nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:16 NA MWANDISHI WETU, MEATU
SERIKALI imeunga mkono wazo la Waziri Mkuu (mstaafu), Edaward Lowassa kwa kukiri kuwa endapo hakutakuwa na mkakati thabiti wa kushughulikia tatizo la ajira kwa kundi la vijana kuna hatari kubwa ya kuleta machafuko katika siku zijazo.
Kauli hiyo ilitolewa na juzi wilayani Meatu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu Stephen Wassira alipozungumza na viongozi wa wilaya hiyo ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Simiyu.
Wassira alitoa matamshi hayo huku kukiwa na kauli kadhaa ambazo zimekuwa zikitolewa na Lowassa kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni sawa na bomu.
Akizungumza na viongozi wa Meatu mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi wakiongozwa na Mwenyekiti wake Rossemary Kirigini, Wassira alisema tatizo la ajira kwa kundi la vijana ni kubwa na linatishia amani hivi sasa.
Asilimia 60 ya Watanzania ni vijana na hawana ajira hivi unategemea nini ndiyo maana wakiambiwa kuna maandamano wao hawaulizi maandamano hayo ni ya nini wanachouliza yanaanzia wapi.
Hatuwezi kuwa taifa huku kundi kubwa la watu ambao ni vijana halina kazi hivyo kama viongozi lazima sasa tuchukue hatua mbalimbali kwa kutumia fursa tulizo nazo tuhakikishe tunapambana na changamoto hii, alisema Wassira.
Kwa sababu hiyo alitaka kupitia Tasaf awamu ya tatu pamoja na kulenga kuwezesha familia masikini kwa ajili ya kuwaongezea kipato kupambana na umasikini.
Pia alishauri halmashauri nchini kote zihakikishe zinahamasisha uundwaji wa vikundi vya vijana vya uzalishaji mali ambavyo vitawezeshwa ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Alisema serikali imechukua hatua mbalimbali ambazo zitawezesha kukabiliana na tatizo hilo la ajira kwa vijana hasa kwa kutumia mkakati wa Kilimo Kwanza.
Kwa mkakati huo vijana kujiunga katika vikundi watawezeshwa kupata zana za kisasa za kilimo kumudu kulima kisasa na kuzalisha kwa tija na kupata kipato kwa ajili ya kupambana na umasikini.