Wasomi, wanaharakati walilarua Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi, wanaharakati walilarua Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jul 31, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  •Waonya ushabiki wa kisiasa, wataka kikao cha haraka

  na Lucy Ngowi

  KUIBUKA kwa vurugu bungeni kwa nyakati tofauti Jumatano na Alhamisi ya wiki hii, na kusababisha wabunge watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutimuliwa ndani ya Bunge, kumeibua hoja nzito nje ya Bunge.

  Wakati CHADEMA wao wakidai hali hiyo imetokana na uongozi mbaya ndani ya Bunge, Chama cha Mapinduzi (CCM) wamewatupia lawama wabunge wa chama hicho, kadhalika wasomi nao wakionya juu ya ushabiki wa kisiasa.

  <b>Kauli ya wasomi</b>
  Wasomi na wanaharakati mbalimbali nchini, wameutaka uongozi wa Bunge ukutane kwa haraka ili kushughulikia malumbano yaliyopo kwenye vikao vya Bunge vinavyoendelea hivi sasa.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wasomi hao na wanaharakati walisema kuwa kuendelea kwa hali hiyo, kutawafanya wananchi wapoteze imani kwa Bunge lao wanaloliamini.

  Msomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika Idara ya Sayansi ya Siasa, Bashiru Ally, alishauri wasimamizi wa Bunge watoe maelekezo stahiki kwa wabunge waliopo kwani kauli zao ama vitendo vyao vina athari za muda mrefu.

  “Suala hili la ushabiki wa kisiasa, chuki binafsi viongozi wa Bunge watawajibika, inawabidi wafanya kikao waliangalie suala hili kwa undani, kwani ni zito ili waweze kurudisha imani kwa wananchi,” alisema.

  Kwa upande mwingine alisema kuwa wabunge ni viongozi wa wananchi, hivyo matendo, kauli, mavazi ama kusinzia kwao bungeni, vinawaathiri. Kama viongozi wa siasa watahukumiwa kwa matendo yao.

  Msomi huyo wa UDSM, alisema hali inayoonekana hivi sasa, inawezekana tabia za wabunge, matakwa na fikra zao zina msukumo zaidi kuliko taratibu zilizopo, na pia kuna aina fulani ya Bunge kushindwa kusimamia kwa kanuni zilizopo.

  “Viongozi wasipokuwa makini, Bunge litapoteza imani kwa wananchi, kwa kuwa matarajio ya wengi ni kuona mijadala inaendeshwa kwa uhuru na hoja.

  “Matokeo imani yao itashuka. Mbele ya safari maamuzi yanayotolewa na Bunge yanaweza yasiheshimiwe na wananchi,” alisema Ally.

  Alieleza kuwa inawezekana kuwa kuwepo kwa hali hiyo ni kutokana na kanuni kupitwa na wakati au kuna ukiukwaji wa makusudi au hakuna taratibu.

  Msomi mwingine, wa UDSM kutoka idara hiyo hiyo, Profesa Gasper Mushi, alisema kuwa anachokiona hivi sasa, ni kwamba Bunge limepoteza mwelekeo na kuacha kusimamia mambo muhimu, na badala yake linasimamia mambo binafsi ya vyama.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Uongozi, Hebron Mwakagenda, alisema kuwa mambo yanayoendelea bungeni hivi sasa ni utoto wa kichama, kwa kuwa uanachama umezidi, yote hayo ni kwa sababu hakuna maslahi ya taifa bali ya chama.

  “Watu wasiotarajiwa kufanya hivyo, wameingia kwenye mtego huo. Nchini India mtu akichaguliwa kuwa mbunge anakwenda chuoni kwa ajili ya kufundishwa jinsi ya kutawala,” alisema Mwakagenda.

  Alisema, kinachotia moyo hivi sasa kuna fursa ya kutengeneza Katiba mpya ambayo itaainishwa ni nini cha kufanya kwa ajili ya maslahi ya taifa.

  “Acha utoto uendelee hapo ndipo tunachuja chuya na mchele, ili tujue viongozi bora ni kina nani,” alisema mkurugenzi huyo.

  <b>Dk. Slaa asikitishwa </b>
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa malumbano ya dhahiri yanayoendelea hivi sasa bungeni baina ya viongozi wa Bunge, wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala cha CCM, ni matokeo ya uongozi mbaya ndani ya Bunge hilo.

  Slaa alisema hayo alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima, kuhusu malumbano yanayoendelea katika Bunge linaloendelea mjini Dodoma.

  “Nafikiri kama uongozi wa Bunge hautabadilisha mwelekeo wake wa kuilinda CCM na serikali, hali hiyo haitavumilika, kwani Bunge haliongozwi kama mtu anavyotaka, akiamka siku hiyo.

  “Kwa mfano jana (juzi), Naibu Spika wa Bunge tokea asubuhi alisema atawatoa watu, na kweli aliwatoa mpaka nje ya geti. Lakini ukiangalia kauli hiyo ya Ndugai, haikuwa popote,” alisema Slaa.

  Slaa aliongeza kuwa hata katika hotuba ya wapinzani iliyosomwa bungeni, hakuna jambo lolote lililozungumzwa kule ambalo halipo, kwani yote yaliyozungumzwa ni ya kweli.

  “Kusema ni uchochezi ni kinyume cha kutoa uhuru kwa kila mtu,” alisema Slaa.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, mambo yote yanayotokea bungeni ni dalili ya kuwa uongozi wa Bunge uliopo hauna uwezo wa kuongoza Bunge la vyama vingi, ama kwa tafsiri nyingine, wanalinda serikali, matokeo Bunge litafika mahali pabaya.

  “Nimepigiwa simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, tunapongezwa, wanasema tuongeze nguvu na vijana walioko bungeni waongeze nguvu.

  “Wajue kazi ya vyama vya upinzani si kupiga makofi bali ni kukosoa serikali. Tusifike mahali tusilaumiwe kuwa vijana wetu wanaleta vurugu. Kanuni zipo wazi, tafsiri hazitegemei jinsi Naibu Spika alivyoamka siku hiyo,” alisema.

  Alisema kuwa utaratibu uliopo hivi sasa wa spika wa Bunge Anne Makinda na naibu wake Ndugai, kuomba uthibitisho kila siku kwa mambo mbalimbali yanayozungumzwa bungeni na wapinzani na pale unapotolewa haufanyiwi kazi, ni sawa na kufanya mazingaombwe.

  “Vijana wangu karibia saba waliambiwa watoe uthibitisho wa yale waliyoyazungumza, lakini walipowasilisha vielelezo, Spika na wenzake wamekaa kimya. Wanatafuta visingizio vya kupotosha ukweli. Uthibitisho unapopelekwa unawekwa kwenye kabati,” alisema Slaa.

  NCCR nao wazungumza. Naye Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema kuwa kinachoendelea bungeni hivi sasa ni matokeo ya mfumo mzima uliopo.

  Alisema, ili mtu apate haki yake inabidi apambane, kwa kuwa mfumo tuliojikita ni wa kifisadi, umeacha pengo kubwa kwa walichonacho na wasichonacho.

  “Hali hii ni matokeo ya mfumo mzima uliopo, mfumo wa biashara ama mfumo wa siasa, ili upate haki yako hapa nchini inabidi upambane,” alisema Mbatia.

  Aliongeza kuwa vyombo vya kufanya maamuzi vinaonekana havifanyi kazi zake vizuri, athari yake ni maangamizi kwa taifa.

  Mbatia alisema Bunge ndiyo linasimamia serikali na kuishauri, lakini kinachoonekana hivi sasa, hakuna kuaminiana kati ya Bunge na serikali.

  Alisema, kinachoonekana bungeni hivi sasa watu wana shauku ya kuzungumza lakini wanaminywa uhuru huo, na wengine wanapata nafasi ya kuzungumza wanachotaka.

  <b>CCM watoa taarifa </b>
  KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es salaam Kilumbe Ng’enda amesema kuwa vurugu, utovu wa nidhamu, jazba na ubabe vinavyojitokeza kwa baadhi ya wabunge katika kikao cha Bunge mjini Dodoma haionyeshi kuwa dhana ya kupata wabunge wenye sifa imezingatiwa.

  Katika kikao chake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema kuwa vitendo vinavyofanywa bungeni na baadhi ya wabunge vinawatia aibu wanasiasa wote ukiacha tofauti zao za kiitikadi.

  “Tunataka wabunge watulie kwenye viti vyao na wafanye masuala ya msingi kama walivyoagizwa na wananchi wao na si kuendekeza masuala yasiyo kuwa ya msingi,” alisema Ng’enda.

  Aidha alisema kuwa hatua hiyo ya baadhi ya wabunge kukosa nidhamu ya kutofata taratibu walizojiwekea wawapo bungeni ni kielelezo cha wazi kuwa vyama vyao havikuwachuja vizuri na wananchi hawakupata walichokusudia.

  Hata hivyo alitetea vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi bungeni akisema kuwa CCM na serikali yake ni vyombo vya wanadamu na vinaongonzwa na wanadamu hivyo hutegemei yasiwepo mapungufu na kwamba ni ukweli na imani kuwa kazi ya mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke haikosi mapungufu.

  Kutokana na hilo Ng’enda alisema katika kuchagua viongozi unatafuta yule ambaye hata kama ana mapungufu ni bora kuliko wenzake, na hali hiyo imejidhihirisha bungeni kwa sasa kuwa wabunge wa CCM ni afadhali kuliko wale wa CHADEMA.

  “Hivi unaweza ukaunda serikali yako ukaletewa jina la Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini ambaye ndiye Waziri Kivuli wa mambo ya ndani iwapo CHADEMA ingeunda serikali, tutategemea ndiye angekuwa waziri wa wizara hiyo?

  “Ungeletewa jina la Shamsi Vuai Naodha Waziri wa mambo ya Serikali, unaweza kweli ukaamua Waziri awe Lema? Ambaye anaweka Jazba, Kiherehere na Ubabe kama vitendea kazi muhimu vya akili yake sidhani!” alisema Ng’enda.

  Ng’enda aliwapongeza wabunge wa CCM na viongozi wote wa Bunge, akimpongeza kwa kumtaja jina mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe ambaye alisema kuwa aliona uchungu na nje ya Bunge aliwaaasa wabunge wenzie waliotoka nje baada yu kutolewa mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje kwa amri ya mwenyekiti.

  Alimalizia kwa kumkumbusha Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni awe kweli ni kiongozi wa wapinzani na kwamba aonyeshe hilo kwa kulaani vitendo vya wabunge kukosa nidhamu wawapo bungeni.
   
 2. ZigiZaga

  ZigiZaga JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 784
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 180
  Hivi unaweza ukaunda serikali yako ukaletewa jina la Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini ambaye ndiye Waziri Kivuli wa mambo ya ndani iwapo CHADEMA ingeunda serikali, tutategemea ndiye angekuwa waziri wa wizara hiyo?
  "k
  uuwa watu ka risasi kwako neema,utaona kama huo m/kiti wa magamba 2015 utaupata tena kama si kunyea debe!acha jembe liitwe jembe.PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSS!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  ukweli wabaki ya kuwa CCM hivi sasa ndiyo tishio la usalama wa taifa hili kwa kukumbatia ufisadi na ubinafsi uliokithiri mno................dawa ni tukubaliane kuifuta ccm kwenye sheria za nchi na mali zote zirudishwe serikaalini kama kweli tunataka kuzalisha demokrasia inayojali utu wa raia wote............
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  nyimbo za ukombozi ndiyo zenye mashiko kwa sasa, ccm wametumia hiyo wanayoiita lugha ya kibunge kwa zaidi ya miaka 30, leo nchi haina umeme, hata sukari ni taabu, nini faida ya lugha hiyo, kama wabunge wa cdm, cuf, ..... mtaipitia hii mistari nawashauri msifungwe na matumizi ya hiyo lugha ya kibunge. inatutia hasara watanzania.
   
 5. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ipo haja ya wapinzani wa kweli walio nje ya bunge kutafuta na kutumia kila nafasi kurudia kusema na kusisitiza misimamo ya upinzani bungeni. Kwa maoni yangu hizi propaganda za ccm kila mahali ktk vyombo vya habari bado zinawapotosha baadhi ya watanganyika. Mfano mtu anamvika Lema ubaya, lakini ukimwambia aonyeshe ubaya kwenye hotuba ya Lema hana cha kuonyesha! Kwa mtu asiyechambua mambo (kumbukeni bado wengi hawaangalii bunge sababu ya majukumu, umeme nk), akisikia tu wamechochea, watovu wa nidhamu nk bila kupewa upande wa pili ni rahisi kudanganyika. Angalieni pia upotoshaji unaofanywa pia na vichwa vya habari kwenye vyo vingi vya habari juu ya matukio ya bungeni.
   
 6. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #6
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lema ningempa uwaziri mkuu!
   
 7. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Do! Hii kali
   
 8. S

  Smafuru Member

  #8
  Jul 31, 2011
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  At the end of the day tutashuhudia minyukano humo bungeni,we were right to vote 4'em but they're wrong 2 sacrify their personels toward sitting allowances ! Imagine wanatumia bil 506 p.a waache kusema NDIYO ? Leo project ya railway ambayo R.O.I iko wazi viable tunaicha inakufa..kumbe kunge re-invest hii posho au kulipa mishahara railway ingekuwa wapi ! ?.TUKOKOTOE-watumishi wote nchini last year walilipwa bil 1.2 kumbe sitting allowance ya bil 5.6 ingeweza kulipa mishahara ya watumishi wote wa railway kwa miaka 4 mfululizo regardless wanazalisha au hapana....leo wanafanya fujo bungeni (does this click into our heads ? ? )
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Ni heri ya vita inayodai haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu.......by GL
   
Loading...