Wassira atimka na daftari la wadhamini

Wassira atimka na daftari la wadhamini

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,504
Reaction score
8,253
Katika hali ya kusikitisha mbunge anayemaliza muda Bunda wake mzee Wassira jana saa 1:30 asubuhi alienda kujaza daftari la wadhamini baada ya kujaza aliondoka nalo ili wagombea wengine wasijaze.

Mgombea CHADEMA Esther Bulaya alifika kujaza daftari hilo na kukuta daftari hilo halipo hali iliyozua sintofahamu, mwanamama Bulaya alichanganyikiwa kwa kweli na kusababisha kuhaha!

Baada ya mambo kuwa magumu ilibidi watu wazame kwenye sheria na ndipo wakaja na style ya kumuuliza Esther kama ana vitambulisho vya wadhamini wake bahati nzuri alikuwa navyo na jahazi likawa limeokolewa.

Hii ndo ilikuwa mbinu ya mwisho kwa Wassira na kwa kuwa imeshindikana i basi tena make kwenye sanduku la kura Wassira hamuwezi Bulaya.

Katika kupiga story na mzee mmoja wa CCM hapa jimboni kuhusu haya mambo ya uchaguzi, mzee huyo alifunguka 'tulimuambia mzee Wasira apumzike amuachie huyu binti lakini akawa mbishi, sasa mambo yameharibika huyu binti kaenda upinzani na ndio wanabunda tunayependa atuongoze sote vijana na wazee, huyu binti katufanyia kazi kwa kweli, katusaidia sana wazee katika suala matibabu, hapa wa kulaumiwa ni Wassira mwenyewe kwa chama kupoteza hili jimbo'.
 
Mzee kajichagulia kaburi lake mwenyewe, acha azikwe October na chama chake.
 
mambo anayonya wasira huko bunda ni aibu sana kwa kweli. sijui huo uwaziri aliupataje. kule bunda amemweka mfukoni mkurugenzi wa halmashauri wa bunda ili kila anachokifanya yeye kisipingwe.
 
Steven-Wasira.jpg
Bulaya-20July2015.jpg
 
Jamani Wasira.......sasa itakuwaje......?......anapeleka wapi daftari........
 
Tanzania mambo yanaenda kienyeji sana, sasa alichofanya Wasira kama ni kweli sio kosa kisheria?? Na kama ni kosa si alitakiwa awe exempted kwenye kinyang'anyiro???
 
ukiwekeza mawazo yako kwenye viposho posho hivi...siku ukijua mrija unaelekwa khziba ndo mwanzo wa kurukwa na akili....
Tyson pamoja na uzee ule bado anayoyafanya ni comedy za kitotoo
 
daftari la wadhamini ni mali ya serikali, mtu kuondoka nalo ni kuvunja sheria, bunda hakuna polisi? hawakupewa taarifa? au ndio kawaida ya bora liende?
 
Mtu wa karibu kabisa na mzee tyson ananidokeza kwamba hii ndo ilikuwa mbinu ambayo mzee alikuwa anaitegemea baada ya ile ya kumpandikiza yule jambazi kuwa mgombea wa chadema kugonga mwamba
 
daftari la wadhamini ni mali ya serikali, mtu kuondoka nalo ni kuvunja sheria, bunda hakuna polisi? hawakupewa taarifa? au ndio kawaida ya bora liende?

Hukuona pale busega waziri kamani alimrukia kichwa kimo cha mbuzi mtangaza matokeo tena mbele ya polisi lakini matokeo yake polisi ndo wakawa wanamuomba radhi mheshimiwa huku wakimsihi aache
 
Hukuona pale busega waziri kamani alimrukia kichwa kimo cha mbuzi mtangaza matokeo tena mbele ya polisi lakini matokeo yake polisi ndo wakawa wanamuomba radhi mheshimiwa huku wakimsihi aache

Halafu mkuu wa wilaya anasema eti ni makosa tu ya kibinadamu!Wakati ni uvunjifu wa amani na ukosefu wa maadili.
 
Back
Top Bottom