na bandari yanastahili kuwa endelevu hapa nchini.

"Nne, elimu nayo ni lazima. Tunahitaji kupiga hatua zaidi, hasa katika sayansi, maana maendeleo yote ni mazao ya sayansi, hata kilimo ni sayansi. Hili litatusaidia kujiajiri na kumudu ushindani mkubwa uliyopo wa masoko kimataifa," alisema

Majina mengine ya wana CCM wnaotajwa kutaka kuwania urais kupitia chama hicho mwakani ni Frederick Sumaye, Edward Lowassa, January Makamba, Bernard Membe, William Ngeleja na Hamisi Kigwangala ambaye naye amekwishaweka bayana atagombea kama ilivyo kwa January.

Chanzo:
Raia Mwema
 
Karibu Wassira ila punguza jazba katika safari hii maudhi ni mengi
Wasira alipokuwa upinzani aliwatukana sana CCM kuwa ni wezi waliofilisi nchi kwa kuua viwanda na mataahira walioshindwa kuinua kilimo pamoja na fulsa ya atdhi nzuri na kubwa tuliyonayo. Aliwatukana CCM kuwa ni mambumbumbu walioua elimu nchini. Toka amehamia CCM ni zaidi ya miaka 15 na amekuwemo serikalini akishikilia nafasi nyeti za uwaziri lakini hali ndio imezidi kuwa mbaya kabla hajawatukana wenzake akiwa upinzani, sasa umri umemtupa mkono (69 yrs) na naonyesha kuchoka na kufikia hatua ya kulala bumbgeni, kweli Tanzania imegeuzwa kuwa mchezo wa sandakalala !!!
 
ukimuona mtu anaanza kutaja eti watu wameniomba nigombee badala ya yeye mwenyewe kuitaka hiyo kazi kwa asilimia 200% basi hujue huyo mtu ni mufilisi kwani hata akichaguliwa huwa hana chochote cha kuwafanyia wananchi kwani amesukumwa na watu tu kama alivyo kikwete. namsubiri mtu atakayekuja na comprehensive economics plan as well as plan restoring the rule of law in this country which we need the most. mpaka sasa ndani ya ccm naona watu ni wale wale sura zile zile za toka miaka ya 80 hawana jipya.
 
Ccm bado wana kizunguzungu cha nani agombee, dah! itafika wakati hata wanachama wao watabaki hawaelewi nani ni nani. (miruzi mingi humchanganya mbwa)
 
Wassira anazo sifa na ni kiongozi aliye tayari kuwatumikia wanyonge, Goo Wassira Gooo!
 
Wasira alipokuwa upinzani aliwatukana sana CCM kuwa ni wezi waliofilisi nchi kwa kuua viwanda na mataahira walioshindwa kuinua kilimo pamoja na fulsa ya atdhi nzuri na kubwa tuliyonayo. Aliwatukana CCM kuwa ni mambumbumbu walioua elimu nchini. Toka amehamia CCM ni zaidi ya miaka 15 na amekuwemo serikalini akishikilia nafasi nyeti za uwaziri lakini hali ndio imezidi kuwa mbaya kabla hajawatukana wenzake akiwa upinzani, sasa umri umemtupa mkono (69 yrs) na naonyesha kuchoka na kufikia hatua ya kulala bumbgeni, kweli Tanzania imegeuzwa kuwa mchezo wa sandakalala !!!

Mwaka 1995 hakutumia mda wake kukashifu CCM zaidi yeye alijikita kupambana na Warioba. Umri so kigezo cha kumfanya asiwe Rais angalia viongozi wengi Wa bara LA Afrika karibia wrote wanazaidi ya miaka 70 kwa Afya mzee Wasira analipa sana
 
ukimuona mtu anaanza kutaja eti watu wameniomba nigombee badala ya yeye mwenyewe kuitaka hiyo kazi kwa asilimia 200% basi hujue huyo mtu ni mufilisi kwani hata akichaguliwa huwa hana chochote cha kuwafanyia wananchi kwani amesukumwa na watu tu kama alivyo kikwete. namsubiri mtu atakayekuja na comprehensive economics plan as well as plan restoring the rule of law in this country which we need the most. mpaka sasa ndani ya ccm naona watu ni wale wale sura zile zile za toka miaka ya 80 hawana jipya.

Hata mm namuunga mkono na nilishawahi kumshauri agombee simply sitaki ujinga tena akiwa Ikulu najua uongo Wa akina Membe na wenzie wanaomdanganya JK sasa utaisha pia Huyu mzee muonekano wake in tofauti sana na Roho yake
 
Ndg wana JF WASIRA anongelea kilimo ambacho yeye alikuwa waziri wake hatukuona alichofanya zaidi ya kujimegea pesa za pembejeo hatukuona cha kilimo kwanza wala kilimo cha trekta,ulishindwa ukuu wa mkoa mara pamoja na kubebwa na mwalimu, hadi alipochoka na kukuondoa wewe unajua TAASISI YA URAISI ILIVYO MUHIMU au kwa sababu flani amekalia kiti na wewe unaona utaweza? subiri watanzani watazijua tabia zako zote tangu miaka ya 70 na 80 ulivyowasumbua kule MKOANI MARA
 
Wassira hongera sana kwa hatua ya kutangaza nia yako,tunakutakia kila la kheri.
 
Ndg wana JF WASIRA anongelea kilimo ambacho yeye alikuwa waziri wake hatukuona alichofanya zaidi ya kujimegea pesa za pembejeo hatukuona cha kilimo kwanza wala kilimo cha trekta,ulishindwa ukuu wa mkoa mara pamoja na kubebwa na mwalimu, hadi alipochoka na kukuondoa wewe unajua TAASISI YA URAISI ILIVYO MUHIMU au kwa sababu flani amekalia kiti na wewe unaona utaweza? subiri watanzani watazijua tabia zako zote tangu miaka ya 70 na 80 ulivyowasumbua kule MKOANI MARA

Acha kukurupuka kwa kuandika umbea aghaaa! Aliibaa hela alikua Mhasibu Mkuu Wa wizara??? Tens hzo kashfa mnzaziibua ndo mnamzidishia umaarufu
 
Back
Top Bottom