Wassira azidi kumng'ang'ania Bulaya Ubunge wa Bunda, Wafuasi wake wakata rufaa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maombi yao.

Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alisema Jumatano hii kuwa rufaa ya wapiga kura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Acetic Malagila iliyosajiliwa kwa namba 199 ya mwaka 2016, itasikilizwa mfululizo kuanzia Februari 20.

Alisema rufaa hiyo itasikilizwa jijini Mwanza na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Salim Mbarouk, Augustine Mwarija na Shabani Lila.

Katika maombi ya msingi waliyofungua Mahakama Kuu, wapigakura hao wanaowakilishwa na Wakili Constantine Mutalemwa, wanaiomba Mahakama kutengua ushindi wa Bulaya dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Stephen Wasira kwa madai kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka 2015 haukuwa huru na wa haki.

Pamoja na madai mengine, Masato na wenzake wanadai kuwa mchakato wa kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria na utaratibu wa uchaguzi, vikiwamo vitendo vya rushwa, msimamizi wa uchaguzi kumnyima haki Wasira kwa kukataa ombi lake la kura kuhesabiwa upya.

Novemba 17, mwaka jana, Jaji Noel Chocha wa Mahakama Kuu alimtangaza Bulaya kuwa mshindi halali wa uchaguzi huo baada ya kutupilia mbali maombi ya wapigakura hao.

Chanzo: Mwananchi
 
Yaani mzee wangu Wasira bado kabisa haamini anaweza kuwa nje ya system.

Mkuu Wasira kila chenye mwanzo huwa na mwisho, pumzika sasa, hakuna ambacho ulishindwa kufanya kipindi cha nyuma utakifanya sasa, umeshakuwa mbunge kwa vipindi vingi tu, imetosha mzee. Inawezekana labda unawaza ukipata ubunge JPM atakukumbuka kwenye uwaziri, una uhakika mzee? Angekuhitaji angeshakupa ubunge wa kuteuliwa.

By the way awamu iliyopita ulikuwa powerful sana kwenye serekali, wewe na Lukuvi mlikuwa na ushawishi sana kwa JK kama kuna cha kufanya chochote kwa Tanzania ungekifanya/ulishakifanya that time
 
Hivi huyu mzee mshipa wa aibu ulishafyatuka..? Ni aibu kubwa kwa familia yake kwa kitu anachokifanya..!
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Kumbe akikata rufaa wa Chadema siyo kujishushia heshima ila akikata rufaa wa CCM ni kujishushia heshima. Duh....Elimu zingine bwana !!!!!!
Hivi angekuwa baba yako ungemwacha afanye hichi kituko.
Kaazi kweli kweli..
 
Ni vyema Mahakama hiyo ikawalazimisha watu hao wanne kuweka cash deposit ya sh 2 bn kama garama ya kesi iwapo wakishindwa.
Kuna wale watu watatu ktk kesi ya Lema baada ya kushindwa mara ya mwisho waliingia mitini hadi leo mahakama haijalipwa garama ya kesi ile. Mawakili wa Bulaya wakazanie hilo kwa kutaja precedent ya kesi ya Lema.
 
Anaugua Uchese ( Ukosefu wa Cheo Serikalini). Anajidaigi "taisoni" kupambania madaraka lakini kwahili anajiaibisha mno
 
Kuna viumbe wana roho ngumu aisee!...huyu kiumbe anayemng'ang'ania Bulaya ni wa kipekee!...Na kwa upepo wa Leo unavyovuma mahajamani hasa juu ya wapinzani, sitashangaa maamuzi yatatolewa yatakayo waumiza wana Bunda!....nisiwe mrithi wa Shekh Yahya. Navuta kiko changu, naongeza Tumbaku navuta taratibu nikisubiri siku ya siku
 
Back
Top Bottom